Hongera CHADEMA, Tumekubali mmeshinda! Timizeni AHADI zenu!

To accept defet is the best way forward...

Nape time to look back and move from that part it is dying and you will be on that history...

Shame Mkapa was busy to support Lowassa and his people... Just remember one day they will pay for all this mess they cause in this country..

NB>>> Nape make sure you hand a clean otherwise you will face the music like the co...
 
Nape bana...sema sababu za kushindwa kwenu.Mimi ninazo chache;
  1. Kumsimamisha mgombea asiye na mvuto,mgombea wa CCM ni bomu,ana aibu,ajui kuongea anakuwa anafanya kampeni kama anapiga stori.Alifunikwa na wapambe wake,yani ni sawa na bwana harusi afunikwe na mpambe wake.
  2. Matusi ya huyu kilaza Lusinde,jamaa ni wa ajabu sana,na maneno ya kejeli toka wa Mkapa,Mwigulu,Wassira,Nagu,Ole Medee,Ole Sendela nk
  3. Uwepo wa Lowasa ni sumu kwa watanzania kwasasa..yani Lowasa akionekana kwa watanzania ni sawa na sumaku yenye hasi kuelekezwa kwenye chanya...
  4. Kudhani kuwa watanzania wanashida na pesa..nikwambie kuwa watanzania ni maskini jeuri kwasasa,umaskini umetukaa na umekuwa ni sehemu yetu..hatudanganywi kwa pesa..tutakula pesa yako kura tutapeleka kwa anaweza kutusaidia.
  5. Mtindo wa CCM kutumia rasilimali za umma kufanya kampeni..hii ni hatari na uhaini na ni chukizo kwa watanzania kwasasa..watu wanaendelea kuelewa na kufahamu kinachotakiwa kufanya na kisichotakiwa kufanywa na viongozi.
Haya ni machache..mengi yapo!!!
 
CCM tutatumia matokeo haya kufanya tathimini ya kina na kuangalia wapi tuliteleza ili tufanye marekebisho kuhakikisha makosa hayarudiwi tena. Kimsingi uchaguzi huu umeisha na tufunge mjadala wa uchaguzi tujikite katika kuwaletea maendeleo wale waliotuchagua.

Nawatakieni kila lakheri wote mliochaguliwa, nawatakieni utumishi uliotukakuka!

Mkuu Heshima Mbele,
Hiyo kauli hapo kwa kweli inasikitisha, Hivi watu wanapoamua kuchagua Mtu wanayemtaka kwenu ni Makosa? Kwanini kwenue yawe makosa??Mkuu hamjateleza mhali popote ARUMERU Wamechagua Mbunge wanayemtaka, Basi sasa makosa yenu nini Hapo!!!
 
well Nape, washauri na wenzio watoe pongezi kina Wasira, Lusinde et al ( wazee wa mipasho na matusi)
 
Tunatoa wito kwa vyama vilivyoshinda kwenye maeneo hayo kuhakikisha vinatumia muda na dhamana waliyopewa kutekeleza yale waliyowaahidi wapiga kura wao.

Sikujua kuwa ccm nao wanajua maana ya msamiati "kutekeleza ahadi".
 
Nape kweli kafurahi kushindwa kwa Lowassa,Lakini na yeye alikwenda kufunga Kampeni so ni part and pacel ya kushindwa.

Nimekusikia Taarifa yako kwenye Tv na Redio yenu CCM TBC-1 & TBC Taifa, Lakini ujue Imeshindwa CCM na Sioi Kashinda maana Karetain Kura za Mzee wake (Hayati),So lile ongezeko mmeshindwa ku-Captcher kwa kukosa mbinu matokeo yake Nassari kajiongezea kutoka 19,000-2010 mpaka hizo 32,000 uchaguzi huu.

So Kamati Kuu yenu Mmefulia Kijana.Halafu kama kawaida yenu.

Mmeshindwa mkatoka Nduki mkamuacha Dogo Sioi peke yake hii ni aibu kwenu kamati kuu,ikiongozwa na jamaa yako Mwigulu
 
Hizi salam za pongezi siwezi kuziamini hadi nipate uthibitisho kwamba aliyezitoa ni Nape Moses Nnauye.

Bado tunayo kumbukumbu ya uchaguzi wa Igunga, alipost matokeo hapa, kadri walivyokuwa wamechakachua na kabla hayajatangazwa na mkurugenzi kwa mujibu wa sheria.

