Hongereni Watanzania mnaodaiwa kutoitakia mema Tanzania

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Kama Kuna kundi lenye uchungu na Tanzania na ambalo linatumia akili na maarifa kuilinda Tanzania ni kundi la WATANZANIA WANAOELEZWA KWA HAWAITAKII MEMA TANZANIA, WASALITI NA WAMETUMWA NA MATAIFA YA MAGHARIBI.

Kila taadhari na ushauri unaotolewa na kundi hili na kupingwa na wanaoitwa wazalendo na Watanzania halisi umekuwa ukileta madhara kwa nchi na uchumi wetu.

Kundi la wasioitakia heri Tanzania limekuwa likizungumzwa kwenye mijadala mipana ya kitaifa na wengi wao wamekuwa wakiadhibiwa Kama waalifu lakini ukiangali mawazo na maoni wanayotoa ni yale yakulivusha Taifa, wamekuwa washauri wasio wanafki kwa nchi ndani na nje ya Bunge lakini hawasikilizwi kwa sababu wapo black listed kwenye nyoyo za watawala na watawaliwa.

Sina kumbukumbu Kama kundi la wasioitakia mema Tanzania Kuna siku limewahi kuishauri vibaya serikali bali wakati wote wamekuwa wakishauri ukweli na kwa Nia njema wakiamini kuwa hawana Tanzania nyingine.

Ni vyema wakajivunia kukataliwa na kundi dogo linaloishi kwa propaganda kuliko kukatishwa tamaa na kuamua kuwaunga mkono hao waitwao wazalendo na ambao wamekuwa vibaraka wa magharibi kwa vitendo ikiwemo kuuza rasilimali zetu, Uhuru wetu na Sasa wanauza utu wetu wakituamianisha kuwa wanatetea msimamo wa wananchi.

VIVA MNAODAIWA KUTOITAKIA MEMA NCHI YENU, MSIFE MOYO SHAWISHINI WENGINE TUIKOMBOE NCHI YETU KUTOKA KWENYE MIKONO YA WAZALENDO UCHWARA.
 
naam hatujawahi kukosea sisi wasaliti. tuliwaambia watoto wa kisichana kusoma ni haki yao ya msingi toka ndani ya katiba tukabezwa. hawa wazalendo uchwara wakamsifia jiwe bila kujiuliza kwa sheria ipi kuwanyima haki yao wakati katiba imesema binadamu wote ni sawa na haki itolewe kwa wote!?

tumewashauri swala la takwimu tukaonekana sisi tunapenda kutoa takwinu kwa vile tunapenda kukosoa . but wamekuja wazungu wamewalazimisha yale yale mawazo yetu wameyapokea. nani kati ya sisi tunaoitwa wasaliti na hawa wazalendo uchwara wanaitakia mema nchi hii??

bora niendelee kuitwa msaliti huku nikiongea ukweli unaodumu siku zote
 
Haaaa nawaona nawaona. Mi leo napita naangalia kwa jicho la kizungu. Maana nyie watu bana mnataka hadi siri nyeti tuwe tunawapa hao wazungu .. Basi sawa endeleeni. Kumbukeni kwamba wazungu zao zimefungiwa miaka nenda rudi na hata wakiua mtu mambo yanakuwa kimya. Shauri yenu mutaendelea kuwa tegemezi hadi mwisho Wa dunia.
 
Ninachoona ni kukataa mawazo yetu kwanza lakini kukubali ya mwingine kutoka nje na hapohapo akilaumiwa aliyetoa mawazo kwanza kwa "kutumwa" (kama ilivozoeleka kisiasa). Kisha wanakuja wazungu au watu wa nje (wanaotuma) na mawazo yao kukubalika. Mwisho wa siku tunaanza kutekeleza mawazo yale yale ya "watumaji"!! - Ni swala la kumkataa mjumbe lakini ujumbe ukapokelewa.

Ni dhahiri sasa kuwa "mkono mtupu haulambwi". Walambaji waliojibandika jina la "wazalendo" hawataki mkono mtupu!! Kama mawazo ya "wasio wazalendo" yangekuwa na kitu kama ilivokuwa kwa WB, AfDB nk - huenda "wazalendo" wangetambua michango ya wasio wazalendo.

WB inataka kuona gender equality katika education. Na kwa kuwa tunataka kutoa elimu bure wakati hatuna "kitu" - yatupasa sasa kukubali mikopo yao yenye masharti na huku tukisimama majukwaani kila siku tukitamba "we are a sovereign country, we make our own choices". Hatusikii tena msemo maarufu "kwa fedha zetu za ndani", tunarudi kwenye "tunakopesheka"!!

Pesa ni kila kitu!!
 
inawezekana kabisa wakawa na ushauri mzuri ila tatizo ni jinsi wanavyoutoa huo ushauri

Hivi unaanzaje kumshuri shetani awaue wachawi,wezi,makahaba,matapeli na wala ngada ni wazi utaonekana unazo hidden agenda

Ukiwa na ushauri nenda kamshauri mtu direct na sio kupost Facebook au twitter
 
Hii serikali kila siku inavuna aibu lakini haijifunzi.
Serikali utakuwa unaisingizia Chama tawala ndio kinachoukoroga uharo serikali unachofanya ni kuwanywesha wananchi

Wananchi wakipiga mbwewe na kusikia harufu ya uharo wakilalamika nguvu ya Dola inawashukia kwa kutunia polisi wasio na huruma na kuwanyoosha
 
Haaaa nawaona nawaona. Mi leo napita naangalia kwa jicho la kizungu. Maana nyie watu bana mnataka hadi siri nyeti tuwe tunawapa hao wazungu .. Basi sawa endeleeni. Kumbukeni kwamba wazungu zao zimefungiwa miaka nenda rudi na hata wakiua mtu mambo yanakuwa kimya. Shauri yenu mutaendelea kuwa tegemezi hadi mwisho Wa dunia.
Hivi bado kuna matangazo us ipige picha hapa
 
Hata suala la anayeshindwa kwny sanduku la kura kutangazwa mshindi kwa ubabe linaelekea ukingoni, maana hakuna asiyejua saivi... Waanze tu kujiandaa kisaikolojia kuwa wapinzani. Ila niwasihi washindi halali watapoingia kwny usukani, waache visasi ili amani itamalaki
 
"Naapa kwenye utawala wangu hakuna mzazi atarudi shule kusoma kwa hela yangu" kumbe hela in za jirani

"TunagharamiaElimu bure kwa fedha zetu" kumbe tuomba mkopo WB kwa ajili ya Elimu bure
 
Hata suala la anayeshindwa kwny sanduku la kura kutangazwa mshindi kwa ubabe linaelekea ukingoni, maana hakuna asiyejua saivi... Waanze tu kujiandaa kisaikolojia kuwa wapinzani. Ila niwasihi washindi halali watapoingia kwny usukani, waache visasi ili amani itamalaki
Taratiiibu dalili za upinzani kushinda tena nakuchukua nchi 2020 zinaanza kuonekana tofauti na ilivyodhaniwa na wengi, wamefeli vibaya kwenye mikakati yao ovu
 
Eti mzalendo mwenyewe ni Musiba, Polepole,Ndugai,Tulia na Magu.Haaaaahaaaaaaahaaaaaa
 
Back
Top Bottom