Hongereni mliovujisha mpango huu wa siri kubwa kwa wabunge (upinzani)

Yani Zitto alisha maliza mchezo wote pale maana kwa huruma ya Rais kati ya Muhongo,AG au Waziri mkuu kuna mtu angeondoka!

Nilitamani wapinzani wote wange muelewa lakini haikuwa hivyo!
Acha kuturubuni, hivi kumwondoa mtu kazini ni huruma?

Zitto alishaona asilimia kubwa mapendekezo ya PAC yanaenda kutenguliwa baada ya kuona Bunge linamsiliza Change zaidi kuliko mapendekezo ya kamati.

Maana aliona anakoenda ni kama utakua ubishi wa yeye na Chenge.

Ndio maana akasema akili imechoka maana aliona kila kitu kinakoendea ni sifuri.

Mbowe alisimama kumsaidia Zitto baada ya kuonyesha dalili za kukata tamaa.
 
Katika hili mimi sijaona namna CCM ilivyoshiriki kulinda mafisadi kuwajibishwa maana kinana, nape, mangula walishatoa msimamo wa chama. Lakini pia tumeshuhudia michango ya wabunge sendeka, wasira, mwigulu, peter, lekule na wengine wengi. ......kosa kubwa amekifanya speaker wa bunge kwa kuwa mwoga kufanya maazimio magumu. Bunge linaweza kabisa kuagiza serikali kuwachukulia hatua watendaji wake.
 
Mi nadhani kama kweli ulikua unafahamu kuhusu huo mkakati ni either ungeuleta mapema hapa jamvini,ama ungeandika mtiririko wote na sio kuishia walipo ishia leo meani ulitakiwa kwenda beyond ya leo walipo ishia other wise ulichokipost hapa kila mtu aliyekua anafatilia bunge kakiona na wala hakuna kitu kigen hapo ulochokipost ni flow tu ya shughuli za bunge...

Huna maana kabisa wewe.
kupost kilichokuwa kinaendelea bungeni ndio lengo kuu la majadiliano yote jukwaa la siasa.
 
Makinda bunge likimshinda tu.

Kjna wakati Simbachamwene alishaanza kuuliza tukimpelekea rais mapendekezo halafu asipoyatwkeleza tufanyeje sasa? Tumu umpeach rais?

Wabunge wengine wakawa washaanza kuongelea kupiga kura ya kukosa imani na Waziri Mkuu.

Kama ni mpango ulianza ku backfire.
 
Hii ngoma inaiangusha serikali ya CCM isipokuwa makini...

Uzuri ni kuwa upinzani upo pamoja isipokuwa wasaliti wachache wasiofika hata watano...
 
Acha kuturubuni, hivi kumwondoa mtu kazini ni huruma?

Zitto alishaona asilimia kubwa mapendekezo ya PAC yanaenda kutenguliwa baada ya kuona Bunge linamsiliza Change zaidi kuliko mapendekezo ya kamati.

Maana aliona anakoenda ni kama utakua ubishi wa yeye na Chenge.

Ndio maana akasema akili imechoka maana aliona kila kitu kinakoendea ni sifuri.

Mbowe alisimama kumsaidia Zitto baada ya kuonyesha dalili za kukata tamaa.

Mkuu,you are very intelligent,umeona mbali sana,kiufupi umenikosha.
 
Pale bungeni kinachoendelea ni mapambano kati ya ufisadi na uadilifu. Kuna wabunge watetezi wa ufisadi wakiongozwa na kina chenge wamepata washirika ndani ya baraza la mawaziri na hata makinda anawapa suport kijanja! Pia kuna kundi la waadilifu likiongozwa na mawaziri wachache kama kina mwigulu kwa upande mmoja na wapinzani! Chenge alipaswa kuwa lupango na sio bungeni.
 
