Hospitali ya Amana ni Hatari kwa wagonjwa: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hospitali ya Amana ni Hatari kwa wagonjwa:

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anold, Jun 20, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Mara kadhaa kwa nyakati tofauti nimesikia malalamiko kutoka kwa wananchi wakiilalamikia Hospitali ya Mwananyamala kuwa kuna uzembe unaofanywa na baadhi ya madaktari wasiowaadilifu ambapo vitendo hivyo licha ya kuwa vimesababisha vifo vingi lakini ni hatari pia kwa wagonjwa ambao wanaenda pale hata kwa matatizo madogo.

  Kutokana na rekodi hiyo mbaya ya Hospitali ya Mwananyamala nilishawishika kufikiri kuwa Hospitali nyingine zina nafuu. Hivyo nikashawishika kumpeleka mgonjwa wangu kwenye Hospitali ya Amana iliyopo maeneo ya Ilala. Ili kuokoa muda niliondoka nyumbani saa 11.00 alfajiri na kufika Amana saa 12.15 asubuhi, nilikuta baadhi ya wagojwa wameshawahi hata hivyo muda ulivyokuwa unaongezeka ndivyo idadi ya wagonjwa ilivyozidi. Tuliendelea kusubiri bila kuona dalili yeyote ya Daktari kwani tulielezwa kuwa mpaka wamalize kutembelea wagonjwa wodini ndiyo sisi tuhudumiwe, tulisubiri Madakatari hao mpaka tukachoka, hata walipokuja walikusanya kadi zote za wagonjwa bila kujali nani aliwahi au nani kaja kwa kuchelewa lakini nataka niwafahamishe wana JF kuwa pamoja na kujidamka mapema mgonjwa wangu alifanikiwa kumuona Daktari saa 9.30 jioni na hata baada ya kumuona huyu Daktari TATIZO la mgonjwa wangu ambalo ilikuwa lazima daktari aliangalie kwa macho alikataa kuliangalia na alichofanya ni kuandika dawa ambazo tulikwenda kununua kwenye duka la dawa tukarudi nyumbani. Nilichokigundua pale ni kuwa kunautaratibu mbaya sana wa kuhudumia wagonjwa aidha inavyoonyesha hakuna usimamizi wa maana ambao unaweza kuwafanya madaktari wafanye kazi zao kwa mujibu wa taratibu zinazotakiwa kinyume chake wanafanya kwa namna ambayo wanafikiri inafaa zaidi sana kunaviashiria vya wazi vya vitendo vya rushwa na kujuana kitu ambacho si rahisi huduma kwenye hospitali hiyo kufanyika sawasawa. Hivyo nawaasa wana JF kama mgojwa wako unataka atibiwe kwa haraka sikutumi utoe rushwa ila kama unampenda usimpeleke Hospitali hiyo vinginevyo usiende mikono mitupu Hospitali ya Amana yasije kukuta yaliyonikuta.
   
 2. oba

  oba JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Pole, labda ni kwa kuwa madaktari wako wachache na hawana operation, consultation allowance; unaonaje kwa kuwa wabunge wameng'ang'ania sitting allowance kwa kukaa na kupiga porojo bungeni madaktari nao wapewe consultation allowance ili kuwa motivate kuwahudumia wananchi wanaoteseka kama wewe?
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Natoa ushauri serikali iifunge hospitali ya Amana.
   
Loading...