Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,353
- 26,194
Juliana Shonza na Mtela Mwampamba wamevunja ukimya. Wamehama CHADEMA na kuhamia CCM. Ni jana tu mambo haya yamejiri. Nawapongeza kwa uamuzi wao kwa sababu/vigezo vifuatavyo:
1. Kuichagua na kuhamia CCM
Wamejua kuwa sifa walizonazo hazitakiwi na chama chochote cha siasa nchini zaidi ya CCM. Wamejua kuwa CCM ni chama cha wapenda kutoa matamko,kuhojiwa na vyombo vya habari na kutofuata utaratibu wa chama. Sifa hizo walizonazo hazikukubaliwa CHADEMA. Hongereni sana!
2. Kuhamia CCM jana
Akina-Shonza wamekwenda na 'movie'. Walijua fika kuwa jana kulikuwa na shamrashamra Dodoma baada ya uchaguzi wa wajumbe wa CC ya CCM.Walijua fika kuwa viongozi waandamizi wa CCM na hata vyombo vingi vya habari vitakuwa pale. Na wao wakapokelewa,wakaongea,wakatamka kutaka kugombea Ubunge(Shonza akiitaka Ubungo). Wakaonekana runingani,wakaandikwa magazetini. Hongereni sana!
3. Kupiga picha na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM
Mkapiga picha na Rais wa nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM. Juliana Shonza ulikuwa kushoto kwa Mwenyekiti Mtela Mwampamba kulia. Mlishikwa kama watoto mliokuwa mkisubiriwa kwa hamu mrejee CCM. Mtela ukajisifu facebook kwa tukio hilo. Mlipendeza sana kwakuwa sasa mpo nyumbani. Hongereni sana!
4. Hamkusubiri maamuzi ya rufaa zenu
Mmekata rufaa kupinga kuvuliwa uanachama wa BAVICHA. Mmekata rufaa kwa uongozi wa juu wa chama.Lakini,mmeshtuka. Mmejua kuwa chama kizima hakiwataki. Kinawaona wasaliti. Mmedhihirisha kuwa wanachodhani ni kweli. Mmerudi kwa 'baba'. Hamhitaji tena majibu ya rufaa. Vipi Juliana Shonza,huaki tena Uenyekiti wa Taifa wa BAVICHA. Umesusa? Hongera!
5. Kuonesha nia ya kugombea Ubunge
Juliana Shonza umenukuliwa ukisema nakujiapiza kuwa lazima umng'oe John John Mnyika Jimbo la Ubungo. Hapo,kama mambo yatakwenda kama unavyotaka yawe,ndipo utakapoona kuwa wewe si maarufu kuliko CHADEMA. Ulikuwa unabebwa na chama. Chama kkilikuvumilia,kilikulea,kilikutunza na kukufunza. Utajua kuwa uongozi wa kuchaguliwa si mchezo...kwakuwa wapiga kura humjua wanayemchagua kinagaubaga. Hongera kwa hatua yako ya kutamka kuutaka Ubunge.Lakini,utaaminiwa na CCM? Ndugu yako Nape Nnauye itakuwaje?
Hitimisho
Kimsingi,mmefanya jambo jema. Sasa mmetoa nafasi kwa CHADEMA kujielekeza katika kujiimarisha zaidi ya kushughulika nanyi kila wakati. Mliko mbaki salama na mjiandae kwa mapambano ya kisiasa dhidi ya mliokuwa mkiwasaliti-kama isemavyo.

Last edited by a moderator: