Hongera magufuli kwa kujirekebisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera magufuli kwa kujirekebisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jatropha, Apr 5, 2011.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Tofauti na ilivyokuwa tabia yake huko nyuma ya kuamini kuwa Wizara ya Ujenzi na wakala wa barabara TANROAD ndio Alfa na Omega katika masuala ya barabara, jana wakati wa uzinduzi wa barabara ya Bagamoyo Mhe John Magufuli licha ya kuonyesha mbwembwe alizozizoea alioneka dhahiri kutii na kutekeleza kwa vitendo maagizo ya Waziri Mkuu na Raisi ya kupunguza ubabe na kujali "Collective Responsibility" pale alipomwambia Rais Kikwete kuwa kazi ya kuwaondoa wafanya biashara waliokuwa katika eneo la hifadhi ya barabara eneo la Tegeta tayari imeanza kutekelezwa na ngazi ya Mkoa na Wilaya ambapo Mkuu wa Mkoa amekwishamuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ndg Jordan Rugimbana kuwaondoa wafanya biashara husika. (Gazeti la Majira la Tar 5 Aprili 2011) limeandika habari hiyo vizuri sana bila ya ushabiki wowote.

  Nachukua nafasii hii kumpongeza Mhe Magufuli kwa kukubali kushuka na kushirikiana na viongozi wa ngazi za Mikoa, Wilaya n.k ambao ameelekezwa kushirikiana nao ili kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwa pande zote katika ujenzi wa barabara yaani Serikali na wananchi.

  Hali hii ya Serikali kuanza kufanya kazi kama timu moja ndio pia ilifanikisha ujenzi wa barabara ya Dar hadi Mlandizi mwaka 2001, ambapo wananchi walioathirika ni wale tu waliokuwepo katika eneo linalihitajika na ujenzi wa barabara kwa wakati huo na si vinginevyo.

  Ni dhairi kuwa ushirikiano kati ya ngazi mbali mbali za Serikali, ujenzi za barabara hapa nchini utafanyika kwa ufanisi na kasi kubwa pasipo kuwepo malalamiko yasiyo ya msingi kutoka kwa wananchi hususan walioko nje ya eneo ambalo kisheria ndio linatambulika kama hifadhi ya barabara yaani Mita 22 kutoka katikati ya barabara; awali kabla ya maagizo ya kusitisha bomoa bomoa kutolewa na Wazri Mkuu na kubarikiwa na Raisi, Mhe Magufuli alikuwa ameagiza wananchi walioko nje ya Mita 22 kuwekewa alama za X na nyumba zao zibomolewe, na hiyo kuwa kiin cha malalamiko.

  ibara ya 27 (2,4,5) za Kanuni za Sheria mpya ya barabara namba 13 ya 2007 zilizopitishwa kupitia Tangazo namba 21 katika Gazeti la Serikali la tar 23 Jan 2009 inamtaka Waziri wa Ujenzi endapo anataka ardhi yoyote itumike kama barabara au kuongeza eneo la hifadhi ya barabara kama alivyofanya kupitia Ibara 29 ya Kanuni hizo zilizopitishwa 2009 na hivyo kupendekeza eneo la hifadhi ya barabara kuongezwa kutoka Mita 22 hadi 30, kufanya mawasiliano na Waziri wa Ardhi kwa lengo la kuhifadhi ardhi husika, ikiwa ni pamoja na kufanywa kwa tathmini ya kutambua wananchi waliopo katika eneo hilo na thamani ya mali zao ili walipwe fidia kwanza ndipo watakiwe kuondoka miezi sita baada ya kulipwa fidia.

  Ninamsihi Mhe John Magufuli aachane na utaratibu wa mamlaka moja kujitwalia majukumu ya mamlaka zingine kama ilivyotokea pale alipoiagiza TANROAD kuwekea nyumba za wananchi nchi nzima alama za X na kutaka zibomolewe hata katika maeneo yaliyoko nje ya Mita 22, ambayo kisheria Wizara ya Ardhi haijayahifadhi kama sehemu za barabara na hifadhi zake. Na badala yake adumishe ushirikiano mpya ulioanza kujengeka baina ya Wizara ya Ujenzi, TANROAD, Mikoa, Wilaya n.k kwa kuwa sekta ya barabara ni mtambuka, kwa kufanya hivyo atalipatia tatizo la hifadhi za barabara kuvamiwa ufumbuzi wa kudumu.
   
 2. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  kaufyata mkia kama m*w*,kadhalilishwa na jk na pinda hadharani lakini kwa uroho wake wa posho za uwaziri kaendelea na cheo chake,..lolote analosema sasa hivi litakuwa linadharauliwa na kila mtu,..he dserves all the humilation boot licker...
   
 3. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  lakini hiyo rekodi ya 2001 kama kumbukumbu zako zikoo vizuri ni huyo huyo Magufuli alikuwa waziri acha kujadili
   
 4. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Hapa hatuzungumzi masuala ya rekodi, ninyi ndio mnaowatia vichwa na viburi viongozi mafisadi wa sasa, zamani kazi nzuri ikifanywa na Serikali sifa zilizkuwa zikienda kwa Serikali nzima na chama. Tanzania iliwahi kujenga barabara kibaop huko nyuma, ikajenga viwanda, ikajenga mashamba makubwa n.k. Lakini vitendo vyenu na wandishi uchwara kuwamwagia sifa watu binafis badala ya tasisi ndio inachoche ufisadi hapa nchini.

