Kuna sehemu ambayo tumekosea, tunakosea, na tunaendelea kukosea. Watanzania walio katika fani mbalimbali wamekosa ujasiri na uthubutu wa kufuata misingi ya sera ya Kibepari inavyohitaji.
Sera za kibepari (Capitalism) ingawa hazisemi wazi lakini zinamtaka mwanadamu awe mbinafsi katika maisha yake ya kila siku na awe makini katika kujijali mwenyewe kwa umakini mkubwa pamoja na Familia yake.
Ni katika Ujamaa tu ndipo ambapo mtu anaishi kwa ajili ya watu wengi waliomzunguka, pamoja na Serikali yake. Wanamichezo wetu na wasanii wamelala katika dunia ya zamani.
Wamelala katika dunia iliyowaaminisha kwamba wao ni wasanii au wanamichezo wa serikali pamoja na wananchi wake. Matokeo yake, matatizo mengi yanayowatokea katika siku za usoni wanayalaza katika mikono ya Serikali pamoja na Wananchi.
TAFAKARI