Actually he's trying to paint a scenario that doesn't Exist ! CCM kweli hizi bakora chache hivi zimewarudisha kwenye line? na bado watakiona cha mtema kuni.............!
Whats the difference.....hujafurahi CHADEMA kushinda
umefurahi LOWASSA kushindwa......
i know you are happy leo.....
Mie bado sijaelewa anaposema nyie ni watani wao. Huu utani umeanza lini? Maana huko nyuma alikuwa wanawaita Chandimu mara ghafla bin vuu sasa mmekuwa watani. Kawapandisha daraja kutoka Chandimu mpaka watani kwa uchaguzi mmoja tuu?
Ndg.Nape,
Hongera pia kwa kata mlizoshinda.Tunaomba ustaarabu huu wa kukubali kushindwa muendelee nao hadi 2015.Uchaguzi umekwisha tujenge nchi yetu.Ningependa kuwashauri msije mkaingia mtegoni kwa kutafuatana wachawi.Jitahidini kuishinikiza pia serikali yachama chenu kutekeleza ahadi za uchaguzi uliopita wa mwaka 2010.Katika utekelezaji wa ahadi za uchaguzi,CCM ni mfano mbaya kwa vyama vingine na mmekosa moral authority ya kuhimiza vyama vingine katika utekelezaji wa ahadi
Mkuu kama ulikuwa nami kwenye mawazo yangu! Vita ya panzi ......hujafurahi CHADEMA kushinda
umefurahi LOWASSA kushindwa......
i know you are happy leo.....
Chama Cha Mapinduzi, kimeyapokea matokeo ya kura zilizopigwa na kutangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi kwa chaguzi ndogo zote, ule wa Arumeru Mashariki na zile za kata nane zilizofanyika jana nchini kwenye maeneo husika.
Kwa heshima nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati watani zetu, CHADEMA kwa ushindi walioupata Arumeru Mashariki na kwenye kata tatu(Kirumba, Kiwira na Lizabon). Lakini pia nawapongeza CUF kwa kushinda ile kata ya Tanga. Katika kata nane zilizokuwa zikifanya uchaguzi CCM tumeshinda kata nne. Tunawashukuru wananchi kule walikoendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kata hizo nne. TUNAWAAHIDI KUWATUMIKIENI KWA MOYO WOTE.
ng'wilage unyanda ng'wana nnauye alekeituja!
Kuna mtu mmoja alikuwa akishukuru kwa kuteuliwa akayatumia hayo maneno, "Nitakupeni utumishi uliotukuka" lakini baadaye ikaonekana kana kwamba hatoi utumishi uliotukuka akalazimishwa kujiuzulu. Nnape bwana kaazi kwelikweli!hapo kwenye red sijui kama ni mimi nimekosea kusoma au ilikuwa typing error!! (siamini kama ni frustration...lol)
Ahsante Kaka Nnape, tunashukuru kwa salamu zako. tafakarini, jipimeni, mchukue hatua........ Kila la heri
Shukran sana kwa maelezo yako yalokwenda shule.... japokuwa moja tu, hiyo Tathimini ya nini wakati unazijua sababu na ziko wazi..Labda nikwambie kubwa kuliko yote ni kushindwa kutekeleza yale mlo waahidi wananchi - Mmeshindwa kujivua magamba!Chama Cha Mapinduzi, kimeyapokea matokeo ya kura zilizopigwa na kutangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi kwa chaguzi ndogo zote, ule wa Arumeru Mashariki na zile za kata nane zilizofanyika jana nchini kwenye maeneo husika.