Hongera jk lakini..........?..soma hii!

LENGEJU BOB

Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
53
Points
0

LENGEJU BOB

Member
Joined Nov 1, 2010
53 0
Suala la Luhanjo kutofautiana kimaamuzi na Boss wake
Ikumbukwe pia Ofisi ya Luhanjo ipo IKULU, si ajabu hata makazi ni hapohapo!

SIDE A.

1. Kama Luhanjo alifanya maamuzi bila kumjulisha Boss wake, hiyo inaitwa "Working around" na ni Dharau ya hali ya juu
2. Kama Luhanjo alikubaliana vingine na Boss wake na akatenda vingine, hiyo inaitwa "working against" ambayo ni usaliti usiomithilika

Kwa yote mawili, if he ever worked around or against his Boss; an easy assumption following an immediate intervention from his Boss.... It is in deed a blunt suprise that Mr. Luhanjo is still the Country's Chief Secretary, in state office, a smelling distance from the State Head!.....Blasphemy!

SIDE B.
Katika mifumo kadha wa kadha ya utendaji kazi wa serikali nyingi duniani, linapokuja suala la Sera au Jambo jipya ambalo serikali inakusudia kuliwasilisha na kilitekeleza, Kwa kawaida kitengo ya planning, mikakati kwa kushirikiana na watu wa propaganda hupeleka suala hilo kwenye jamii katika namna ya kujaribu hivi...kupima Public opinion, Public support na hata wakati mwingine Public sympathy.

Hapa, suala fulani, hata liwe la kipuuuzi, mtu mmoja (wa ngazi ya juu-kati)huteuliwa kubeba jukumu la kuvujisha imformation....kusambaza na hata kutoa Tangazo rasmi la kiserikali juu ya suala uwepo wa suala hilo... Kama jamii ikilipokea vema suala hilo...Haraka mtandao mzima unabeba bango, kwamba mpango uliokubaliwa actually ni msimamo wa serokali nzima ikiongozwa na Kiranja Mkuu...na hata mara kadhaa huweza kuchukuliwa kama ugunduzi binafsi wa Mheshimiwa.Hii husaidia si tu kutengeneza CV ya mkuu wa nchi lakini pia kuwapa imani watawaliwa juu ya watawala wao.. Ikiwa sera, suala au jambo linalojaribiwa litapokelewa kwa hasira na wananchi...basi Serikali inajikausha, ionekane ni msimamo binafsi wa huyo kiongozi aliyelizua, hakutumwa na mtu na mara chache hata huweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu (kisanii). Lakini kwakuwa ni mkakati wa kitaalamu kujua msimamo wa jamii kuhusu suala flani, mhanga wa matokeo ya utafiti huu huweza kunufaika kwa namna nyingine hata baada ya kufukuzwa kazi. Hapa ndo unakuta mtu amehamishwa kutoka mkuu wa mkoa kwenda kuwa katibu wa wizara n.k (Siri ya mtungi ajuaye kata).

ANGALIZO:
Hayo yote hufanyika kuangalia uwezekano wa kusimika sera muhimu ambayo kuwepo au kutokuwepo kwake ni kwa usalama, ustawi na manufaa ya NCHI.. Kamwe haiwi katika masuala yaliyo wazi kabisa kama wizi wa pesa za nchi.Hapa ndiko ambako nahisi washauri wa ofisi ya kiongozi wetu wa nchi wameshindwa kabisa kuhusianisha maudhui ya Technique hii ya kupima 'Public Opinion'..Wao wanatumia hata kupima upuuzi.....Haitumiki hii mahala ambapo ni wazi mtu au watu wamekwapua pesa za Umma kwa mtindo wa Harambee isiyotambuliwa kikatiba wala na sheria yoyote ya nchi, sheria ya fedha, ya mapato, ya matumizi wala sheria yoyote ya michango ya umma.. Hakuna namna ambayo mtu , taasisi, au taaluma yoyote inaweza kuhalalisha upuuzi huu. Na katika nchi zilizopiga hatua ya kuheshimu sheria, taratibu na haki, hasa linapokuja suala la kusimamia heshima ya nchi na wananchi, suala hili lisingehitaji tume ya Rais, Mkaguzi wa mahesabu wala kamati ya Bunge...ni suala la kukamata wezi na kuwafikisha mbele ya sheria..Lakini pengine hatujafika huko, ingawa very soon tutafika!

Fikiriria mtu anaonekana hana hatia kwakuwa alituhumiwa kuiba ng'mbe kumi lakini kakutwa na ngo'mbe wa tano tu wa wizi! Waliomtuhumu ni waongo, mmesema Bilioni...wakati ni Tumilioni mina tani tu! (Ze Komedi)...Tena kama haitoshi anarudishwa kazini kwa kiburi na mbwembwe, anapokewa kwa mavuvuzela na akikanyaga zulia jekundu..wenye akili timamu na vitambi vikubwa wanasukuma gari lake, naye bila aibu anatangaza "kuwasamehe waliomtuhumu"....Jamani...Luhanjo.....Mh. JK......Huku ndiko kupima public opinion kweli?
I think this is more like testing a Public Patience and/or Public Anger....

wahenga walishasema....Ncha ya Mkuki haipigwi kwenzi na Sumu haijaribiwi kwa kuilamba...
SOMENI MAANDISHI UKUTANI!
 

Forum statistics

Threads 1,356,559
Members 518,911
Posts 33,133,121
Top