Hongera Magufuli na Museveni kwa kuikataa EPA ya kikoloni.

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
16,349
26,498
Economic Partnership Agreement~EPA, ni mkataba uliopigiwa upatu saana na nchi za Ulaya.
Ati "Partneship Agreement" hii lengo lake ni kuondoa kodi na vikwazo vyote vya bidhaa za viwanda kibiashara kati ya Afrika Mashariki na nchi za Ulaya.
Msingi wake tu ni kutimiza masharti ya ubora na umadhubuti wa bidhaa.

Mtu yeyote angeweza kuona mtego ambao nchi za EAC zingeingia wangekubaliana na mkataba huo.

Wazungu wangesema kwa urahisi,sukari, bia,mfuta ya kupikia au nguo zetu hazina ubora na viwango kuingia ulaya.
Wakati huo huo siye tungejaziwa hapa cheap european products hivyo kujigeuza kuwa soko lisilo na kodi kwa nchi za ulaya.

Wakati mwingine nakereka kufikiri, huwa hawa wazungu wanatuonabsisi ni wajinga kihivyo?

Hivyo nawapongeza marais John Pombe Joseph Mgufuli na Kaguta Museveni kwa kuwapa za uso wazungu hawa.
 
Inafika wakati na kipindi kama walivyofanya wenzenu wa UK, uhusiano ni jambo jema lakini kumbuka "wema usizidi uwezo"
issue ya kuikacha EPA naiunga mkono ila UK na brexit yao naona kama wamechemka aisee
 
Economic Partnership Agreement~EPA, ni mkataba uliopigiwa upatu saana na nchi za Ulaya.
Ati "Partneship Agreement" hii lengo lake ni kuondoa kodi na vikwazo vyote vya bidhaa za viwanda kibiashara kati ya Afrika Mashariki na nchi za Ulaya.
Msingi wake tu ni kutimiza masharti ya ubora na umadhubuti wa bidhaa.

Mtu yeyote angeweza kuona mtego ambao nchi za EAC zingeingia wangekubaliana na mkataba huo.

Wazungu wangesema kwa urahisi,sukari, bia,mfuta ya kupikia au nguo zetu hazina ubora na viwango kuingia ulaya.
Wakati huo huo siye tungejaziwa hapa cheap european products hivyo kujigeuza kuwa soko lisilo na kodi kwa nchi za ulaya.

Wakati mwingine nakereka kufikiri, huwa hawa wazungu wanatuonabsisi ni wajinga kihivyo?

Hivyo nawapongeza marais John Pombe Joseph Mgufuli na Kaguta Museveni kwa kuwapa za uso wazungu hawa.

hatuna tu hivyo viwanda....wala hatuna bidhaa za kusafirisha ..na isipokuwepo sio kwamba hio sukari watainunua na bado tununua kutoka kwao vifaa mbali mbali na spares..ingekuwa tuna mkataba huu vingeingia kwa uraihisi..tunahitaji viffaa vya mahospitali na kilimo kwa bei poa..
hatuna mbinu tu za ku negotiate ..mkataba ni pande mbili kama kuna kipengele kina shida you seat na ku discuss sio mkataba wote mbaya ..kuna faida nyingi zaidi kuliko hasara...
 
Back
Top Bottom