Mi nadhani kama kweli ulikua unafahamu kuhusu huo mkakati ni either ungeuleta mapema hapa jamvini,ama ungeandika mtiririko wote na sio kuishia walipo ishia leo meani ulitakiwa kwenda beyond ya leo walipo ishia other wise ulichokipost hapa kila mtu aliyekua anafatilia bunge kakiona na wala hakuna kitu kigen hapo ulochokipost ni flow tu ya shughuli za bunge...

Upon Uzi wa yeriko nyerer tafuta uusome aliuleta kabla ya jana
 
Mafisadi ni wachawi balaa dhidi ya maadui zao kama tulivyoona bungeni KAZI YA USHIRIKINA ILIVYOFANIKIWA !
 
Why wasirudi? Hamjifunzi tu?
Kwani wasiporudi kuna kitakachosimama?
Wamegomea vingapi na wakapata faida gani?
WARUDI NA WAENDELEZE.
Hata hivyo hii sio UPINZANI Vs CCM

Ni PAC Vs MAFISADI
UPINZANI KUGOMEA NI KUIGAWA PAC.

Wapinzani wakiondoka inaleta message duniani kwamba hawajakubaliani na kitu chochote kitakachoamuliwa na ndio maana katiba pendekezwa kila mtu anaipinga.
 
Makinda alionekana wazi kuwa kuna Maelekezo kapewa na Chama chake au Wakubwa wake kimamlaka.

Alichokuwa anafanya jana ni kukiuka utaratibu tuliozoea katika upitishaji wa Maazimio ya Bunge.

Wapinzani wasaidieni Kamati ya PAC Mapendekezo yao yapite hasa kuhusu Muhongo,Maswi na Tibaijuka. Suala la Pinda linazungumzika endapo hao wataondoka kwanza.
 
[F. T=comic sans ms]Kuna wadau labda mmeshanga sana ni nini kimetokea katika majadiliano bungeni kuhusu sakata la escrow, hasa baada ya kufika kifungu cha 7 cha kumuwajibisha muho

hii gemu ilichorwa siku nyingi sana tangu j3 wiki hii (master plan mkuu alikuwa chenge, wengine waliotoa mawazo ya kufanikisha hili walikuwa pinda, wassira, makinda, na kinana)

serikali iliona hakuna jinsi inaweza kumnasua muhongo, maswi na waziri mkuu katika uzembe huu na watuhumiwa hawa waliahidiwa kulindwa kimkakati

zaidi ya yote serikali ilishapima upepo kwa nyakati hizi za uchaguzi wa serikali za mitaa, na uchaguzi mkuu ujao ikaona si vyema kuruhusu serikali kuanguka tena maana yale makundi ya uraisi yanazidi kuhasimiana, na pia ikaona itatoa image mbaya sana kwa jamii

sasa plan ikawa kama ifuatavyo

sasa bwana job ndugai intelejensia ya chama ilionyesha kuwa si mtu strong anayeweza kuliendesha bunge na kulikuwa na hisia kuwa huenda anapokea maelekezo kutoka kwa wabaya wa serikali hii, kwahiyo ishu mbili zikafanyika faster 1. Kumuondoa job ndugai katika kiti, na kupewa karipio kali sana kwa kuruhusu majadiliano haya
2. Plan b hii ilikuwa kali sana serikali ikafanya mawasiliano na iptl, na kuwaamuru wanasehria wake kupeleka zuio mahakamani la bunge kujadili ishu hii, na zaidi ya yote barua hiyo ilikuwa on the way na ilifika dodoma, ndipo serikali wakawa wanajaribu kupima kina cha maji, lakini pia mahakama tena ingizwa katika kulitega bunge kwa kuwatisha kuwa hawapaswi kujadili suala hilo kisa liko mahakamani wakati shauri lililopo mahakami ni suala la madeni/madai,

lakini lengo hasa lilikuwa ni kumtumia makinda leo atumie kete ya kuruhusu demokrasia na kutoingilia mamlaka zingine kisa tayari kashaingilia suala la mahakama, na alipangiwa zaidi kuonyesha kuwa anaruhusu democrasia ili kupesha kuikwanza serikali kuu eti kisa kashaikwaza mahakama kwa kuruhusu majadala huu kuendelea. Lakini suala hilo lilikuwa limepangwa kabisa kuwa ionekane kuna mtifuaano wa kimamlaka kati ya bunge na mahakama

