Responded Hospitali ya Muhimbili Mloganzila yaomba radhi baada ya huduma kusimama kwa saa kadhaa Januari 13, 2026

Responded Hospitali ya Muhimbili Mloganzila yaomba radhi baada ya huduma kusimama kwa saa kadhaa Januari 13, 2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
UFAFANUZI KUHUSU HITILAFU YA MTANDAO ILIYOATHIRI UTOAJI WA HUDUMA.

Dar es Salaam: Tarehe 13. 01. 2026

Leo tarehe 13. 01. 2026 ilitokea hitilafu ya kifaa cha mawasiliano cha mtoa huduma za mtandao (ISP) kiitwacho Fiber Optic Media Converter. Hitilafu ya kifaa hiki ilisababisha kukatika kwa mawasiliano na kuathiri kwa muda utoaji wa huduma zinazo tegemea mfumo wa kielektroniki.

Timu ya wataalam wa hospitali kwa kushirikiana na mtoa huduma wa mtandao (ISP) imeshughulikia changamoto hiyo kwa kufanya matengenezo ya kiufundi yanayohitajika na sasa hali imerejea vizuri na wagonjwa wanaendelea kupata huduma za matibabu kama kawaida.

Aidha, kwa sasa Hospitali kwa kushirikiana na watoa huduma wa mtandao (ISPs) inapitia mifumo pamoja na vifaa vyake vya mawasiliano na kuiboresha ili kuepuka changamoto na usumbufu unaoweza kujitokeza.

Kufuatia hali hiyo, uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza na unawashukuru wananchi kwa kuwa wavumilivu wakati tatizo hilo lilipotokea.

Imetolewa na;

Neema Mwangomo
Afisa Uhusiano Mwandamizi

Screenshot_20260113_215712_Samsung Notes.jpg

Hoja ya Mdau ipo hapa ~ Hospitali ya Muhimbili Mloganzila hakuna huduma tangu asubuhi, wanadai system inasumbua
 
Back
Top Bottom