Hongera Meya Jacob, kazi yako twaiona

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,284


HONGERA MEYA JACOB, KAZI YAKO TWAIONA.
Jacob ndugu kongole, kazi yako twaiona,
Umetangulia mbele, usiku pia mtana,
Upate neema tele, toka kwake subhana,
Kazi yako twaiona, kongole kaka kongole.

Hatuna khofu na ndwele, bima tatufaa sana,
Mafua ama upele, haraka twenda Amana,
Umelenga pelepale, afya mbadala hana,
Kazi yako twaiona, kongole kaka kongole.

Tumelima ili tule, wote ama kupeana,
Tuachane na ukale, ule wa kuoneana,
Tusirudi kulekule, tulipo paacha jana,
Kazi yako twaiona, kongole kaka kongole.

Nimesoma vipengele, ili nipate bayana,
Madawati kwa mashule, bajeti imeliona,
Taka hasa za Tandale, zitaisha imenena,
Kazi yako twaiona, kongole kaka kongole.

Fadhila yake tungule, kwa nyama iso nona,
Imewafanya wafule, tumbo mfano hakuna,
Haina kipaumbele, kwa waja wenye khiyana,
Kazi yako twaiona, kongole kaka kongole.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
whatsapp/call 0622845394 Morogoro
 
Nimpe kongole pia ,pamoja na madiwani wote wa kinondoni....ukwel uwazi Meya Jacob ....habahatishi anatumikia wananchi ,bajeti aliyoisoma kwa niaba ya baraza la madiwani kinondoni imetoa mwelekeo mzuri sana .......naomba wengine igeni ...ni bajeti ya wanyonge ,yenye mikakati madhubuti ya kufuta ujinga na maradhi kabisa.........
 
Wale mameya wa ccm waliopita sijui wanaficha wapi nyuso zao, kazi ilikuwa kuwaficha wauza unga tu, na kwa jinsi wanavyoisoma namba nao sasa watakuwa wateja wa huo unga.. Hongera Jacob, kaza buti uibadilishe kinondoni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom