yohana charles
Senior Member
- Mar 21, 2013
- 134
- 10
Hapa niko hospitali ya rufaa Mbeya,kuna wagonjwa ambao wamefika tangu saa 1,mpaka sasa ni saa 4 bado huduma hazijaanza eti madaktari wapo kwenye kikao...kiukweli napata tabu kupata jibu kwamba..>ni kwa nini vikao vinafanyika muda wa kazi?wakti huohuo ikifika saa 6 tu watasema muda wa lunch...hivi ni lini watanzania tutajali muda? aah Tanzania ingekuwa daladala tungeshuka wengi tukapanda daladala nyingine.!
nimekupenda je?kwa jibu zuri maana hakuna wa kumlaumu mwenzake wakati tulichagua wenyewe.Unalalamika hivyo kumbe kwenye uchaguzi uliwapa ccm kura, vumilia hiyo ndio ccm ya tieni! tieni! nambari wani heee...!
SASA Kichwa chako kitaachaje kuwa NYUMBA ya 'STRESS' (Gagazuko na Jakamoyo) Wakati tangu KUZALIWA Kwako mpaka UNAINGIA KABURINI Kazi yako ni KUANGALIA 'MAKOSA na KASORO' TU!! Hushukuru, Husifii, Huridhiki wala Hukubali!! Wewe ni kulaumu na kulalamika tu! - Masoud Kipanya
Hata ukipenda kusifu utawasifu kwa lipi mkuu, barabara zetu za mitaa, maji na umeme wa uhakika,huduma bora za jamii, ufisadi uliokidhiri kona zote, bunge la katiba, dharau za wana siasa au kipi. Huduma kama ni mbovu ni mbovu tuu, tatizo hata viongozi, wale ambao tumewapa jukumu la kutekeleza matakwa yetu nao ni walalamishi, wasipolalamikia watendaji - ambao wao wenyewe ndo waliwapa hizo kazi, watalia na wapinzani au chochote kile. Hili la afya linatakiwa liwepo kwenye mjadala wa kitaifa maana ni wengi wanaunamia kwa kukosa hizo huduma bora wanazopata India na South Africa.SASA Kichwa chako kitaachaje kuwa NYUMBA ya 'STRESS' (Gagazuko na Jakamoyo) Wakati tangu KUZALIWA Kwako mpaka UNAINGIA KABURINI Kazi yako ni KUANGALIA 'MAKOSA na KASORO' TU!! Hushukuru, Husifii, Huridhiki wala Hukubali!! Wewe ni kulaumu na kulalamika tu! - Masoud Kipanya
Hapa niko hospitali ya rufaa Mbeya,kuna wagonjwa ambao wamefika tangu saa 1,mpaka sasa ni saa 4 bado huduma hazijaanza eti madaktari wapo kwenye kikao...kiukweli napata tabu kupata jibu kwamba..>ni kwa nini vikao vinafanyika muda wa kazi?wakti huohuo ikifika saa 6 tu watasema muda wa lunch...hivi ni lini watanzania tutajali muda? aah Tanzania ingekuwa daladala tungeshuka wengi tukapanda daladala nyingine.!
Mkuu ni wengi saa wanaangamia kwa style hii, hospitali kukosa vifaa, dokta yupo nje au kwenye kikao na akirudi hana muda wa kupitia historia ya mgonjwa wake. Mbali na kuwa na vifaa vya kazi ni bora zaidi kuwapa maslahi mazuri ma-dokta na kuwaondolea zile part time zao, maana wakishakuona wanakupa referral kwenda kwenye clinic zao private, au hospitali za private wanapopiga part time. Mwisho wa siku lazima kuwepo na order ili hata wanaopenda kusomea u-dokta wajue kabisa pale sio money-making-machine, badala yake ni kutoa huduma bora.Mimi nalia na ubora wa hizo hospitali...Ok tumezowea "wakubwa" na familia zao wakiumwa wanakimbilia nje ya nchi kutibiwa.Majuzi nimepata msiba wa ndugu yangu katika basi la mkoa...kuna uwezekano mkubwa kuwa uhaba wa huduma bora za dharura hospitali ulichangia kuharakisha kifo chake...hapo nikakumbuka barabara hiyo hiyo hutumiwa na "wakubwa" wanapoelekea mjengoni...hivi hawaoni kuwa hata ungekuwa lifted na private jet kwenda South unaweza kupoteza maisha kabla hujafika huko? Na je hawana hata ndugu zao huko vijijini wasiokuwa kwenye list ya kipaumbele cha kwenda kutibiwa nje? Au hawajali? Haya tuendelee na katiba!
