Hospitali ya Mkoa wa Morogoro yasitishwa huduma ya chakula kwa sababu ya ukata

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,690
239,249
Hayo yamesemwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr Francis Samwene.

Alisema chakula cha wagonjwa kilikuwa kinapatikana kutokana na fedha za matumizi mengineyo ( OC ) wanazopokea kutoka serikalini , lakini sasa fedha hizo zinalenga matumizi mengine .

Hospitali hiyo ina vitanda 450.

Wakizungumzia hali hiyo baadhi ya wagonjwa walisema wanakabiliwa na hali ngumu baada ya huduma za chakula kusitishwa .

Chanzo - Mwananchi .

Swali uchwara - Hivi vipaumbele vya serikali hii ni nini , mbona kila nafuu iliyokuwepo inang'olewa ?
 
waache wananchi nao waisome namba. Madaktari walivyopunguziwa mshahara kwa asilimia 30 wananchi walishadadia sanaa wakisema nao waishi kama mashetani. Kuisoma namba hakuchagui huyu ni daktari na huyu ni mwananchi wa kawaida. kila mtu kwa muda wake ataisoma namba. It is a matter of time
 
Mkuu NIFEDIPINE hii serikali inakatisha tamaa sana , mbele naona giza totoro !
 
Haaa! kazi kweli walikuja na gia ya KULIPIA chakula muhimbili wakashindwa kabla hawajaanza, aibu zaidi hata waliokutwa wanakula wameshindwa kuendelea kuwalisha. Mbona tutaimba namba wala si kuisoma. Fedha zinapambana na chadema tu maskini. Ikulu si push ups jamani.
 
Wengine walijaza mahospitali kwa sababu ya hizi huduma za bure. Ukienda MNH sasa hivi utaona jinsi wagonjwa walivyo wachache. Kuna dada alikuwa mbele yangu, akaambiwa aende counter ya NMB kulipia shs.2,000/- kwa ajili ya huduma, yule dada alishindwa kulipa na kurudi nyumbani.
 
Je alikuwa haumwi ?
 
Magufuli alishashindwa kabla hajaanza atakopa fedha za wahindi wee na bado huduma zitakuwa chini
Zis kantry is veri veri had kuiendesha hata ibilis
Akipewa aongoze atachemsha ...chini ya chichiem
Ovaaa
 
Back
Top Bottom