TCRA, hawa wa kuliza watu bado wapo, mmewachukulia hatua gani?

Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
14,007
13,799
Ndugu zangu Watanzania, wale wahuni bado wapo sana. Sahivi sio ile hela tuma kwenye namba hii au niwekee laki tatu nikuwekee milioni moja. Leo wamenijia na mbinu mpya kabisa kwangu. Au wengine walishawajia kwa pigo hizi? Kwangu mimi hizi pigo ni mpya.

Nimetulia nafanya mambo yangu mara namba ngeni inaingia, nikajifikiria kuitosa ila nikasema wacha nisikie huyu boya ana habari gani. Mazungumzo yakaanza:

Jamaa: Hellow mteja, mimi ni customer care wa tigo. Natumai u mzima na unafurahia huduma zetu.

Mimi: Naam, bila shaka.

Jamaa: Asante sana ndugu mteja. Sasa kuna shida moja tungependa utusaidie wewe kama mteja mwaminifu..

Mimi: Jambo gani hilo?

Jamaa: Kuna pesa imetumwa humo kwako kimakosa ndugu mteja. Tunatumai umeiona ili tukupe maelezo zaidi.

Mimi: Sijaona meseji mimmi

Jamaa: Basi kata ikiingia tutakupigia.

Ujumbe ukaingia, kiasi hewa kilichoingia 498,000/=(Ntaweka screenshot hapa chini). Akapiga baada ya sekunde chache. Maongezi yakaendelea tena;

Jamaa: Umeiona ndugu mteja mwaminifu?

Mimi: Ndiyo nimeiona.

Jamaa: Unaweza kututajia ni kiasi gani kama hutojali.

Mimi: Ndiyo naweza.

Jamaa: Ni kiasi gani.

Mimi: 498,000/=.

Jamaa: Vizuri sana ndugu mteja mwaminifu. Sasa tunaomba uaminifu wako katika hili. Chukua kalamu na karatasi, nenda sehemu kimya kabisa tulivu tukupe maelezo, usikate simu.

Mimi: Haya tayari

Jamaa: Mbona tumesikia sauti ya vyuma kugongana.

Mimi: Nimefunga geti

Jamaa: Haha, vizuri sana ndugu mteja. Unaonekana mwaminifu halafu mjanja sana. Kwa kweli tumepata bahati sana pesa ya mteja wetu kufika kwako. Upo wapi kwanza?

Mimi: Nipo Mwanza

Jamaa: Haha kumbe mtani kabisa (Akasifia wee)

Mimi: Nipe maelezo unanipotezea muda

Jamaa: Samahani ndugu mteja, Andika hii namba 0675566220 jina ni Elizabeth Nyanda. Hebu rudia(Nikarudia)

Jamaa: Sasa nenda kwa wakala wa tigo pesa. Usimwonyeshe hiyo SMS wala usimwambie mtu kakosea namba..Hao mawakala ni wahuni sana. Cha kufanya Mwambie wakala Atume 450,000 kwenye hiyo namba. Hiyo 48,000 inayobaki itakuwa zawadi ya uaminifu wako kwetu. Tumefurahishwa sana na uaminifu wako.

Mimi: Sawa bro. Sasa mzee nakuuliza swali (akakubali). Kwanini hiyo hela nisiitume kwenye hiyo namba mimi mwenyewe.

Jamaa: Hapana ndugu mteja, hiyo hela imeingia humo kwa Master Card. Haiwezekani kufanya hivyo

Mimi: Kaka yaani mimi ni wakala mstaafu hivyo naelewa kila kitu. Huwezi nidanganya

Jamaa: Ulikuwepo kwenye semina ya mawakala jana? Ndio ilipitishwa hivyo

Mimi: Sawa mzee. Sasa mi nafanya hivi; hiyo hela siitoi wala siigusi. Nyie wenyewe Tigo muitoe muirudishe kwa mwenye nayo.

Jamaa: Hiyo hela imeingia kwa MasterCard, mwenye nayo katuma kwa USD hivyo sisi hatuwezi irudisha. Hiyo njia niliyokuambia ndio msaada pekee.

Mimi: Wewe ni tapeli

Jamaa: Unasemaa?

Mimi: Wewe ni tapeli mchanga kwenye utapeli

Jamaa: Kwa nini ndugu mteja?

Mimi: Meseji za tigopesa kwangu zikiingia zinakuwa na Jina la tigo pesa na sio namba ya mtu

Jamaa: Usikariri ndugu mteja, siku mitambo ikisumbua tuna haki ya kutumia namba yoyote ile.

Mimi: Mshenzi wewe kawatapeli wa kuja labda, wewe bado sana kwangu.

Jamaa: Ahaa unatutukana, ngoja nimwambie bosi hapa akufungie laini halafu tunamwambia na polisi hapa aje akukamate kwa kutudhalilisha sisi taasisi kubwa.(akampa simu huyo bosi wake).

Bosi fake: Wewe unatuchezea. Tutakupeleka polisi

Mimi: Polisi na tigopesa wapi na wapi. Washenzi tu nyie katapelini wajinga huko sio watanzania wajanja.Tulishajanjaruka sasa hivi

Jamaa: Mjanja wapi wewe (tusi halafu akakata)
…………………………

======

TCRA hawa watu bado wapo. Sijui kama kuna ambao walishachukuliwa hatua. Ukiona maelezo hapo juu ni rahisi kwa watanzania wengi kulizwa.

Halafu huu mfumo wa kuwa na namba nyingi unawanufaisha hawa sababu mwananchi anajua ana laini moja kumbe kuna nyingine zilizosajiliwa kwa taarifa zake zinatumika bila kujua.TCRA liangalieni hili tena halafu fanyeni hima kuwakamata wajinga hawa.

Nawasilisha.
Screenshot_2020-03-26-15-29-13.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu kwa kunusurika na majizi makubwa hayo.Siku chache zilizopita nilisalimisha kiasi cha fedha kutoka kwa jirani yangu aliyetumiwa SMS kama hiyo.

Mada za malalamiko juu wizi kama huu zinatolewa mara kwa mara humu jamvini lakini sioni hata hatua zinazo chukuliwa na mamlaka husika(TCRA ) .

Ni wakati sasa wahusika kusikia na kusikiliza kilio chetu na kuchukua hatua stahiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu kwa kunusurika na majizi makubwa hayo.Siku chache zilizopita nilisalimisha kiasi cha fedha kutoka kwa jirani yangu aliyetumiwa SMS kama hiyo. Mada za malalamiko juu wizi kama huu zinatolewa mara kwa mara humu jamvini lakini sioni hata hatua zinazo chukuliwa na mamlaka husika(TCRA ) . Ni wakati sasa wahusika kusikia na kusikiliza kilio chetu na kuchukua hatua stahiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole kiongozi kwa mkasa huo...kama ni hivyo watuambie tija ya kusajiri kwa mfumo wa alama za vidole ilikuwa nini
 
Hapo sasa ndio pa kujiuliza. Kila kiongozi akichukua ofisi anayengeneza ulaji wake.
Yanini kuwa na kitambilisho cha kura na national Id card wakati zote zinatatua shida zinazofanana?
Haswaa...halafu huu mfumo inaelekea ni white elephant...,umekula pesa bure.
 
Demu mmoja amepigwa Laki sita na hamsini kwa utapeli huu.


TCRA kazi yao kutafuta wanaokosoa Gavumenti.

"What is yours will always be yours no matter what "
 
Demu mmoja amepigwa Laki sita na hamsini kwa utapeli huu.


TCRA kazi yao kutafuta wanaokosoa Gavumenti.

"What is yours will always be yours no matter what "
Wanawake wengi wanapigwa kwa sababu ya tamaa tena akiambiwa usionyeshe msg ndio kabisa ,akifika kwa wakala utasikia wewe tuma tu wewe tuma 😀😁😀 mimi hizo simu za tuma sijui umeshinda hazina nafasi kwenye simu yaani simsikilizi hata sekunde tano,msg inafutwa ndani ya sekunde haijalishi mkubwa kiasi gani
 
Mkuu usajili ni kwa ajili ukiitukana serikali yako wakupate kirahisi hayo mengine hayawahusu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata ikiwa hivyo anaweza tukana mwingine akakamatwa mwingine..sababu jina moja laweza kuwa na laini nyingi... Ni one to many... Labda watumie location za mitandao ya simu kwa msaada wa jina hapo mhusika atakamatwa vizuri kabisa.
 
Back
Top Bottom