Lovery
JF-Expert Member
- Aug 15, 2014
- 1,540
- 3,135
Kuna ndugu yangu wa damu "ke" anaishi kibaha, bahati mbaya aliugua ikabidi akatibiwe zahanati fulani jina nalihifadhi. Bahati mbaya hakupata nafuu ikabidi apewe rufaa kwenda HOSPITAL TEULE YA RUFAA MKOA WA PWANI "TUMBI"
Jumanne 26/01/2016 Baada ya kufika hapo tumbi mchana akiwa hoi sana aliwekewa dripu la maji na akachukuliwa damu kwa vipimo na gharama akadaiwa alipie 23,000 na ikalipwa bila risiti.
Baada ya damu kuchukuliwa hakuna majibu yaliyorudi kwa mgonjwa kila wauguzi wakiulizwa wakawa hawana maelezo hadi mmoja wapo alipoamua kujibu bila hata vipimo kwamba ana malaria.
Jambo lililofata madaktari wakaanza kumuuliza anajisikiaje akaanza kutibiwa kwa kuhisi na kubadilishiwa dawa aina tofauti hadi siku ya leo mchana nilipofika.
Nikaamua kufatilia nikabaini damu ilichukuliwa na haikufika maabara, baada ya kuwa mkali na huku manesi wakilalamika nina kihelehele wakaamua kumchukua vipimo upya, na leo ni siku ya nne sijui kama watabaini magonjwa yote maana walishaanza kumtibu.
Ndipo nikaamua kuzungumza na wagonjwa wengine nao wanadai wamepewa ruhusa na wametibiwa bila hata kupewa majibu ya maradhi yao huku wakiwa wamelipia vipimo, wengi walikili waliombwa rushwa.
Nb:mgonjwa wangu alikuwa na msaidizi ambaye ni binti mdogo wa form 4.
Hakika wizara ya afya sijaona kazi yake hapa.