Hongera Prof. Muhongo

Hongera Prof. Muhongo

mkonomtupu

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
441
Reaction score
119
Kwa kuvunja bodi ya wafanyabiashara wanaoagiza mafuta ni hatua madhubuti ya kupambana na ukosefu wa nishati hii ambao umekua ukitokea nchini mara kwa mara.
 
Mpongezeni tu huyo Prof Muhogo wakati asilimia 75 ya watanzania wanatumia vibatari hawana umeme.

Asilimia 5 ya wenye umeme ndio wanao uhakika wa kupata huduma hiyo kila siku huku asilimia 95 wakiwa katika mgao usio rasmi na serikali haitaki kusema kama kuna mgao.

Tupongezane kwa ujinga wetu watanzania na kuchezewa na watawala huku tukiwasifia kwa mambo madogo madogo yasiyo na tija
 
Ameivunja PIC? What a move....hawa jamaa wa PIC ndio chanzo cha matatizo ya mafuta nchini.
 
Kwa kuvunja bodi ya wafanyabiashara wanaoagiza mafuta ni hatua madhubuti ya kupambana na ukosefu wa nishati hii ambao wkua ukitokea nchini mara kwa mara.

Mtoa mada naona umejichanganya Ninachojua amefuta leseni za wafanyabiashara walioomba kuagiza mafuta lakini hawaagizi wanafanya biashara ya mfukoni,amesema watachunguzwa kama wana uwezo wa kufanya biashara hiyo.

Kama nimekosea wanabodi mnisahihishe.hii ni kurekebisha wanaokurupuka kutoa mada.
 
na bodi ameivunja, ataiunda tena upya, au unataka source?
 
Nakupongeza prof Muhongo.Umeonesha ujasiri wa kuchukua maamuzi.Hayo ndo yalomshinda ngeleja.Natumaini wauza mafuta hawatatuchezea tena
bodi mpya ifanye kazi yake kwa weledi.
 
Unajua kukurupuka kubaya sana. Nakienzi kiswahili changu kwamba asiyejua maana haambiwi maana. Kaa na upumbavu wako kaka/dada Domy
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuvunja bodi ya wafanyabiashara wanaoagiza mafuta ni hatua madhubuti ya kupambana na ukosefu wa nishati hii ambao umekua ukitokea nchini mara kwa mara.

Lakini mhusika wa tatizo la mafuta ni Mwakyembe aliyeondoa wenye uwezo wa kuendesha bandari na kuachia washkaji na wasanii ambao wamegeuza upakuaji wa meli kuwa dili sasa foleni ya meli baharini zikiwamo za mafuta na general gargo na TRA walisaidia kutoa kibali yauzwe ya Transit, jambo ambalo nalo kimetoa mwanya wa ukwepaji kodi. Hapa tatizo ni ku wa sana kwa wanasiasa kuoneana haya. Nimemsikia Muhongo na pia Naibu wake, Simbachawene bungeni wote wamesema tatizo liko bandarini na huku kwa wwagizaji ni kachumbari kwa pilau aliyopika Mwakyembe bandarinu na hadi sasa anakomaa akichakachua ripoti ya kamati aliyoiunda mwenyewe
 
Ndugu yangu mimi nimempongeza mganga, sikutaka kutafuta nani mchawi. Ndio maana hatuendelei kwa kuweka visasi badala ya kuendelea mbele. Kuna vitu lazima tusahau kuhusu yaliyopita na tugange yajayo ili tuendelee. Sio kuweka visasi kwa kila kitu jamani. Kiranja
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu mimi nimempongeza mganga, sikutaka kutafuta nani mchawi. Ndio maana hatuendelei kwa kuweka visasi badala ya kuendelea mbele. Kuna vitu lazima tusahau kuhusu yaliyopita na tugange yajayo ili tuendelee. Sio kuweka visasi kwa kila kitu jamani

Si kutafuta mchawi, bali ni kutafuta chanzo cha tatizo ambacho bado hakijatatuliwa. Huwezi kuanza dozi ya malaria bila kujua kama ni malaria ama ni tatizo jingine.
 
Lakini mhusika wa tatizo la mafuta ni Mwakyembe aliyeondoa wenye uwezo wa kuendesha bandari na kuachia washkaji na wasanii ambao wamegeuza upakuaji wa meli kuwa dili sasa foleni ya meli baharini zikiwamo za mafuta na general gargo na TRA walisaidia kutoa kibali yauzwe ya Transit, jambo ambalo nalo kimetoa mwanya wa ukwepaji kodi. Hapa tatizo ni ku wa sana kwa wanasiasa kuoneana haya. Nimemsikia Muhongo na pia Naibu wake, Simbachawene bungeni wote wamesema tatizo liko bandarini na huku kwa wwagizaji ni kachumbari kwa pilau aliyopika Mwakyembe bandarinu na hadi sasa anakomaa akichakachua ripoti ya kamati aliyoiunda mwenyewe

mkuu unataka kusema Mwekyembe alikurupuka...
 
