Tangu maamuzi ya kumfungia mkuu wa mkoa Dar Makonda utolewe na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na kuungwa mkono na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT) na taasisi nyingine za kihabari nchini, familia za watumishi wa umma waliokuwa wanadhalilishwa mbele ya vyombo vya habari zimeanza kufuatilia taarifa zenu pasipo kuwa na hofu ya kushuhudia udhalilishaji uliokuwa unafanywa na kiongozi huyo.
Nakumbuka yule mama wa ardhi alivyotukanwa matusi ya nguoni, hivi watoto wake na rafiki zake walijisikiaje, nakumbuka aliyekuwa mkurugenzi wa Jiji Kabwe alivyodhalilishwa mbele ya kamera, vilevile nawakumbuka watendaji wa serikali za mitaa walivyokuwa wakifokewa kama watoto wadogo, nawakumbuka maafisa aridhi walivyoamuliwa kuswekwa ndani bila kujitetea, nakumbuka mwingine alifukuzwa kazi kwa kitendo cha kuchelewa site.
Haya yote yalikuwa yanafanyika mbele ya vyombo vya habari na kuonyeshwa kwenye TV, leo hatuoni tena, ilikuwa ni aibu kuangalia taarifa ya habari ukiwa na watoto.
Isingekuwa nyie hata kitendo cha juzi cha Makonda kusema angekuwa yeye waliobeba mabango ya kudai nyongeza za mishahara angewachapa viboko kingeonekana mbele ya watoto wetu.
Naomba muendelee na msimamo huo kwa viongozi wote wanaoonekana kuwa na elements za tabia zinazofanana na hizo.