Hongera Mzee Mugabe, hata mimi namkubali. Ni kiongozi mwenye maono na anajua watu wake wanataka nini. Mugaabe hakuchaguliwa na wazazi wake, kaka zake na wala marafiki zake kwa maana wote ama wamekufa au ni wazee sana na waliosalia ni wachache mno. Hii inatuonyesha amechaguliwa na watu wneye umri sawa na watoto wake na wajukuu.
Wanauna msimamo wake na wamesoma historia ya nchi yao. Hawakuyumbishwa na msimamo wa nchi za magharibi. Hongera sana wazimbabwe, mmetuonyesha njia na kasumba ya umri ishindwe na ilegee.