Unajua kukurupuka kubaya sana. Nakienzi kiswahili changu kwamba asiyejua maana haambiwi maana. Kaa na upumbavu wako kaka/dada Domy

Gamba ni gamba tu,we unafikiri source yako ndio ya wote,source uliyopata wewe sio niliyopata mimi ulitakiwa kutetea hoja yako mbona mwenzio Itnojec kanielekeza vizuri,wewe huna tofauti na Mwigulu inawezekana ndio mwalimu wenu wa matusi,wasalimie Magamba wenzako
 
Last edited by a moderator:
Hata mimi nampongeza sana kwa ujasiri huo maana hawa jamaa wakiona tu mafuta yameshuka bei wanatafuta njia za kuyapandisha...sasa bado Tanesco. Haitoshi kumuondoa Mhando, na Mboma na bodi yake waondoke ili umeme ushuke bei na tupate umeme wa uhakika kuanzia mjini mpaka vijijini
 
Mpongezeni tu huyo Prof Muhogo wakati asilimia 75 ya watanzania wanatumia vibatari hawana umeme.

Asilimia 5 ya wenye umeme ndio wanao uhakika wa kupata huduma hiyo kila siku huku asilimia 95 wakiwa katika mgao usio rasmi na serikali haitaki kusema kama kuna mgao.

Tupongezane kwa ujinga wetu watanzania na kuchezewa na watawala huku tukiwasifia kwa mambo madogo madogo yasiyo na tija

Acha kuwa myopic, Muhongo ana miezi mi5 tu, lkn kafanya mambo ya maana na yenye tija.
Na hivyo vibatali hajavileta yeye, japo atavipunguza taratibu pia.
Jifunze kuona kazi njema za watu na kuzithamini.
 
Nimegundua jamii forum siku wajinga wengi kuliko GT sasa am not here to argue bali kuelimisha. Wajinga kaeni na Ulugo wenu. Aka slip of the tongue
 
Acha kuwa myopic, Muhongo ana miezi mi5 tu, lkn kafanya mambo ya maana na yenye tija.
Na hivyo vibatali hajavileta yeye, japo atavipunguza taratibu pia.
Jifunze kuona kazi njema za watu na kuzithamini.

Siwezi kumpongeza mtu ambaye ametekeleza majukumu yake ipasavyo. sasa aliwekwa pale ili atekeleze kinyume au?? analipwa mshahara ili atekeleze majukumu yake na sio ili tuje tumpongeze, for what?????? Tusiwe wajinga kiasi hicho. Nyie ndio mnaowapa manesi hospitali asante kwa kukutibu, upuuzi huo kwani kazi yake nini??

Lazima niwakosoe pale wasipotekeleza majukumu yao kama wanavyoshindwa kusambaza umeme vijijini na kutuhakikishia umeme wa uhakika hawa wachache wanaopata. Ni jukumu lao ambalo tunawalipa mshahara wlaitekeleze, wasipotekeleza lazima tuwalaumu.

Tatizo sie watanzania tunaona kama viongozi wetu wakitimiza wajibu wao kuwa wametutendea hisani. huu ni umbumbumbu
 
Ikiwa wewe kwa kumpa mtoto wako zawadi tu hutaka aseme asante wakati ni wajibu wako kufanya hivyo,kwa nini prof sospeter asipongezwe?.

Maana wengine wanakabiziwa majukumu na kushindwa sasa kama yeye amweza apongezwe,acha wivu utakukondesha ndugu yangu,unadhani angefanya nini ndio ungempongeza? na je wewe ungekuwa kwenye nafasi yake ungethubutu hata kuvunja hiyo kamati?.mmezidi watu wengine kulaumu na kutoa takwimu na hi inaonekana kuwa ndio mtindi wa maisha sasa.

Kila mtu ni mjuzi wa kulalamika na sio kutoa soluhisho la matatizo,ebu jiulize katika ngazi ya familia yako tu wewe umeweza kukizi haja za wale wote wanaokutegemea?.
 
Ni majukumu yake lakini pia sina dhambi nikimpa hongera zake kwa kutekeleza majukumu yake kama ambavyo nitasema kwa Mwakyembe na Magufuri. Wale waoshindwa pia nitasema hamstahili hongera bali rekebisheni mtekeleze vyema majukumu yenu.

Hakuna haja ya kuwa na roho ya korosho. Je mjamzito akijifungua ukimwambia hongera kuna kosa gani. Basi mngekuwa mnapita tu kimya kimya na kusema ni jukumu lake ajifungue salama!! Hivi mbona kila mara watu wako kwenye masinagogi wanasema 'asante Mungu'; wanashukuru nini wakati ni majukumu ya muumba wao kuwabariki?

Muhongo elewa kuwa wapo wananchi wengi wanakutakia mema na uwajibikaji mzuri kama ambavyo kuna wachache pia wabaya ambao wao hawataki kuona kila raia anafuraia maisha hapa nchini. We kula mzigo nishati tuione wananchi watasimama upande wako.
 
Back
Top Bottom