Hongera Prof. Muhongo

Hongera Prof. Muhongo

wabongo mmezidi kupongeza pongeza
kwanza kachelewa kufanya alichofanya na ni wajibu wake kufanya yanayotakiwa kufanya
wenye tabia ya kupongeza pongeza ni damu ya magamba
karne hii sio ya kupongezana ni karne ya kuwajibika
 
ukisoma shule za ukweli na kupata degree basi kila kazi utaiweza. tofauti na degree za akina mulugo,huyu mzee jembe
 
Prof. Muhongo atatupeleka mbali sana kwa style hii ya uongozi. Ifike mahali mawaziri wengine waige mfano huu wa kushughulikia masuala nyeti yanayojitokeza kwenye wizara au sekta zao promptly badala ya kukaa kimya na kuwaacha wananchi wakihangaika.
 
Mtu akifanya kazi vizuri lazima apongezwe maana ni wengi wamepita Wizara hiyo na wamekuwa wanajinufaisha binafsi wakishirikiana na Muhando, sasa Muda wao umekwisha, tunamsubiri tena na Sarah Msafiri , eti aliniomba nnikamfuatie mkataba halafu niende nao nyumbani ataupitia, sasa kama mkataba huna maslahi nao inakuaje ukachukue na kwenda nao nyumbani kwako, na kwa nini mwenyewe hakwenda kuchukua husemi sababu za wewe kwenda kuchukua , je alikuwa azungushwa au la, ila weee utatumia Ubunge na urembo kupata mkataba, ayaaaaa weee naishia hapo
 
Mpongezeni tu huyo Prof Muhogo wakati asilimia 75 ya watanzania wanatumia vibatari hawana umeme.

Asilimia 5 ya wenye umeme ndio wanao uhakika wa kupata huduma hiyo kila siku huku asilimia 95 wakiwa katika mgao usio rasmi na serikali haitaki kusema kama kuna mgao.

Tupongezane kwa ujinga wetu watanzania na kuchezewa na watawala huku tukiwasifia kwa mambo madogo madogo yasiyo na tija

Mwanampotevu: Hapo nilipoweka red ni kwamba,Prof. Muhogo anajitahidi na ni jasiri sana tofauti na viongozi wengi ndani ya serikali ya sasa. Kazi yake si mambo madogo madogo kama ulivyosema. Tumpe ushirikianao na mawazo mbadala ya kujenga kama yapo badala ya kumbeza. Hivi ni kweli utendaji wake katika huu muda mfupi ni dhaifu kuliko wa yule waziri aliyemtangulia? Miaka zaidi ya 50 ya uhuru vibatari vipo kwa wingi tu, Prof Muhogo ana miezi mitano tu kazini hahusiki na kadhia hii tuwaulize waliomtangulia.

My take: Prof. Muhogo big up!!! don't give up, please make sure you stand out of the crowd by fighting corruption. Watanzania tumechoka sana juu ya ufisadi na rushwa tupe matumaini. Mungu akutangulie.
 
Siwezi kumpongeza mtu ambaye ametekeleza majukumu yake ipasavyo. sasa aliwekwa pale ili atekeleze kinyume au?? analipwa mshahara ili atekeleze majukumu yake na sio ili tuje tumpongeze, for what?????? Tusiwe wajinga kiasi hicho. Nyie ndio mnaowapa manesi hospitali asante kwa kukutibu, upuuzi huo kwani kazi yake nini??

Lazima niwakosoe pale wasipotekeleza majukumu yao kama wanavyoshindwa kusambaza umeme vijijini na kutuhakikishia umeme wa uhakika hawa wachache wanaopata. Ni jukumu lao ambalo tunawalipa mshahara wlaitekeleze, wasipotekeleza lazima tuwalaumu.

Tatizo sie watanzania tunaona kama viongozi wetu wakitimiza wajibu wao kuwa wametutendea hisani. huu ni umbumbumbu

Ina maana wewe hujawahi kupongeza au kupongezwa?
 
Back
Top Bottom