Hospitali ya Mkoa wa Iringa yanusurika kufungiwa na NEMC

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa imenusurika kufungwa kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya usafi vya baraza la taifa la usimamizi wa mazingira (NEMC) baada ya kichoma taka chake kuharibika na kushindwa kufanya kazi kwa kipindi cha miezi minne ambapo serikali imeuagiza uongozi wa mkoa na hospitali kufanya matengenezo ya kichoma taka hicho haraka.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano na mazingira Luhaga Mpina ametoa agizo hilo hospitalini hapo na kutoa muda wa mwezi mmoja kwa uongozi wa mkoa na hospitali hiyo kutekeleza agizo lake ambapo amesema amelazimika kutoa agizo hilo kutokana na ummuhimu wa huduma zitolewazo hospitalini hapo lakini ukosefu wa kichoma taka hicho kisheria unamlazimu kufunga hospitali hadi kitakapoanza kufanya kazi.

Kwa upande wake mratibu wa baraza la taifa la usimamizi wa Mazingira nchini Kanda ya nyanda za juu Kusini Godlove Mwansojo ameshauri taka zinazozalishwa hospitalini hapo zitenganishwe ili taka ngumu zisizooza zihifadhiwe hadi hapo kichoma taka hicho kitakapotengemaa na kufanya kazi.

Akiwa hospitalini hapo Naibu Waziri Luhaga Mpina ameelezwa kuhusu ukosefu wa eneo la kupanua hospitali hiyo kutokana na kubanwa na gereza la mkoa wa Iringa ambapo ameutaka uongozi wa mkoa kupeleka mapendekezo serikalini ya kuomba kuhamishwa kwa gereza hilo ili eneo hilo libakie kwaajili ya hospitali hiyo pekee.
 
Back
Top Bottom