Alipobanwa athibitishe alikoyapata matokeo akakimbilia kwenye vyombo vingine vya habari kukanusha kwamba siye na hana user ID hapa JF. Kama anataka taarifa zake tuanze kuziamini, ni lazima afanye kama walivyofanya Zitto na Mwigulu(kwa kutaja wachache) wame verify user ID zao.

Short of that, tutaendelea kuchukulia taarifa zinazotolewa kupitia hii ID kama si za Nape Nnauye, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ccm.

Mkuu ndio haswa Nape Nnauye umjuae. Na kayasema haya kwa hakika. Uzuri ni maandishi so yatasimama daima. HOJA HAPA NI JUU YA AINA YA UWAKILISHI SI UNAJUA HUYU NI KATIBU MUENEZI? Je kasema haya kama Nape as Nape or Nape as Party Secretary? Na jee hii ndio taarifa rasmi ya chama? NAPE NNAUYE HEBU TUFAFANULIE JUU YA UTATA HUU.
 
Kwa picha hiyo ya kuona uchaguzi hu katika neno lenye rangi nyekundu kambi hiz mbili Wagalu na wagika sasa zitawafaha CDM na CCM.

Hakika tunakwokwenda kwa sasa CCM ningewashauri sana KUIGA MFANO WA NGOMA MBILI MAALUFU SANA KWENYE MIKOA YA KANDA YA ZIWA [Mwanza,Shinyanga na Tabora] maalufu kwa jina la BAGIKA NA BAGALU.

Kwa watu wa makabila ya wasukuma, wanyamweiz na wasumbwa wanazijua NGOMA hizo ambazo zina asili moja nzuri sana inayoleta msisimko kwa wapenzi na washriki wake kwa uchezaji wake,mbinu na mikakati yote yenye kila dalili za kuleta ushindani kati ya ngoma hizo mbili yani BAGIKA NA BAGALU.

ng'wilage unyanda ng'wana nnauye alekeituja!
 
wasiwasi wangu nikuwa hii kauli umeitoa kwa shingo upande maana sikuwaona wakati wakutolewa matokeo mlimwacha jamaa kama mtoto mkiwa alikuwa hana wakuongea naye alisimama huku kapigwa na butwaaa kaeni naye katika wakati huu mgumu maana kaondokewa na baba na jimbo wamemnyanganya inauma sana
 
Tatizo la ccm, mfanye demokrasia ya ukweli ktk kuwapata wagombea na hasa ya urais, msiruhusu nec kukata watu wakati kura ya maoini ya wananchi halisi imetumika.

Tatizo la ccm, muache kurithishana uongozi kutoka baba hadi mjukuu ama mtoto , hili ni chukizo kuu. Watoto/wajukuu wapate nafasi kwa kura kutoka kwa wananchi na sio NEC ama kuteuana.

Vinginevyo mie naona kifo chenu kiko paleeee.
 
Tumekusikia Mwenezi! Unapongeza kisha kutoa maelekezo kwa washindi watimize ahadi zao huku kauli za makada waliowakataza WanaArumeru Mashariki kutomchagua Mbunge wao Nassari eti kwa vile jimbo hilo "litakuwa likizo".

Tunawataka mavuvuzela hao warudi jukwaani na kuwaeleza Watanzania ikiwa ule ulikuwa ni "utani" au walikuwa serious maana wengine tunashindwa kujua ni lini mnatania na lini mnamaanisha mnachokisema. Halafu jambo muhimu ninalokusihini ninyi mtokao Chama Cha Magamba (Si Si Em) ni bora muanze kuwa waungwana kwa Watanzania wenzenu wakati huu mnapoanza kuporomoka kisiasa kabla hamjakabidhiwa rasmi benchi lenye la upinzani pale mjengoni.

Kwa trend mliyo nayo mtajajikuta ninyi ni maadui wa Watanzania wote. Mtaficha wapi nyuso zenu!!!!!!!!!
 
Chama Cha Mapinduzi, kimeyapokea matokeo ya kura zilizopigwa na kutangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi kwa chaguzi ndogo zote, ule wa Arumeru Mashariki na zile za kata nane zilizofanyika jana nchini kwenye maeneo husika.

Kwa heshima nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati watani zetu, CHADEMA kwa ushindi walioupata Arumeru Mashariki na kwenye kata tatu(Kirumba, Kiwira na Lizabon). Lakini pia nawapongeza CUF kwa kushinda ile kata ya Tanga. Katika kata nane zilizokuwa zikifanya uchaguzi CCM tumeshinda kata nne. Tunawashukuru wananchi kule walikoendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kata hizo nne. TUNAWAAHIDI KUWATUMIKIENI KWA MOYO WOTE.