SASA Kichwa chako kitaachaje kuwa NYUMBA ya 'STRESS' (Gagazuko na Jakamoyo) Wakati tangu KUZALIWA Kwako mpaka UNAINGIA KABURINI Kazi yako ni KUANGALIA 'MAKOSA na KASORO' TU!! Hushukuru, Husifii, Huridhiki wala Hukubali!! Wewe ni kulaumu na kulalamika tu! - Masoud Kipanya
SASA Kichwa chako kitaachaje kuwa NYUMBA ya 'STRESS' (Gagazuko na Jakamoyo) Wakati tangu KUZALIWA Kwako mpaka UNAINGIA KABURINI Kazi yako ni KUANGALIA 'MAKOSA na KASORO' TU!! Hushukuru, Husifii, Huridhiki wala Hukubali!! Wewe ni kulaumu na kulalamika tu! - Masoud Kipanya
Changamoto zipo nyingi, na hizo hazina budi kuwepo, lakini huwezi kunidanganya kuwa serikali haijafanya chochote kile kizuri kwa wananchi.Nafikiri ni vyema baadhi ya watu kama wewe wakapewa ufahamu wa mambo yafuatayo:
1. Kuna watu wanalipa kodi kwa lazima na wengine wa hiari lakini matumizi ya kodi zao ni kwenye kustarehesha baadhi ya watu huku wengine wakipata shida sana na kuona huduma mbovu.. Hii peke yake ni stress tosha..
2. Kuna maeneo mengi yanakosa huduma za msingi. Kwa mfano ukijaribu kutembea kwenye hospitali za vijijini na hata kwenye miji mikubwa, kama sio misaada ya nchi kama Marekani na wafadhili wengine nakuhakikishia hali ingekuwa balaa zaidi. Imagine, lab machines au equipments, drugs, computers, urekebishwaji wa vituo vya afya, allowances za madaktari na wauguzi kwenye vituo vya afya ili wafanye kazi muda wa ziada, ulipwaji wa mishahara kwa baadhi ya wauguzi au wafanyakazi wa vituo vya afya; vyote hivi unafanywa na donors and kuna watu wengine wanaenda kuvitumia vyote hivi kwenye kampeni na kutaka kusifiwa kama unavyoshauri wewe.. Umeona watu wanavyolala chini kwenye mahospitali huku wabunge wanalilia laki tano kama posho na huku hadi wafanyakazi wa chini serikalini wanatembelea V8..?
3. Barabara mbovu, unapita kwenye miji mikubwa kama Dar na bado kuna mapango kibao barabarani...
4. Huduma mbovu za maji.. Imagine Dar tu watu wanatembea na toroli zenye madumu hadi sehemu za mijini kisa hakuna maji safi na salama..
5. Elimu duni.. Watu mpaka wanaishia kusifia Division 5 na kuona kiwango cha kufeli ni jambo la kawaida, litapita tu...
Sasa vyote hivi halafu mtu akose stress..?? Unless wewe ni wale wanaofaidika na system...
Changamoto zipo nyingi, na hizo hazina budi kuwepo, lakini huwezi kunidanganya kuwa serikali haijafanya chochote kile kizuri kwa wananchi.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ali-ya-kikwete-imefanya-nini-2005-2015-a.html