MpiganiaUhuru
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 777
- 912
Wana-JF!
Nichukue fursa hii kusema kuwa kwa muda mrefu sasa CCM imekuwa ikiishi kama miungu-watu mpaka kufikia sehemu ambayo wananchi tuliridhika na hali hiyo na kuiona ya kawaida! Walipoanza kujitokeza wapinzani kama kina Marando na Mrema enzi hizo wala watu hawakuwaelewa zaidi ya kuwashabikia tu kwa muda mfupi. Lakini sasa mambo ni tofauti kabisa.
Kwa sasa CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani wameweza kuwafanya CCM kuweweseka na kupoteza mwelekeo kiasi cha kujikuta wakifanya mambo ambayo hayapaswi kufanywa na chama kinachomiliki serikali! Kwa kauli za viongozi wa CCM kama vile; "Wanatekeleza mpango wao kuwa nchi haitatawalika", "Wanawavisha watu nguo za JWTZ na polisi wafanye mambo ambayo yataonekana kuwa yamefanywa na serikali ya CCM", "Wanawatumia watumishi wa Serikali wakiwemo JWTZ na Polisi ili kutekeleza matakwa yao na kuisingizia CCM", nk, zikihusisha viongozi kama Kikwete, Pinda, Lukuvi, Hawa Ghasia, Mwigulu Nchemba na wengineo, ni wazi kuwa hawa watu wa CCM maji yamewafika shingoni tofauti na miaka ya nyuma ambayo walikuwa wanawabeza wapinzani wanavyotaka, HONGERENI SANA MAKAMANDA KWA MAFANIKIO HAYA! Keep it up!
Natoa hongera hii kutoka moyoni kwani moja ya mbinu za kivita pale unapotaka kumshinda adui yako kirahisi ni kumchanganya akili (kisaikolojia)! Hawa jamaa wamefanikiwa kumchanganya adui yao na kumtoa kabisa kwenye line!🙂