Msanii Lucas Mhuvile, almaarufu kama Joti, anayepiga kazi kwenye kampuni ya Orijino Komedi, amemvisha pete mpenzi wake wa siku nyingi, ikiwa ni ishara na dalili njema kwamba safari ya kuelekea kwenye taasisi muhimu zaidi duniani ya NDOA imewadia..
Akiwa na swahiba wake wa siku nyingi, Mr. Mjuni Sylvatory a.k.a Mpoki, Joti alionekana mwenye furaha muda wote kwa kutimiza tendo hilo huku akiwa amealika watu wachache sana kuhudhuria tukio hilo.
Binafsi, nampongeza sana na kumtakia kila la kheri yeye pamoja na mwenza wake. Big up Joti!!!!
Aaaahh! Joti tukio muhimu kama hilo mbona umeniangusha namna hiyo?. Hiyo Back ground ya location ya tukio kama hilo hasa kwa status yako haviendani kabisa!
Kwani Pete ndo nn? Napata shida na haya mambo ya kuiga iga, km muoaji aoe tu hizi show za Pete zilifanywa sn na wema saivi kimya. Mi nahis ni kupata njia ya kuhalalisha zinaa tu bac.