Matokeo ya kura hizi kwa ujumla yameonyesha sauti ya wapiga kura kwenye maeneo husika, ndo maana tunaheshimu maamuzi yao.
Tunatoa wito kwa vyama vilivyoshinda kwenye maeneo hayo kuhakikisha vinatumia muda na dhamana waliyopewa kutekeleza yale waliyowaahidi wapiga kura wao.

CCM tutatumia matokeo haya kufanya tathimini ya kina na kuangalia wapi tuliteleza ili tufanye marekebisho kuhakikisha makosa hayarudiwi tena. Kimsingi uchaguzi huu umeisha na tufunge mjadala wa uchaguzi tujikite katika kuwaletea maendeleo wale waliotuchagua.

Nawatakieni kila lakheri wote mliochaguliwa, nawatakieni utumishi uliotukakuka!

Mheshimiwa Nnauye nimefurahishwa na ujumbe wako kwa wana CHADEMA ambao kimsingi unaihusu CCM kwa kuwa sisi wapiga kura tutawadai vyama vyote viwili mueleze kwa kina mmefanya nini kutekeleza ahadi kedekede mlizozitoa mwishoni mwa mwaka juzi wakati mnatafuta nafasi mbalimbali za uongozi wa kisiasa na kiserikali. Kipimo cha Nassari kitazingatia muda mfupi uliobaki atakaotumikia jimbo lake lakini kwa wengine kuanzia rais mpaka wabunge tutahitaji maelezo ya kina ni kwa kiasi gani wametekeleza ahadi lukuki walizotoa wakati wa kampeni zile. Ni vyema ukawakumbusha viongozi wa chama chako pia kwani tunajua wao ndio wameshika fuko la fedha na rungu la dola.
 
democracy at work!
CCM mnanishangaza sana na zile sera zenu za "Msipomchagua mgombea wetu, msitegemee kabisa huyo wa upinzani kupata ushirikiano kutoka Serikalini".
Hii ni kauli ya kitumwa,kibabe na kidikteta na wala sio demokrasia hata kidogo,tena inakiuka misingi ya uwepo wa vyama vingi!
Mkichagua CCM huduma zitakuja haraka; mkichagua mpinzania tutacheleweshachelewesha!!
 
With pleasure.

Angalau wapo wanachama wa CCM wanaojua siasa si hoja ya nguvu bali nguvu ya hoja. Na CCM inaweza kuwashawishi wananchi endapo tu itaacha kukumbatia walanguzi, wahujumu uchumi, wala rushwa, wabadhirifu, wezi wa mali ya umma, majambazi, mapusha n.k.

Hatuikatai CCM kwa rangi za bendera yake, ama kwa ubovu wa sera zake, bali tunaikataa CCM kwa ubovu wa viongozi wake. To be frank the major threat for the fall of CCM is not CDM, it is her chairman (Mr. President). Is the only one who is above the law, and he may use all machinery he has to make things done better, but is always afraid of himself.

Hakuna wa kuwahujumu, mnajihujumu wenyewe na kama mtashindwa kufanya uamuzi mgumu wa kufanya mabadiliko makubwa ndani ya chama chenu, not just kuvuana magamba even to change the party chairman, the truth is mtakuwa mmetengeneza njia ya kutokea 2015, na kupotea kabisa kwenye ramani ya siasa. Ni uamuzi mgumu sana kwenu kwani mmezoea kufanya mambo kwa mazoea, lakini ni uamuzi muhimu sana, ni lazima mumpate mwenyekiti imara atakayesaidia chama kusimamia serikali itekeleze ilani yenu ya uchaguzi. Otherwise, CHADEMA has very strong leaders who have deliver, na kila mmoja anaona matunda ya ushawishin wao.

Good Lucky Nape and your part.
 
hujafurahi CHADEMA kushinda
umefurahi LOWASSA kushindwa......

i know you are happy leo.....
A photo can speak thousands language!!.....
[h=6]Nape Nnauye
[/h][h=6]Hongereni watani (Chadema) kwa ushindi Arumeru Mashariki. Ninawapongeza mmeshinda! Ndio kauli ya wana Arumeru Mashariki nasi tunaiheshimu! Fanyeni kazi kutimiza mliyowaahidi wapiga kura. Kila lakheri!![/h]
 
Back
Top Bottom