Hongo kwa Askari wa barabarani ni haki?

Retreat

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
229
70
Ma great thinker, hivi ukipata ajali barabarani labda umegonga gari la watu kwa nyuma kisha askari wa usalama barabarani akaja eneo la tukio kuangalia hiyo ajali na nyie mkikubaliana kulipana, yaani aliyegonga akamtengenezee mwenzake gari lake, je kuna haja ya kumpa na askari wa usalama barabarani hela?

Maana nao huwa wanakaba penalti, sheria zinasemaje kwanza kuhusu ajali za namna hii?
 
Retreat

Hakina sheria inayomtaka mtu kumpatia askari hela! Nijuavyo kama mkikubaliana (hata kama Jamhuri ndiye mshitaki), askari hapaswi kupewa chochote. Endapo gari lako lina makosa mengine (kama break, bima road licence na mengine) hilo ni suala lingine...ambalo unaweza kulipia faini wala si kumpa askari hela.
 
ssiku zote ajali ikitokea wao nao lazma wapate chochote kama vile haki yao sio lazma uwape pesa tunawaendekeza hao
 
Bube
Nimekusoma mkuu, kwahiyo kama gari lako lina break fresh, bima, road license unamtosa tu. Ila hawakosagi kosa hawa jamaa. Na kama hivyo ulivyotaja huna kimoja wapo, fine ni sh ngapi kama ukipelekwa kituoni?
 
Back
Top Bottom