VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Napongeza na kutoa pole. Kwa watendaji wawili wa kiserikali. Wa kwanza, ninayempongeza, ni Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako. Ni jana tu, Waziri Ndalichako ameagiza kufutwa kwa mfumo wa GPA kwenye kusahihisha na kutoa matokeo ya mitihani kwa kidato cha pili, cha nne na cha sita.
Mfumo wa GPA ulikuwa ukipigiwa kelele na wadau wa elimu nchini. Ulikuwa ukionesha kuwa mitihani ilikuwa ikisahihishwa kwa kuwapendelea wanafunzi. Mitihani ilikuwa ikisahihishwa kisiasa ili ionekane kuwa elimu imeimarika kwa wengi kufaulu. Elimu iliendelea kushuka na kusawajika. Hata vyuoni sasa, wanaokwenda ni kama wasiokwenda.
Kuanza kurekebisha mfumo wa elimu ni hatua njema. Waziri Ndalichako unastahili pongezi na kupewa moyo wa kufanya kazi kuirejesha elimu yetu kwenye heshima yake. Anayefaulu afaulu kweli, anayefeli afeli kweli. Si kinyume chake kama ilivyokuwa. Madaraja ya kwanza, pili,tatu,nne na sifuri ni muhimu. Hata udahili vyuoni utakuwa rahisi.
Pili, natoa pole kwa Ndugu Eliakim Maswi. Ndugu Maswi alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara. Baadaye, mwka jana mwishoni, aliteuliwa kuwa Kaimu Naibu Kamishna Mkuu wa TRA. Jana, amerejeshwa Manyara kuendelea na kazi yake ya awali-Katibu Tawala wa Mkoa kwa kile kinachosemwa kuwa 'amemaliza kazi yake aliyotumwa TRA'.
Siasa hutumia maneno ya kisiasa na kisasa. Ndiyo hayo ya kumaliza kazi aliyotumwa TRA. Kiukweli, Maswi hakuweza kuhimili manenomaneno pale TRA kuwa yeye si 'msafi' kuendesha chombo kilichosafishwa cha TRA. Alihusishwa na sakata la Esrow. Maneno hayo yalimfikia Rais Magufuli. Rais akaamua kumuondoa. Hakuwa ameteuliwa kwa 'kazi maalum pale TRA'.
Nampa pole Maswi kwakuwa kuondolewa kwake TRA na kurejeshwa Manyara ni kama kushushwa cheo. Maswi ameondolewa kistaarabu kwa maneno ya kistaarabu. Hata watanzania wengi wameamini kuwa Maswi ameondolewa kwakuwa amemaliza kazi yake TRA. Ukweli uko tofauti na hivyo.
Pole Maswi kwakuwa Escrow is still haunting you Comrade!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam