Hongera Nchemba

Joined
Aug 19, 2021
Posts
38
Reaction score
58
Pongezi kwa Mh. Nchemba

Leo nasimama hadharani bila kupepesa macho. Ndio, nakupongeza kwa ubunifu wa kukusanya kodi bila manyanyaso kwa raia. Tulishuhudia maduka yakifungwa kwa ajili ya kodi, tulishuhudia ukadiriaji kodi usio rafiki kwenye biashara, tuliaminishwa kuwa serikali haikopi ila tulipe kodi nchi isonge mbele, kumbe ni danganya toto.

Ombi langu kwako, kodi unazokusanya zilete tija kwenye maendeleo ya jamii. Mshauri mama, gharama za umeme ziwe zileile tsh. 27,000,

Pili, serikali igharamie chakula shule za kata nchi nzima. Kumchangisha mzazi michango hii ni kukusanya kodi mara mbili kwa kitu moja. Mshauri mheshimiwa kuwa, shule moja ya kata yenye wanafunzi wa kidato cha 1 hadi 6 O-level wanashinda njaa na advance wanakula ni kutengeneza matabaka shuleni.
 
Unawaza kula tu na kusifia ujinga. Sijui unasoma shule gani ya kata nyau wewe!!
 
NAKUPONGEZA KWA UBUNIFU WA KUKUSANYA KODI BILA MANYANYASO KWA RAIA
UBUNIFU upi hapo amefanya..??? na tafsiri yako ya Manyanyaso ni ipi....???? Hizi double taxation wewe bado hujaona kama ni manyanyaso...


Hakika Bichwa Lisilo na akili ni adhabu tu kwa Miguu...au ni sawa na Banda la kufugia nywele.
 
Hizi ni ID za vijana wake.

Umeandika kwa herufi kubwa kuonesha namna swala lenyewe lilivyokugusa.

Zama za kudanganyana zineshapita.

You must come clean.

Nchi yetu sote.
 
UBUNIFU upi hapo amefanya..??? na tafsiri yako ya Manyanyaso ni ipi....???? Hizi double taxation wewe bado hujaona kama ni manyanyaso...


Hakika Bichwa Lisilo na akili ni adhabu tu kwa Miguu...au ni sawa na Banda la kufugia nywele.
Staha ya viongozi wetu ilipotea, yupo jukwaani kama vile Mondi anatumbuiza. Yaani utasikia kibwagizo “nitumbue, nisitumbue? ... Tumbua×2”, yaani ni unyama juu ya unyama. halafu kuna watu leo wanajifanya wanauchungu kuliko maovu yale. Usibishane na duni, fanya yako nenda zako. Dunia mali ya mungu, sote tutaiacha.

Imagine;

  • Waziri anatishiwa bastola
  • Waziri mkuu wa nchi anaambiwa "ukitaka kuandamana watangulize shangazi zako!”
  • Viongozi waliomtangulia na watoto zao wakaonekana ni mafisadi na wauza madawa ya kulevya.


Kwa maslahi ya watumishi sisemi chochote, dunia inatambua nini kilifanyika. Tumwombe Mungu asituletee uongozi wa namna ile tena.

 

#DOMOTOZO
kama unabisha weka picha yake uone. kwanza domo halafu tozo.
Yupo Makini
 
Mbwa mwenye mnofu mdomoni habweki. Mleta uzi nae inawezekana ana mnofu mdomoni au ndo mnofu unaandaliwa kwaajili yake
 
Mapinduzi ya Ufansa kupinga matumizi mabaya ya kodi na kulimbikiziwa kodi wanachi miaka ya 870 huko, bado kuna nchi za dunia hii iliyopo, yatajirudia punde!

Wananchi wanarundikiwa kodi na tozo kila pahala, halafu viongozi wetu ndio wanakwenda kuzitumbua watakavyo!.?

Hawana uchungu Kwa maisha magumu wanayoyaishi wananchi Kwa sasa..?

Wameziba masikio na wanaona mambo yako saw a tu!

Walishazoea kila kitu wanakuta vipo tayari Kwa kuliwa tu, hawajui bei zake huko mitaani,!

Kazi yao ni kujitengenezea semina, warisha na safari za hapa na pale ili wagawane kodi zetu Kwa kujilipa posho?

Hii ni mbaya na haiwezekani,
 

Tofautisha tozo na Kodi. Huwezi kutoza too kwenye mshahara uliokatwa payee na VAT huo ni wizi na dharau kwa raia. Ndio maana Rais alisema wananchi hawana shida wakitozwa tozo. Maana alishatudharau na kuona hatuna la kufanya.
 

Mwigulu amelipa vijana kuja kumsupport Jamii forum. Naona chawa wake wanampongeza kwa tozo huku nao wakiugulia maumivu. Hatuna serikali Bali wauaji wa uchumi, unakopa Sana, misaada Sana, Kodi inalipwa na tozo juu.
 
Mkiweka makodi,tozo na kukusanya
Na nyie mpunguze matumizi,msimamie vizuri fedha pia

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…