Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 879
- 969
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi mh. Selemani Jafo amefanya ziara ya kikazi mkoani Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea kiwanda cha kutengeneza madawati ya shule kilichoko wilayani Mbarali, kukagua ujenzi wa ghala la mpunga ambapo aliweka jiwe la msingi na baadae kutembelea kiwanda cha kuchakata mpunga Mbarali.
Aidha mh. Jafo ametembelea hospitali ya mkoa wa Mbeya ambapo alikagua maabara na wodi ya wazazi kabla ya kuzungumza na watumishi wa jiji na halmashauri ya Mbeya.
Katika hatua nyingine Mh. Jafo aliagiza madawati 150 kupelekwa katika shule ya Lusese iliyoko wilayani Mbarali baada ya kuitembelea na kukuta wanafunzi 400 wanakaa chini. Madawati hayo 150 yana uwezo wa kubeba wanafunzi 450.