Hongera mhe. James Mbatia, Umeonesha njia kwa CHADEMA

Nicholas J Clinton

JF-Expert Member
Mar 13, 2014
877
486
Ni ukweli ambao unaweza kupinga kwa hoja kijana huyu ni very smart kwa kila anacho kifanya hasa baada ya kuchaguliwa kuwa waziri kivuli wa uchumi na fedha japo anashirikiana na chama kikuu chu upinzani CHADEMA ambacho kinaonekana kuyumba japo si sana kama watu wengi au wachache tunavyojua.

James Mbatia amekuwa akitoa hotuba zenye mashiko katika wizara yake mawazo ambayo hata Zitto Kabwe hajawahi kutoa leo nchi imezizima kwa badget nzuri ya UPINZANI iliyosomwa na kijana Mbatia huku wengi wakijua kuwa ni ya CHADEMA sasa nashudia kuwa budget ya serikali imebugi na hivyo kushauliwa na kutumia ya upinzani kwa 100% na hivyo kuupandisha hadhi ya CHADEMA Mbatia well done tujifunze kupitia kwako.
 
Hahahah hahahah UKAWA itawasumbua sana.

Yote hii ni chokochoko ya kutamani kujua modus operandi ya UKAWA. Poleni.

Ok. Tufanye tunakubaliana na baadhi ya maneno kwenye ulichoandika, basi mshaurini Rais Kikwete aende akajifunze kwa KUB Freeman Mbowe namna ya kufanya uteuzi na kupanga timu ya wachapa kazi serikalini.

Matunda ya utendaji kazi mzuri wa Baraza Kivuli Mawaziri ni matokeo ya uteuzi makini.

Mwambieni Kikwete afike kwa Mbowe (kama alivyosema mwenyewe jana CCM wasione aibu kwenda kupata mawazo ya kusaidia nchi) ajifunze kufanya uteuzi na makini unaozingatia KANUNI KUU ya kugawana majukumu SI vyeo kwa kuzingatia uwezo, uadilifu na umakini.

Akimaliza kujifunza hilo la uteuzi makini, pia ajifunze namna ya kufanya uwajibikaji wa kufuatilia utendaji kazi wa watu aliowateua na kuwapatia majukumu.

Kwa mtindo wa Kikwete na watu wake kufanya uteuzi kwa kugawana vyeo na kisha kuachia kila mtu atende ajuavyo kumeifanya nchi inaonekana Kama vile iko kwenye 'outo- pilot'.

Ndiyo maana tunawajibika kuiondoa CCM kwa haraka madarakani.
 
bajeti haiandaliwi na mbatia peke yake, yale ni mawazo ya kambi nzima ya upinzani bungeni, kwahiyo sifia kambi nzima, na kuiunga mkono katika harakati zake za kuwakomboa wananchi.
 
Kuna watu wamejaliwa kuchonganisha wenzao, kama mama shangingi vile. Kwani ungetoa hoja ya ubora wa Mbatia tu bila ya kuwagusia hao magwanda ingekuwaje?
 
bajeti haiandaliwi na mbatia peke yake, yale ni mawazo ya kambi nzima ya upinzani bungeni, kwahiyo sifia kambi nzima, na kuiunga mkono katika harakati zake za kuwakomboa wananchi.

Mwenzetu pale alipokuwa nasema "kambi rasmi ya upinzani bungeni inaitaka/inaishauri serikali" alikuwa hasikii, alisikia "mbatia naishauri serikali"
 
Jamani CHADEMA sijui matatizo yenu ni yapi yani nyie mnafuata upepo mna akiri kama za machine ya kusaga unga hasa wanaojiita washabiki wa CHADEMA naona nimewagusa sana mnataka msifiwe nyinyi peke yenu wakati huwa mnafanya ugoro muda mwingine Makene unatakiwa kuelewa nilicho andika na si kuniita gamba usiende kwa hisia kama bata fanya na sema unachokiamini kama kiongozi nani kakwambia mimi gamba uwe na adabu kijana. Mbatia kawasaidia pakubwa mbona hata Zitto hakuwahi kufanya hivyo leo kambi ya upinzani ikivunjika nyie ndo mtabaki profitable sasa mnatoa macho jifunze kukosolewa msiwaze kama kuku.
 
Ni ukweli ambao unaweza kupinga kwa hoja kijana huyu ni very smart kwa kila anacho kifanya hasa baada ya kuchaguliwa kuwa waziri kivuli wa uchumi na fedha japo anashirikiana na chama kikuu chu upinzani CHADEMA ambacho kinaonekana kuyumba japo si sana kama watu wengi au wachache tunavyojua.

James Mbatia amekuwa akitoa hotuba zenye mashiko katika wizara yake mawazo ambayo hata Zitto Kabwe hajawahi kutoa leo nchi imezizima kwa badget nzuri ya UPINZANI iliyosomwa na kijana Mbatia huku wengi wakijua kuwa ni ya CHADEMA sasa nashudia kuwa budget ya serikali imebugi na hivyo kushauliwa na kutumia ya upinzani kwa 100% na hivyo kuupandisha hadhi ya CHADEMA Mbatia well done tujifunze kupitia kwako.

Big up kikwete kwa kumteua mbatia kuwa mbunge na sasa serikali yetu inanufaika na ushauri wake. Big up rais.
 
Angalizo kwa mh. Mbatia,kuhusu hawa ccm magamba wanavyo jifanya eti kumsifia ni unafiki,wanataka wamsifie sifa kadekede akilewa sifa tu,wataanza kumrubuni kwa lengo la kudhoofisha UKAWA nasema hivyo maana hata Zito nae walianza hivihivi wakamsifia sana kila kukicha na Zito alipo lewa sifa akarubuniwa kwa lengo la kudhofisha Chadema na upinzani kwa ujumla.
Vilevile hiyo hotuba hajaandika peke yake ameandika kwa kushirikiana na wabunge wengine wa kambi rasmi ya upinzani,katika hali ya kawaida Mbatia hawezi kuandika hotuba peke yake bila kuwashirikisha wabunge wengine.
 
Ni ukweli ambao unaweza kupinga kwa hoja kijana huyu ni very smart kwa kila anacho kifanya hasa baada ya kuchaguliwa kuwa waziri kivuli wa uchumi na fedha japo anashirikiana na chama kikuu chu upinzani CHADEMA ambacho kinaonekana kuyumba japo si sana kama watu wengi au wachache tunavyojua.

James Mbatia amekuwa akitoa hotuba zenye mashiko katika wizara yake mawazo ambayo hata Zitto Kabwe hajawahi kutoa leo nchi imezizima kwa badget nzuri ya UPINZANI iliyosomwa na kijana Mbatia huku wengi wakijua kuwa ni ya CHADEMA sasa nashudia kuwa budget ya serikali imebugi na hivyo kushauliwa na kutumia ya upinzani kwa 100% na hivyo kuupandisha hadhi ya CHADEMA Mbatia well done tujifunze kupitia kwako.

Mbona alipoteuliwa kuwa mbunge mlikuwa mnadai ni kibaraka wa CCM, leo hii mnamuona mtu wa maana? Ama kweli politics ni dirty game
 
Mwenzetu pale alipokuwa nasema "kambi rasmi ya upinzani bungeni inaitaka/inaishauri serikali" alikuwa hasikii, alisikia "mbatia naishauri serikali"

We ni Ngonyani wa wapi usiyejitambua. Pa mdindifu waku. Uwe makini kwa ukombozi wa jamii ya Ruvuma.
 
Back
Top Bottom