Hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda ni chafu balaa.

Muwazi

JF-Expert Member
May 16, 2014
355
81
Uchafu uliopo hapa hospitalini unatisha sana. Vyoo vyenyewe hutamani kuingiapo kutokana na hali mbaya ya uchafu. Yaani mikojo, Mavi na maji machafu yametapakaa hadi kinyaa. Haya yote yanafanyika na uongozi mzima wa hospitali upo bila kuchukua hatua yoyote ya kufanya usafi.
Pamoja na hayo pia kuna baadhi ya wagonjwa wa kipindupindi wodini wakati kuna sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili Ya wagonjwa hao.
Sasa kwa hali hii ni bora waziri wa afya aje ashutukize ili ajionee maana kwa hali hii sio rahisi kipindupindi kuisha na wakati huo mkuu wa wilaya naye yupo kama vile hayupo.
 
Subirini ziara ya kushtukizia ikatayofanywa na waziri wa Afya...ngoja awaandae waandishi wa habari kwanza ili aje nao huko

Ovaa
 
Back
Top Bottom