Hongereni ACT-Wazalendo, CHADEMA mnasubiria nini?

Muju4

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
5,322
7,161
Salam wanajukwaa,

Kwanza nianze kuwapongeza ACT-Wazalendo kwa ukomavu mkubwa wa kisiasa waliouonesha hakika hii ni ishara ya kuwa ni chama ambacho kinaweka maslahi mapana ya Taifa mbele.

Katika wakati kama huu kususasusa ni ishara ya kuonesha utoto wa hali ya juu, kitu ambacho kitaonesha maturity ya hali ya juu ni kusimama ulipojikwaa na kuwa relevant na hali ya uwanja ilivyo kwasababu ukikaa kimya haitasaidia na utajiondoa masikioni mwa mapenzi na washabiki zako na mfano halisi ni pale wasanii mahili wanaposhindwa kutoa nyimbo mpya ili kukonga mioyo ya mashabiki wao hiyo hupelekea kusahaulika.

Nini CHADEMA mfanye?

Msishupaze shingo zenu hakikisheni kila nafasi mtakayopewa mnaichukua na kuweka watu mahiri ambao watawawakilisha vyema.

Ni muhimu sasa kukubaliana na hali ilivyo na kuungana kujenga nchi, mimi naomba na nyie CHADEMA muige huu mfano wa ACT-Wazalendo.

Asanteni sana muwe na siku njema.
 
CHADEMA ni moja ya chama makini na bora hapa nchini na barani Afrika, CHADEMA siyo kikundi cha kutafuta fedha kutoka kwa watawala.

CHADEMA haipo tayari kuuza utu wa watanzania kisa ruzuku, Chadema kitaendelea na msimamo wake daima.
 
Huyu mpuuzi hajui hata ameandika nini?
Wewe unaonekana umejaa chuki tu, hata vitani huwa pana meza ya mazungumzo na mambo yanakwenda mbele. Wewe ni mchawi wa Taifa.
 
Cdm ni moja ya chama makini na bora hapa nchini na barani Afrika,cdm siyo kikundi cha kutafuta fedha kutoka kwa watawala.

Cdm haipo tayari kuuza utu wa watanzania kisa ruzuku,cdm kitaendelea na msimamo wake daima.
Masikini ulipotaja ruzuku tuu nikajua kumbe haujui vizuri CDM
 
Ofisi na maamuzi yao wanafanyia twitter mwenyekiti kigogo na maria sarungi sura zao hazionekani maamuzi ya maana yatatoka wapi!
 
Mkuu mmeanza tuma sumaku yenu kwa chadema? Haiwezi nasa MAANA sumaku ya chadema ni kali kweli na ncha zinakinzana,
So uliyoyaandika hayawezi tokea CHADEMA wanajua wanaelekea wapi, chama kimekomaa Sana na kiko tiyari kutawala nchi, japo kinacheleweshwa tu, ni swala mda
 
Ndugu yangu subiri muda mchache tuu nao Chadema watawaruhusu akina Halima kuwa wabunge. Hilo ni dhahiri. Wamechelewa tuu ili kuwaridhisha Tundu na Mabeberu waliowapa mpunga wa kampeni. Mpunga ule wa milioni moja kwa kila mbunge kwa kila mwezi wauache? Haiwezekani.
 
Kwani kuna taifa la ngedere?
Labda!
IMG_20201202_170329.jpeg
 
Wewe ni mnuarwanda,habari za siasa za Tanzania zinakuhusu nini?
Tusifikie kubaguana namna hiyo ndugu yangu Mimi ni Mtanzania na nimezaliwa na shujaa wa Tanzania
IMG_20190906_113158.jpg
 
Mkuu mmeanza tuma sumaku yenu kwa chadema,?haiwezi nasa MAANA sumaku ya chadema ni kali kweli na ncha zinakinzana,
So uliyoyaandika hayawezi tokea chadema wanajua wanaelekea wapi ,chama kimekomaa Sana na kiko tiyari kutawala nchi,japo kinacheleweshwa tu, ni swala mda
Ishaurini vizuri isishupaze shingo wawe na busara na hekima katika maamuzi yao ni muhimu wakawa wanasikika kwa wananchi kwa kushiriki katika MAENDELEO
 
Back
Top Bottom