Hoteli ya Serena na Siasa za upinzani Tanzania!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,951
29,533
Wadau hebu tujiulize kwa nini Hoteli ya Serena inapendwa sana hasa hasa inapokuja maswala mazito mazito ya kisiasa tena siasa za upinzani.

Ukifuatilia humu jamvini unaweza kukuta hoteli hii ni hoteli iliyotajwa mara nyingi sana kwenye matukio na harakati za kisiasa.

Baadhi ya matukio ni pamoja na

1-Zitto Kabwe kusigana na hatimaye kuachana na Chadema.
Hapa Hoteli hii ilitajwa sana kwenye vikao vya siri hadi vya wazi.

2-Dr Slaa alivyoanika ushenga wa Gwajima na yaliyojiri kwenye kamati kuu ya Chadema juu ya uamuzi wa kumpokea lowassa.

3-Sumaye kutangaza kujitoa CCM

4-Lowassa kutangaza kujitoa CCM na kutangazwa kuwa mgombea wa urais kupitia Chadema.
5- lipumba kutangaza kujiengua uwenyekiti wa CUF.

.........MATUKIO NI MENGI

6-Maalim Seif kwenda kujipumzisha Serena wakati wa marudio ya uchaguzi Zanzibar.

Hebu taja tukio la kisiasa nililosahau lililotokea hapo Serena...halafu jaribu kudadavua kwanini hii ni hoteli maarufu kwa siasa za Tanzania?
 
Taja na ubungo plaza shuhuli nyingi hufanyika pale hata Makonda alimchapa makofi Mzee Warioba pale.
Hata Sugu naye alishafanya yake hapo...teh teh teh...sidhani kama Ubungo plaza inaweza kuvunja rekodi ya Serena kwa matukio ya kipekee katika siasa za upinzani
 
Nina mashaka na kumbukumbu zako kama ziko sawa, Lipumba, Lowassa na Sumaye nina mashaka kama walitumia hotel hizo. Hi ya kusahau sahau nakuchanganya mambo ndio ambayo ccm hua wanaipenda sana kwetu Watanzania.
 
Back
Top Bottom