Hotuba ya Kihistoria ya huyu Bwana Harusi

Hotuba ya Kihistoria ya huyu Bwana Harusi

Mtamile

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
2,838
Reaction score
1,274
MC: Na sasa tupate maneno machache kutoka kwa Bwana Harusi.

Bwana Harusi: Asante MC, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa kumuumba mke wangu, kwa hilo Mungu uko juu.

Pili, nimshukuru baba mwenye nyumba wangu kwa kukubali niwe na deni la kodi ili kufanikisha harusi hii.

Naomba nitoe shukrani kwa bosi wangu kwa kunipa likizo fupi ili nikamilishe shughuli hii.

Naishukuru kamati yangu ya harusi kwa kuwezesha kukusanya fedha zilizofanikisha harusi hii, nimshukuru mke wa kaka yangu kwa kutuazima gauni la harusi, na kaka yangu kwa kuniazima suti hii niliyovaa.

Natoa shukrani kwa mtengeneza keki kwa kutuazima keki, nitairudisha keki kwako kesho kama tulivyokubaliana.

Nawashukuru wazazi wangu kwa kuja na kikundi cha ngoma toka kijijini, kweli kimeziba pengo la burudani katika harusi hii.

Naishukuru kamati ya wazee wa kanisa kwa kufanikisha kumshawishi mke wangu aolewe na mimi, niwape aksante akina mama jirani kwa kuja na vyakula toka makwao ili kufanikisha harusi hii, na vijana kwa kuja na pombe za halali na haramu mradi harusi hii ni furaha tupu.

MC, wewe ni rafiki yangu, nashukuru kwa kukubali tulipane kidogokidogo.

Aksante sanaaaaa.
 
Harusi poa sana,sasa huo mchango umetumika wapi?
 
Hahahaha bwana harusi katisha jamani, hhha harusi kujipanga kwa kweli

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
kwan alilazimishwa jaman au ndo alifanywa ndondocha ili akamilishe ndoa,harus za mikopo ni nying sana co yy tuu
 
He hii nayo kiboko, bi harusi ana moyo mana mpaka madeni yaishe, na watoto atakua keshazaa
 
Alilazimishwa kufanya harusi nini maana naona kila kitu sio chake unaweza kuta hata mke ameazima ili kuonyesha watu kama ameoa.
 
Haahaa! Nimependa hapo kwenye keki! Kwahiyo hamna kulishana hapo! Daa !
 
Namshukuru sana baba mkwe kwa kukubali kupokea mahari ya fedha feki!
 
Ni kweli tupu hata mimi na mke wangu tunamdai pete za ndoa alsema akishafunga tu ataturudishia jaman mwee!
 
Back
Top Bottom