Hongera Mh Rais, madini yetu sio ndizi, tukikosa uwezo wa kuchimba leo tusubiri hayataoza

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
HONGERA MH RAIS.
MADINI YETU SIO NDIZI, TUKIKOSA UWEZO WA KUYACHIMBA LEO TUSUBIRI, HAYATAOZA.

Nimewiwa kutoa hongera sana kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kusimamia marufuku ya mchanga wa kutoka migodini kutosafirishwa nje ya nchi yetu kwenye makontena.

Hakika kama taifa ni lazima tuungane na uamuzi huu katika kutetea rasilimali zetu na hasa madini yetu kwa faida ya nchi yetu.
Madini katika nchi ni zawadi toka kwa Mungu kwa taifa husika. Madini hakuna anayeyatengeneza wala aliyeyaunda isipokua Mungu.

Kila nchi imepewa tunu ya madini yake. Mataifa ya kiarabu ambayo sehemu kubwa ya ardhi ni jangwa hayalimi. Lakini yamepewa tunu ya mafuta. Leo hii ukienda Saudi arabia utapata kila tunda na chakula kinachopatikana duniani. Ni kwasababu wameyatumia mafuta yao kujenga nchi yao. Nchi za kiarabu ni matajiri wakubwa kwasababu ya mafuta yao. Hiyo ndiyo zawadi waliyopewa na Mungu.
Lakini waliisimamia vizuri rasilimali hiyo kwa faida ya mataifa yao.

Waarabu hawasafirishi mafuta ghafi kwenda nje ya nchi zao. Wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha wanachimba na kuuza mafuta yaliyosafishwa ili kuzuia kupoteza thamani na mapato.

Tukirudi nchini kwetu, sheria, mikataba na mazoea ya muda mrefu (hata kama ni mabaya) haviwezi kuwa juu ya maslahi ya taifa letu. Sheria tunazitunga wenyewe bungeni. Tuna nafasi ya kuweka sheria nzuri na kuipitia mikataba (kama ipo) na sheria (kama zipo) zinazotoa mwanya kwa rasilimali za taifa kusafirishwa kwenda nje bila kunufaisha taifa letu.

Hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema kuwa madini sio ndizi, kama hatutayachimba leo hayawezi kuoza (kuharibika).
Kama hatuna uwezo wa kutosha kuchoma mchanga wetu nchini ili tupate madini mbalimbali ni bora tusubiri hadi tupate uwezo huo kwa faida ya taifa.

Mchanga unaotoka machimboni migodini una madini mengi ya aina tofauti na yenye thamani kubwa.

Madini haya hubainika baada ya kuchomwa kwenye kinu mchanga huo.
Hivyo kwa kuruhusu mchanga usafirishwe nje ya nchi ambako hatujui nani anayechoma, wala madini yanayopatikana baada ya uchomaji, wala thamani yake ni sawa na kuruhusu nchi kuibiwa rasilimali zake huku tukibaki na mashimo ardhini mwetu (migodini).

Tuungane kama taifa kuunga mkono juhudi hizi za Mh. Rais kutetea rasilimali zetu kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadae.

Hatuwezi kuwa na reli ya kisasa, barabara nzuri, elimu bora, maji safi na salama na uchumi imara kama hatutalinda rasilimali zetu.
Tukumbuke madini huisha ardhini.
Ally S. Hapi
[HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG] kwanza
 
pamoja mkuu mimi pia namuunga mkono mhe. rais kwa dhati kabisa ya kulinda rasilimali zetu.chamsingi tujipange tuiletee nchi yetu maendeleo
 
Dhahabu yetu si mafuta useme Ulaya wanahitaji sana haya ni mapambo ambayo kuyaacha chini bado utachimba na kuwaomba wazungu waje wanunue hakuna ujanja na bei wapange wao
 
Wale jamaa wanywa viroba wakiona hii wanatamani wakulaani, thanks brother.
 
Ni bora tukawa na rundo la mchanga wenye madini ya dhahabu kuliko kuiibia nchi eti kwa kuusafirisha nje
 
Nimewiwa kutoa hongera sana kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kusimamia marufuku ya mchanga wa kutoka migodini kutosafirishwa nje ya nchi yetu kwenye makontena.

Hakika kama taifa ni lazima tuungane na uamuzi huu katika kutetea rasilimali zetu na hasa madini yetu kwa faida ya nchi yetu.
Madini katika nchi ni zawadi toka kwa Mungu kwa taifa husika. Madini hakuna anayeyatengeneza wala aliyeyaunda isipokua Mungu.

Kila nchi imepewa tunu ya madini yake. Mataifa ya kiarabu ambayo sehemu kubwa ya ardhi ni jangwa hayalimi. Lakini yamepewa tunu ya mafuta. Leo hii ukienda Saudi arabia utapata kila tunda na chakula kinachopatikana duniani. Ni kwasababu wameyatumia mafuta yao kujenga nchi yao. Nchi za kiarabu ni matajiri wakubwa kwasababu ya mafuta yao. Hiyo ndiyo zawadi waliyopewa na Mungu.
Lakini waliisimamia vizuri rasilimali hiyo kwa faida ya mataifa yao.

Waarabu hawasafirishi mafuta ghafi kwenda nje ya nchi zao. Wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha wanachimba na kuuza mafuta yaliyosafishwa ili kuzuia kupoteza thamani na mapato.

Tukirudi nchini kwetu, sheria, mikataba na mazoea ya muda mrefu (hata kama ni mabaya) haviwezi kuwa juu ya maslahi ya taifa letu. Sheria tunazitunga wenyewe bungeni. Tuna nafasi ya kuweka sheria nzuri na kuipitia mikataba (kama ipo) na sheria (kama zipo) zinazotoa mwanya kwa rasilimali za taifa kusafirishwa kwenda nje bila kunufaisha taifa letu.

Hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema kuwa madini sio ndizi, kama hatutayachimba leo hayawezi kuoza (kuharibika).

Kama hatuna uwezo wa kutosha kuchoma mchanga wetu nchini ili tupate madini mbalimbali ni bora tusubiri hadi tupate uwezo huo kwa faida ya taifa.

Mchanga unaotoka machimboni migodini una madini mengi ya aina tofauti na yenye thamani kubwa.

Madini haya hubainika baada ya kuchomwa kwenye kinu mchanga huo.
Hivyo kwa kuruhusu mchanga usafirishwe nje ya nchi ambako hatujui nani anayechoma, wala madini yanayopatikana baada ya uchomaji, wala thamani yake ni sawa na kuruhusu nchi kuibiwa rasilimali zake huku tukibaki na mashimo ardhini mwetu (migodini).

Tuungane kama taifa kuunga mkono juhudi hizi za Mh. Rais kutetea rasilimali zetu kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadae.

Hatuwezi kuwa na reli ya kisasa, barabara nzuri, elimu bora, maji safi na salama na uchumi imara kama hatutalinda rasilimali zetu.
Tukumbuke madini huisha ardhini.

[HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG] kwanza

NI SAWA, CHA MAANA UCHANGIE BUDGET YA TANZANIA
 
Mkuu maneno yako sawa .lakini ujuwe mikataba ya hao wachimbaji itatutia u maskini kwenye court za kimataifa .tujitayarishe
 
Tumeibiwa sana na maendeleo yanapatikana kwa kutumia chako vizuri ni wakati wa kujua thamani ya rasilimali zetu si kuletwa invoice tu tunataka kujua kile kinachopatikana si kusoma kilichopatikana
 
Back
Top Bottom