sasa leo ndio maana mama makinda karuhusu sana watu wajadiliane kwa kupitia azimio moja badala ya lingine na kujifanya anaomba sapport ya wabunge hasa wa upinzani. Na lile lililotokea kwa chenge kupewa nafasi ya kutoa muongozo na kushauri anavyoona hayo maazimio yakaeje hasa yanayogusa watendaji walioteuliwa na raisi, plan hiyo ilikuwa imepangwa kupigiwa chapuo na wakina mama mawaziri, ilikuwa ni plan, sasa information zikaliki zikamfikia mbowe , na mbowe akawajulisha watu wote wa karibu yake kuwa hapa tayari kuna mtego. Maana kama kila jambo la mtu ambaye hawakumchagua wabunge kuwaachia mamlaka za uteuzi maaana yake ulikuwa huwezi baadae kufuatilia tena kudai why fulani hakuwajibishwa.

Na ndio maana kila wakati spika alijifanya, kuwa ohh nataka jinsi ya kuweka hapa form ikaaje ili kuzuia kuingilia mamlaka zingine, eti kisa tayari anakesi kwa kuingilia mahakama, lakini plan hapa ilikuwa ni kumukoa muhongo, na waziri mkuu, maana huteuliwa na rais mbali ya kwamba waziri mkuu huthibitishwa na bunge, lakini kwa hari ilivyokuwa tangu juzi katika vikao vya ccm, tayari watu walishaadaliwa kumtetea mno waziri mkuu, maana serikali ilikuwa inaenda kuanguka, hasa ni visa vya madaraka vya wasaka urais. Chuki binafsi baina ya wabunge wa kamati ya pc toka ccm na wale wasio wajumbe. So mbowe alipenyezewa mchongo huu mwishoni kabisa, na kuamua kufanya aliyofanya.

Lakini plan ilikuwa ni kila mtu ambaye hakuchaguliwa na bunge basi bunge lishauri tu akawajibishwe na mamlaka za uteuzi baada ya uchunguzi, na suala hilo lingefika hadi mwakani bunge linavunjwa wakina muhongo, maswi, na pinda wangekuwa madarakani wakati woote huo;

sasa tayari kuna ugomvi mkubwa unaendelea kati ya wale wajumbe 19 wa pac walikuwa ni wa ccm, wanalaumiwa sana na ccm wenzao kwa kuandika yale mapendekezo na kumshambulia muhongo, na baadhi yao wameanza kutishiwa;

kwa jinsi hili suala la uchotwaji wa pesa hizi za escrow lilivyo mamlaka ya juu kabisa inalijua, na wamefaidika kabisa na mgao huu, ni mission nyeti sana ya serikali kupata pesa hizi kupitia kwa singa singa ili kutumika mwakani wa kati w chaguzi na kampeni;

kwa jinsi hali ilivyokuwa imepangwa hakuna cha kuwalaumu watu wa vyama pinzani, na pac yoote, ccm walidhani hii mission yao isingeliki; maana wakina ngeleja, au kagasheki waliwajibika kwa uzembe wa watu wengine na, si wao tu direct walienda kutenda makosa yale sasa iweje hawa wakina muhongo wakafikiriwe tena na rais, eti kisa tu wamegoma kujiudhuru.

Hongereni wabunge woote mlioamua kuangalia maslahi ya taifa.
[/FONT]

Nakupongeza sana kwa utunzi Ingawa hauna vina.

Vipi mbowe ni moja ya watuhumiwa au? Mbowe yuko kwenye kamati ya uongozi au? Mbowe na Zitto wakoje? Nani yuko tayari kuwa outshined na mwenzie? Je nani atajiuzulu? Je baada ya eskrow bungeni what next?
 
Back
Top Bottom