  Tunazungumzia reality, halafu napenda ukitaka kujadili thread yangu uweke kifungu cha sheria ya kile unachopinga, maana washabiki wengi wa Magufuli mnamini yeye ni muumini mzuri wa kufuata sheria, mlijuaje kuwa anafuata sheria wakati ambapo hizo sheria zenyewe hamjawahi kuziona sembuse kuzisoma. Hii ni ishara kuwa mnachukua maneno na kauli za vinywani
   
 5. Panga La Shaba

  Panga La Shaba JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 209
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pamoja na kusifiwa sana,Magofuli ufanyaji wake wa kazi na mfananisha Mrema Augustine alipokuwa waziri wa mambo ya ndani.......kwanza Magofuli ni mtu ambaye anapenda cheap popularity......kama kweli anauchungu na nchi mbona pindi wa uhuzwaji wa nyumba za serikali ndie aliyeshikilia kidedea nyumba ziuzwe......Mimi na muona kama ni mtu wa Jeuri,Zarau, Kiburi.....
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,600
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Nyumba zilizopangwa kubomolewa zitabomolewa tu, iwe sasa au mwakani au 2016! wala msipeane moyo!

  JK hakukataza magufuli kuvunja nyumba, kama hamumjui JK subirini muone moto wake na rangi zake halisi

  Leo kafukuza mtu na mabati yake ..HARAKA..same style ambayo hakutaka magufuli aifanye

  JK ndiyo anataka popularity, kasema, kamaliza, kasifiwa na nyie..lakini ubomoaji uko pale pale!! haikwepeki!
   
 7. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Shida yenu waote mnaochangia thread hizi za Mgufuli ni mambumbumbu wa sheria, hamleti arguement za kisheria mnaleta ushabiki tuu. Haiwezekani mtu mzima katika masuala ya kisheia utegemee kichwa cha Magufuli halafu utake kuzungumza wanaume wenzio wanapataka kuzungumza wakati kichwani hamna kitu kuhsu hoja husika.
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,600
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280

  Unajua sheria kuliko Mwakyembe? au Magufuli anajiamulia tu na Mwakyembe hana nafasi?

  cheers!
   
 9. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  RED-NI LAZIMA MTU UJIAMINI BAADA YA KUTAFUTA NA KUSOMA SHERIA HUSIKA, SISI KAMA WENGI WETU AMBAO HUTEGEME MATAMSHI YA MAGUFULI NA WAO KURUKIA KUWA NDIO SHERIA.

  GREEN-BAADA YA KUFUATA UTARATIBU UNAOTAKIWA NA KUWASHIRIKISHA WASAIDIZA WAKE WANASHERIA NDIO MAANA LEO KWA MMARA YA KWANZA NIMEMPA MAGUFULI PONGEZI, KATIKA GAZETI LA MAJIRA AMENUKULIWA KUWA ATASHIRIKIANA NA MWAKYEMBE NA BALOZI MTANGO AMBAO WOTE NI WANASHERIA. nNIO MAAN KAZI YA KUWAONDOA WAVAMIZI WA HIFADHI YA BARABARA HAPO TEGETEA INAFANYWA NA MKUU WA MKOA NA WILAYA KAMA ALIVYOSHAURIWA NA WAZIRI MKUU, TOAFAUATI NA ALIVYOTAKA ZOEZI HILO KUENDESHWA NA TANROAD KIMABAVU.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Hajajirekebisha na hawezi kusameheka kamwe -- yeye na Ben Mkapa. Walivunja sheria (na pia katiba) kwa kuuza nyumba za serikali kinyume kabisa na sheria katika usiri mkubwa ambao unaonyesha kulikuwapo ufisadi.

  In fact tunaweza kusema alishiriki kikamilifu katika kujigawia nyumba zilizotokana na hela za walipa kodi. Magufuli anayo dhambi kubwa sana ambayo haiwezi kufutika labda kwanza atubu mbele ya wananchi na sidhani kama wanaweza kumsamehe.

  Kuchecheka kwake kote huko na kujifanya eti ni 'mchapa kazi' niu unafiki mtupu -- ni fisadi wa kubobea. Wananchi -- mbona tunadanganywa kirahisi namna hii.
   
 11. k

  kibokogiziba Member

  #11
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha tabia kama hii maana mtu lazima ubadilike na jkubali kukosolewa . Hivi ni nani asieteleza ? tumia hekima kujenga nchi na kua na subira kijana hasira hasara kwani magufuli bado anahitajika na yeye anaelewa hilo ndo maana bado ana moyo wa kuwatumikia watanzania.
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Magufuli na Mkapa wake wana dhambi ya kuuza nyumba ambayo wananchi hawatawasahau mpaka waendapo kaburini na vizazi vijavyo vinaweza kuyachapa viboko makaburi yao!!
   
 13. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wengi wao ni wana chama wa chama kile kinacho amini kila jambo ni kuandamana tu! Hivyo kuchangia kwao utawaona tu! Ubongo wao umekaa kimaandamano tu wakiita pipizi pawa!
   
Loading...