Hongera Roma kwa kujaribu, Hongera Serikali kwa ukomavu

hamis77

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,642
19,018
Alichokiimba Roma Mkatoliki siyo kitu kigeni ktk siasa za upinzani nchini, sehemu kubwa ya alichokieleza Roma ni mwendelezo wa tuhuma na lawama za kila siku zinazotumiwa kujitangaza kisiasa na kuichafua serikali, haya ni malalamiko ambayo dhamira yake huwa ni kuituhumu serikali ktk nyanja mbalimbali huku wanaofanya hivyo wakijificha ktk kichaka cha UANAHARAKATI.

Kwa mtazamo wa haraka mashairi ya aina hiyo yanakuwa na lengo la kuikosoa serikali japo kwa Tanzania mara nyingi aina ya ukosoaji inayotumika inakuwa na lengo la kuichafua serikali kwa maslahi ya kisiasa au binafsi kutokana na jinsi ambavyo msanii hudhihaki kila kitu hata yale ambayo huonekana wazi kuwa ni mazuri.

Tungo za aina hii ni tungo ambazo siyo ngeni ktk maskio ya Wengi, kwahiyo ni busara kusema kuwa serikali itakapokuwa inaona hakuna shida ktk maudhui ya wimbo na hakuna aliyetukanwa ni vyema nyimbo za aina hii ziwe zinaachwa kama zilivyo bila serikali kuzizungumzia maana kitendo cha kuzigusa kwa namna yoyote ile ktk kujaribu kuzipinga au kuzifunga ni kuzipa 'publicity' ya bure (Kwa hili serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa)

KUANZIA awamu ya nne, Roma aliimba hivyo hivyo, nakumbuka wimbo wake mmoja uliwahi kufungiwa kwasababu ulikuwa na lugha ya matusi mabaya tena ya aibu sana wakati alipokuwa akijaribu kuukosoa utawala wa Kikwete, kwahiyo maudhui ya nyimbo za Roma siyo ngeni na 'hazishtui' hadhira, tukishtuka ndipo tutakuwa tumempa anachokitafuta (kick na huruma ya kisiasa)

Uhuru huu ambao serikali imeendelea kuuacha kwa wasanii ni uhuru mzuri sana cha msingi wasije kuvuka mipaka na kuanza kutukana watu au kutunga tungo zinazochochea MACHAFUKO, CHUKI na UVUNJIFU wa amani, hapo ndipo BASATA inapaswa kuwa makini sana na tungo mbalimbali kwa maslahi mapana ya taifa, lakini Basata ikijiridhisha kuwa hakuna shida hiyo basi wasanii waendelee kuwa huru kama walivyo sasa. Uhuru huu wa mawazo ni ushindi tosha dhidi ya yeyote aliyetaka kuitumia fursa hiyo kuendeleza propaganda za kuichafua Tanzania ndani na nje ya nchi.

Ukimya huu wa mamlaka inayohusika na sanaa na maudhui yake (Basata) na ukimya wa serikali unatoa tafsiri nzuri kuwa wimbo huo hauna shida yoyote ya KIMAUDHUI au KIMTINDO, kwahiyo wimbo uko sawa kabisa na waliokuwa wakisubilia 'Negative REACTION' mwitikio hasi wa serikali ili wamsaidie Roma kupata HIFADHI ya KISIASA nchini Marekani wameshindwa kwa kishindo ktk mpango WAO.

Kwahiyo busara ya serikali na viongozi wake utasababisha lengo la Roma kupata hifadhi ya kisiasa nchini Marekani kama mkimbizi wa kisiasa kukwama, maana kadri nchi inavyokuwa na wakimbizi wa kisiasa wengi kutoka makundi mbalimbali ndivyo ambavyo inatoa kigezo kikuu cha mataifa ya nje kuitangaza nchi husika kama nchi ya kidicteta. Mpaka sasa kuna mkimbizi mmoja pekee wa kisiasa ambaye ni mwandishi wa habari na aliyekuwa kiongozi wa CHADEMA kanda ya ziwa Ndugu Ansbert NGURUMO, Mange Kimambi alijaribu kufanya yote ili apate fursa ya kuwa mkimbizi wa kisiasa lakini mwisho wa siku alishindwa mpaka leo,ndiyo maana nasema wakati mwingine ukimya wa serikali ni dawa mbadala inayotibu bila kuumiza.

Hili la Roma, ni mkakati uliokuwa umeandaliwa vizuri sana baina ya baadhi ya watu ambao mpaka sasa wako Marekani wakisubilia agizo la Roma kukamatwa ili iwe tiketi ya Roma kupata hifadhi ya kisiasa. Kinachotafutwa hapa ni hoja moja kuwa WATU wanafungwa midomo kuongea nchini Tanzania, kinachotafutwa hapa ni kujaribu kuuthibitishia umma na dunia kuwa Tanzania hakuna uhuru wa watu kutoa mawazo yao nk, kwahiyo serikali na mamlaka zake wanapaswa kushughulikia mikakati ya aina hii kwa akili sana na siyo kukurupuka.

Jambo lingine jipya ambalo Roma hajawahi kulisema ktk nyimbo zake zote za kisiasa tangu ameanza mziki ni hili ALILOWAITA wenzake kuwa ni WANAFIKI, sijajua amewapima kwa mambo mangapi mpaka akahitimisha hivyo, lakini natumai aliowataja wanajua zaidi kuwa kwanini ROMA amewaita WANAFIKI (Hili tutaliangazia siku nyingine)

Na Magoiga SN
 
Ko unamanisha roma kapiga Ngoma af akacheza mwenyewe, 🤣 af mbna wimbo ushachuja tayar
 
Kama serikali ingetia kauli yoyote ingekua bonge la Kiki kwa roma. lakini jamaa wameuchuna wimbo unazidi kupolomoka.
 
Nchi haieleweki inapoelekea sasa hivi wala haieleweki nani ni kiongozi mkuu, nani mtoa maagizo, nani mtekelezaji na nani wakulaumiwa.

Kila kiongozi sasa hivi anafanya anachotaka na kutoa maagizo anayojisikia, na baada ya week akija kingozi mwingine anatoa lawama na kutoa maagizo mengine.

Imekua ni purukushani na tafrani kwa raia wa chini.
 
Kama serikali ingetia kauli yoyote ingekua bonge la Kiki kwa roma. lakini jamaa wameuchuna wimbo unazidi kupolomoka.
Hata Mwakyembe hakutakiwa kusema vile. Huu ukimya ulitakiwa uwe jibu tangu anaingia madarakani.
 
Hata Mwakyembe hakutakiwa kusema vile. Huu ukimya ulitakiwa uwe jibu tangu anaingia madarakani.
huyo mzee nayeye si ana kiherehere si unakumbuka alipokwenda kumsubiri wema sepetu wapi sijui hapo.hawa watendaji wa namna hii ndio wanaharibu mambo.

kimya ni jibu baya sana kwa asiyekutakia mema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom