VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Nawapongeza watani zangu CHADEMA kwa kupata Katibu Mkuu mpya. Hongereni kwa kupata Mtendaji wenu mkuu wa kichama. Nawapongeza kwa mambo matano.
Kwanza,nawapongeza kwa kumpata Katibu Mkuu aliyeifagilia mbali tuhuma ya ukanda na ukabili. Dr. Vicent anatokea kanda ya Ziwa. Msukuma.
Pili,nawapongeza kwa kupata msomi,mwenye Ph.D. Mwanzoni,enzi za Dr. Slaa,Ph.D ya Dr. Slaa tuliizunguzia kama ya kimagumashi. Ya Dr. Vicent iko tofauti. Yake iko wazi.
Tatu,nawapongeza kwa kutambua umuhimu wa kanda ya Ziwa. Pamoja na kupoteza majimbo mengi mwaka jana,bado mnasimama na kanda hiyo. Ndiyo maana mmemuamini Dr. Vicent. Mkijirekebisha mlipokosea,mambo yatakuwa mazuri.
Nne,nawapongeza kwa kumpata Katibu Mkuu nje ya Bunge. Atakuwa muda wa kutosha kujenga na kutangaza chama. Hakika,mtatuamsha CCM ili tusibweteke.
Tano,mmetambua kuwa uanasiasa unajengwa. Dr. Vicent atakuwa mwanasiasa mahiri atakapoishiriki kila siku. Namfahamu. Yuko vyema upstairs. Mjenzi wa hoja. Mtu mwenye msimamo.
Lakini,mpeni ushirikiano. Mwekeni mbali na mapandikizi. Kila la heri!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam