Hongera sana Mama Wambura

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Mbunge asaidia kifaa cha ultrasound

Hassan Simba, Mtwara
Daily News; Thursday,October 16, 2008 @20:20

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Anastazia Wambura, ametoa msaada wa kifaa cha kupimia magonjwa (ultrasound) kwa Hospitali ya Wilaya ya Tandahimba, mkoani humu.

Akikabidhi msaada huo uliogharimu zaidi ya Sh milioni 70 katika hafla iliyofanyika hospitalini hapo juzi, Wambura alisema lengo ni kuwawezesha wananchi kupata huduma ya vipimo vitakavyowawezesha wapate tiba sahihi.

“Sasa madaktari wetu wataweza kutambua ugonjwa unaomsumbua ….ile dhana ya kutumia dalili kama kielelezo cha ugonjwa sasa itakuwa haipo. Kutokana na kukosekana kwa kifaa hiki wataalamu wetu huenda walikuwa wanatoa tiba kinyume na maradhi ya mgonjwa,” alisema Mbunge huyo.

Alifafanua kuwa msaada huo umetolewa na rafiki zake nchini Ujerumani na kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imegharimia kusafirisha vifaa hivyo kufanikisha lengo la kuboresha huduma hizo za afya katika hospitali hiyo.

“Kifaa hiki kitatumika pia kupima maendeleo ya mtoto awapo tumboni mwa mama yake, hivyo kupunguza vito vya watoto na wajawazito wakati wa kujifungua…si ultrasound pekee bali pia nimeleta kifaa cha kupimia shinikizo la damu, sukari mwilini, uzito wa mtoto na kifaa cha kupumulia” alisema Wambura.

Awali akisoma taarifa, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. James Ligwa alisema msaada huo umeondoa adha kwa wagonjwa ya kwenda Hospitali ya Mkoa Ligula kupata vipimo, jambo ambalo alisema lilikuwa kero kubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akipokea msaada huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Ndingo aliwataka wataalamu wa kutumia kifaa hicho kukitumia kwa uangalifu ili kisiharibike katika muda mfupi.
 
Hivi jamani huu ni msaada au ni wajibu wake yeye kuhakikisha anaowawakilisha wanapata huduma za kuridhisha iwe kwa kutumia marafiki zake ama mumewe.
Naona hapo katimiza wajibu tu wa kimsingi.
 
Nashangaa mtu anapotimiza wajibu wake anapewa hongera! HUO NI WAJIBU WAKE na hatakiwa kuishia hapo.

Tatizo Watanzania wengi hatujui kutofautisha kati ya haki na msaada (rights and a favour)
 
Nashangaa mtu anapotimiza wajibu wake anapewa hongera! HUO NI WAJIBU WAKE na hatakiwa kuishia hapo.

Tatizo Watanzania wengi hatujui kutofautisha kati ya haki na msaada (rights and a favour)
...Good point. Na wanasiasa wetu ndipo wanapowapigia bao watu wetu...2010 kwenye kampeni atakumbushia vyote alivyotoa kwenye hiyo hospitali ili aonekane kuwa alifanya kitu cha maendeleo na wadanganyika wanampa kura..
 
Anastahili hongera jamani maana kutimiza wajibu wako kwa Wabunge wetu ni utata sana maana wangapi wanatakiwa kufanya hivyo na wamefanyaje?mimi nampa pongezi sana .................moyo wake kusaidia kwa hali na mali uendelee....na wengine waioge mfano wake
 
Anastahili hongera jamani maana kutimiza wajibu wako kwa Wabunge wetu ni utata sana maana wangapi wanatakiwa kufanya hivyo na wamefanyaje?mimi nampa pongezi sana .................moyo wake kusaidia kwa hali na mali uendelee....na wengine waioge mfano wake

Hao ni marafiki zake binafsi angeweza kabisa kuwaomba zawadi ya gari akawa anatamba nayo mtaani, lakini kaomba zawadi ya kuwanufaisha wengi, hivyo anastahili pongezi.
 
Back
Top Bottom