Geza Ulole
Platinum Member
- Oct 31, 2009
- 76,397
- 108,095
Wana JF,
Mimi binafsi sijafurahishwa na kitendo cha Mh John Magufuli kupinga ujenzi wa nyota Tano unaotaka kufanywa na Tantrade. Kwangu mie ule ni ukiritimba na ujuaji usio na tija. Hulka ya walimu wengi. Kwanza Mh Magufuli anapaswa kujua taasisi ya Tantrade imejikita na kubobea kwenye kutoa huduma yaani service provision entity.
Pili Mh anapaswa kufahamu Jiji la Dar lina vyumba vichache vyenye hadhi vya kulala wageni ukilinganisha na majiji mengine Africa yenye watu wanaokaribiana nasi kama ya Nairobi ama Addis Ababa na hata Zanzibar yenye watu wachache. Kama tunataka Dar iwe kitovu cha biashara kuunga mkono jitihada zake za uchumi wa Viwanda na miundombinu, basi yapaswa kuwapo na jitihada za kuwezesha multiplying effect ya juhudi za uwekezaji wa viwanda.
Kwa mfano mbali na ajira zisizopungua 150 za moja kwa moja kutoka kwa mradi wa hoteli ya nyota tano kwa waliosomea kozi za utalii na usimamizi wa hoteli, unapojenga kiwanda cha nyama ama cha vinywaji ama kilimo cha horticulture mteja wako mkubwa ni mwenye hoteli. Ukiachia mbali wenye viwanda vya detergents ama hata mahali pa kukutania wenye kutaka kuwekeza.
Tatu kurudisha gharama zile za mradi wa mabasi ya mwendo kasi, mradi wa barabara za juu, mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwl. Nyerere awamu ya tatu, mradi wa upanuzi wa Bandari na zile ndege za ATCL anazonunua ambazo itabidi zije kujaa abiria basi moja wapo ya sekta inayoweza kuwezesha hilo ni utalii utakaingizia nchi mapato ya kodi za uhamiaji. Huduma na miundombinu bora ni vivutio vya Utalii wowote ule duniani.
Utalii uwe mikutano ya kibiashara, ya kiafya ama chochote kile tukiachia mbali utalii wenyewe wa majiji wa kihistoria ama makumbusho ama kuwapa malazi wafanyabiashara wakubwa wa nchi jirani watakaokuja kutumia Bandari yetu ya Dar es salaam. Ni sekta chanya kwa mustakabali wa ukuaji wa uchumi wetu unaochangiwa na sekta ya huduma kwa asilimia kubwa.
Nne ujenzi wa hoteli utatoa ajira za muda kwa kampuni za ujenzi na usanifu mbali na kutoa soko kwa viwanda vya kutengeneza nondo, saruji na hata wenye kutoa huduma ya usafirishaji.
Naomba Mh. aache kasumba ya ujuaji wa kuingilia mamlaka na maamuzi ya kila idara kwa vile tu ni Rais. Urais una mipaka na Idara na taasisi zilizopo zina mamlaka ya kuamua uwekezaji bora kutokana na miongozo wa Taasisi wanazosimamia ku-complement uzalishaji wa viwanda anavyopigania kwa nguvu zote. Kama Tantrade imeandikisha mikataba ya mradi huu itawapasa kulipa fidia kwa kampuni zolizokuwa zijenge hoteli hii. Kisa pingamizi la Mh.
Service sector ni muhimu kwa nchi pia. Si sawa kulazimisha taasisi za kutoa huduma kujenga kwenye uzalishaji sidhani kama kufanya hivyo kutaleta tija ya mwendelezo wa kudumu kwenye kuendesha miradi hiyo. Hili ni angalizo kwako Mh. tusije jikuta na miradi ya hoteli za kata zisizokidhi viwango hapo baadae.