Hongereni sana serikali sikivu ya CCM

Hongereni sana serikali sikivu ya CCM

Acha upumbavu.mafisadi wakubwa nyie unasifia ujinga.ukikua utaacha.ccm imeoza na 2015 itakuwa ni chama cha upinzani kama kilivyo udp.
Naona hujamwelewa mleta uzi pole,katumia fasihi unawezakuelewa tu ukisoma kwa makini na utulivu.
 
Hongera sana cccccccccccccm kwa maisha bora kwa kila mwana ccccccm mwenye cheo na njaa kali kwa kila mlala hoi hata kama ni mwanaccm!
 
watu wazima wanapofika mahala mnajigeuza kuwa watoto na vituko kwenye jamii ni shida sana endelee kujipotosha na kupotosha wasiokuwa na upeo ila siyo wenye upeo wao.

Kosa lake ni kuipongeza ccm?
 
Hongereni serikali sikivu ya ccm, shule zote zipo katika hali nzuri tu, hazina uchakavu hata chembe ni propaganda za upinzani kutaka kuwakosanisha na wananchi, nyie ni wapiga kazi balaa ndo maana mpo kwenye BMK mkichakalika ili kutuletea katiba iliyo bora huku mkipokea pesa kiduchu laki 3 kwa siku mkiwa mmeacha mamilioni mpokeayo kwa siku ninawapongeza sana kwa hilo, mahospitali na zahanati zetu ndo usiseme maana zimejaa madawa na vifaa tiba kedekede, wajawazito hawalali mzungu wa nne vitandani na wengine chini maana vitanda vipo vya ziada, hamna wajawazito wanaofariki kwa kukosa huduma muhimu na hilo tujipongezeni

Viongozi na familia zao huenda nje siyo kwa minajili ya kutibiwa bali kwenda kulinganisha hali za utabibu za wenzetu zilivyo chini kuliko zetu, big up kwa sana, vyuoni mikopo hutolewa kwa wingi hasa kwa watoto wa masikini na watoto wa wakubwa mara nyingi hupata asilimia 100 ili kuwafuta jasho wazee wao kwa uzalendo ulotukuka nchini, madada zetu wa chuo wanaosimama mabarabani wakati mwingine ni kwa ajili ya kutafuta tu kipato cha ziada maana boom walilopewa huishia kwenye brazilian hair na viwalo vya kukata na shoka, alama za ufaulu zimeongezwa na serikali hii sikivu kiasi kwamba mwanafunzi wa sekondari kufeli ni ndoto, hao wanaowasema ni wivu wa kike unawasumbua na mtaendelea kutawala nchi hii kwa miaka elfu na moja, hongereni sana.

na huyu je?
 

Attachments

  • 1412017167903.jpg
    1412017167903.jpg
    35.3 KB · Views: 77
watu wazima wanapofika mahala mnajigeuza kuwa watoto na vituko kwenye jamii ni shida sana endelee kujipotosha na kupotosha wasiokuwa na upeo ila siyo wenye upeo wao.
Mada inatafakarisha ila wewe umekurupuka kama nape.
 
Back
Top Bottom