Hongera Lema kwa kubadilika

Hongera Lema kwa kubadilika

Arusha sasa itatulia.sana labda.mpaka wakati wa uchaguzi tena.maana chadema wamepata haki yao ya kuongoza ... Issue iliyobakia ni ya umeya ambayo nafikiri chadema wameweza kupata njia mbadala za kudeal naye

Ushindi wa 4-0 umeiweka Arusha sawa,'magamba yamenywea' na uchaguzi wa kata ya Sombetini wanauogopa kwani wanajua hawana chao pale ndiko waasisi wa mageuzi katika jiji la Ars.Jana walikuwa na mkutano waliouandaa wiki nzima kwa wakazi wote wa Arusha lakini mahudhurio ilikuwa aibu hawakuzidi watu 15,ilibidi mkutano ufupishwe ufanyike kwa nusu saa tu."wanatia huruma" sijui 2015 watakuwaje!!!
 
Heshima haiji hivihivi, huwa inajengwa na wakati mwingine kwa gharama kubwa! Ndicho Lema alichokuwa anafanya muda uliopita, kitu ambacho wewe ulikuwa huelewi!
 
Hivi ndivyo nilivyoandika July 2, 2012

[h=2]Kurekebishana: Lema badilika[/h]
Mimi ni kijana ambaye kwa sasa nina makazi nje ya nchi lakini ni kijana niliyekulia Arusha. Nilipoenda Arusha mwezi wa tatu kuna vitu ambavyo sijafurahia. Kwanza ni kile kitendo cha Lema kuwaambia watu sokoni wafanye wanachotaka na hivyo kufanya watu kuanza kuuza vitu barabarani bila utaratibu wa mji.

Pamoja na kuwa na demokrasia haina maana watu wa mipango ya mji wapuuzwe ni lazima kuwe na utaratibu wa kufanya biashara na kufungua vigenge. Vilevile kuhusu sehemu nyingine za maandeleo kama sehemu za kujenga masoko ya kisasa na miji ya kisasa. Ni kweli kwamba kama mbunge Lema anatakiwa kuhakikisha hakuna kufukuzwa watu kwenye maeneo lakini ni lazima vilevile Lema ahakikishe ujenzi na maendeleo ya mji wa kitalii Arusha unafanyika.

Malalamiko ya wananchi ni muhimu lakini huwezi kufurahisha kila mtu mmoja mmoja utakiwa uangalie Project na manufaa ya Arusha kwa ujumla. Vilevile Lema unatakiwa ujihusishe zaidi kwenye kutangaza Arusha nje ya nchi, kwenye balozi, na kufanya kazi na wizara ya utalii maana wana zile contact za groups za kifaifa za wageni lakini sijawahi kukusikia unafanya chochote. Kwenye Meeting ya Diaspora ya Marekani na uingereza ungekuja kutangaza Arusha maana wewe ni mbunge wa mji ambao unategemea utalii lakini sijakuona mwaka jana pale Virginia ingawa kulikuwa na watu wengi wa kampuni ya utalii.

Sijawahi kusikia Lema unafanya mkutano na wafanyabishara wote wa Utalii na biashara nyinginge Arusha na kuwauliza shida zao ni zipi Arusha ni mji wa biashara hivyo huwezi kuongelea chadema pekee.

Pamoja na ukweli kwamba umefanya kazi nzuri ya kueneza chama Arusha ni wakati wa kuongea biashara na kusaidia kuleta maendeleo Arusha.​
 
Unayajua maneno japo hujui maana yake! Lema hakubadilika bali he is pragmatic; landscape ya kisiasa hapa Arusha imebadilika sana baada ya Brush ya 4 kwa Zero! Sijui kama una habari kuwa Lema sasa anahudhuria vikao vya Madiwani na Meya wa kichina Lyimo ndie anakwepa vikao, makamanda wako ulingoni hana majibu ya hoja kibao za tuhuma za ufisadi!

Lema anahudhiria vikao ili kuganga njaa tu.
 
Unayajua maneno japo hujui maana yake! Lema hakubadilika bali he is pragmatic; landscape ya kisiasa hapa Arusha imebadilika sana baada ya Brush ya 4 kwa Zero! Sijui kama una habari kuwa Lema sasa anahudhuria vikao vya Madiwani na Meya wa kichina Lyimo ndie anakwepa vikao, makamanda wako ulingoni hana majibu ya hoja kibao za tuhuma za ufisadi!




hajapelekwa Mahakani?
 
LEMA:"Ni afadhali vita inayodai haki kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mtu".

Hongera kamanda Lema kwa kupigania haki za wanyonge bila kuchoka,kiongozi wa kweli ni yule aliyekubali kujitoa kwaajili ya waliomchagua,tunakuunga mkono na tutapambana nawe bega kwa bega mpaka kieleweke.
"SAUTI YA UMMA NI SAUTI YA MUNGU"

TULIANZA NA MUNGU
TUKO NA MUNGU NA
TUTAMALIZA NA MUNGU
 
Back
Top Bottom