Hospitali gani nzuri ya kuondoa Bawasiri au Uvimbe?

kwanini tu

Member
Nov 8, 2011
50
63
Naombeni msaada wa hospitali nzuri ya kuondoa Bawasiri au Uvimbe huko njia ya haja kubwa. Sipati maumivu yoyote nimeamua tu kukitoa hicho kinyama sikitaki.

Naombeni msaada wa hospitali na gharama zake
 
Pole sana. Kama upo maeneo ya kanda ya ziwa mwanza na mara kuna sabuni walalahoi tunazitumia zinaitwa B29 za rangi nyeupe. Endapo una bawasiri ya nje wakati wa kuoga tumia kuisugua sabuni hiyo mahari penye kivimbe cha bawasiri alafu njoo unishukuru.

Vile vile tumia mboga za majani mara kwa mara kunywa maji ya kutosha walau lita 5 kwa siku. So far saga alovela changanya na juisi hata ya azam embe kunywa. Mm sio mtaalam wa tiba ila niliambiwa bawasiri ni bacterial infection. Sasa tumia njia izo arafu utakuja nishukuru.
 
Kanunue mafuta ya nyonyo Castor oil...halafu uwe unapaka hako kauvimbe asubuhi na jioni ukiwa safi...inaondoa uvimbe kabisa kabisa unayeyuka unapotea...mimi ni shuhuda sijahadithiwa...na nilijifunza hapa hapa jamii forum..hii ni dawa kuliko zote popote..trust me..nayaheshimu haya mafuta na ninayatunza sana..oparesheni ni mateso hasa kuuguza jeraha ukizingatia eneo husika.

Nimeshauri wengi ambao wamepata hili tatizo na hakuna aliyejutia..labda awe alichelewa mpaka uvimbe ukapasuka..
Namshukuru sana mdau wa humu jamii forum aliyewahi toa elimu hii kwa faida ya wote..ni kweli ni kweli..imenisaidia kama sio kuniponya..

Nilipata mara ya kwanza..ilikuwa critical nikaja pata suluhisho humu..nikatumia bila imani kabisa..aisee ndani ya siku 3 tatu uvimbe ukayeyuka..nikakaa kama mwaka na nusu..ukarudi..sikuogopa nikatumia tena ukapotea..ikapita miaka kama miwili nikaona dalili tena..

Nikaiacha ikolee sana nikaanza kutumia ikapotea..imepita miaka 3 sijaona dalili yoyote.

Kumbuka kurudia kunatikana kama tatizo la kukosa choo na mfumo wa uyeyushaji chakula usipokuwa sawa..soo ili tatizo lisirudie suluhisho na mfumo wa ulaji vyakula tuu.
 
Kanunue mafuta ya nyonyo Castor oil...halafu uwe unapaka hako kauvimbe asubuhi na jioni ukiwa safi...inaondoa uvimbe kabisa kabisa unayeyuka unapotea...mimi ni shuhuda sijahadithiwa...na nilijifunza hapa hapa jamii forum..hii ni dawa kuliko zote popote..trust me..nayaheshimu haya mafuta na ninayatunza sana..oparesheni ni mateso hasa kuuguza jeraha ukizingatia eneo husika...

Asante kwa ushauri nitajaribu mkuu
 
Asante kwa ushauri nitajaribu mkuu
Amina Mungu akuponye..ila ukinunua nunua yale masafi yanayouzwa kwenye maduka ya vipodozi..kichupa kidogo 2000 -3000 Tsh.

Kuna wakati nilinunua kwenye maduka fulani wanaita sijui soon sijui Suni..yalikuwa meusi meusi nadhani yaliandaliwa kienyeji au yaliungua...aisee hayakunisaidia nilitumia siku 3 mfululizo sioni mabadiliko..

Nikaenda kununua yale special madukani nilipoanza tuu muda mfupi uvimbe ulipotea..
 
Naombeni msaada wa hospital nzuri ya kuondoa bawasiri au uvimbe huko njia ya haja kubwa .sipati maumivu yoyote nimeamua tu kukitoa hicho kinyama sikitaki
Naombeni msaada wa hospital na gharama zake
Dawa ya hiyo ni upasuaji tu, hospitali yoyote ya mkoa wanafanya huo upasuaji,sio ishu kubwa
 
Kanunue mafuta ya nyonyo Castor oil...halafu uwe unapaka hako kauvimbe asubuhi na jioni ukiwa safi...inaondoa uvimbe kabisa kabisa unayeyuka unapotea...mimi ni shuhuda sijahadithiwa...na nilijifunza hapa hapa jamii forum..hii ni dawa kuliko zote popote..trust me..nayaheshimu haya mafuta na ninayatunza sana..oparesheni ni mateso hasa kuuguza jeraha ukizingatia eneo husika...

Yanapatikaba wapi haya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom