Hongera CHADEMA, Tumekubali mmeshinda! Timizeni AHADI zenu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera CHADEMA, Tumekubali mmeshinda! Timizeni AHADI zenu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Honey K, Apr 2, 2012.

 1. H

  Honey K JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Chama Cha Mapinduzi, kimeyapokea matokeo ya kura zilizopigwa na kutangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi kwa chaguzi ndogo zote, ule wa Arumeru Mashariki na zile za kata nane zilizofanyika jana nchini kwenye maeneo husika.

  Kwa heshima nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati watani zetu, CHADEMA kwa ushindi walioupata Arumeru Mashariki na kwenye kata tatu(Kirumba, Kiwira na Lizabon). Lakini pia nawapongeza CUF kwa kushinda ile kata ya Tanga. Katika kata nane zilizokuwa zikifanya uchaguzi CCM tumeshinda kata nne. Tunawashukuru wananchi kule walikoendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kata hizo nne. TUNAWAAHIDI KUWATUMIKIENI KWA MOYO WOTE.

  Matokeo ya kura hizi kwa ujumla yameonyesha sauti ya wapiga kura kwenye maeneo husika, ndo maana tunaheshimu maamuzi yao. Tunatoa wito kwa vyama vilivyoshinda kwenye maeneo hayo kuhakikisha vinatumia muda na dhamana waliyopewa kutekeleza yale waliyowaahidi wapiga kura wao.

  CCM tutatumia matokeo haya kufanya tathimini ya kina na kuangalia wapi tuliteleza ili tufanye marekebisho kuhakikisha makosa hayarudiwi tena. Kimsingi uchaguzi huu umeisha na tufunge mjadala wa uchaguzi tujikite katika kuwaletea maendeleo wale waliotuchagua.

  Nawatakieni kila lakheri wote mliochaguliwa, nawatakieni utumishi uliotukakuka!
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  That's great Nape,
  Hongera kwa kukubali kushindwa, hiyo ndiyo siasa.
  Japo kulikuwa na mbinu ya kutaka kuchakachua matokeo ya Arumeru, makamanda wa chadema walikuwa makini sana.

  Thanks anyway, hiyo ndiyo gharama ya democrasia


  [​IMG]
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,466
  Trophy Points: 280
  hujafurahi CHADEMA kushinda
  umefurahi LOWASSA kushindwa......

  i know you are happy leo.....
   
 4. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,971
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  RIP CCM. Kama kwenye chaguzi ndogo ulikuwa unashinda 80 - 90% na sasa unaanza kuambulia 40% basi ujue kifo kimekukaribia. Hakika ccm itakufa, maana hamna njia ya kijitibu na kujiponyesha ugonjwa wenu.
   
 5. G

  Gurti JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chadema itachukua nchi 2015 hili halimhitaji shehe yahaya kutabiri.
   
 6. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Ngoja basi tujidai hata kwa siku moja si unajua watu kibao wamepigana kufa kupona hata hivyo Dogo Janja Mh MB Nasari kashaanza kazi....
   
 7. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu Nape hongera kwa taarifa nzuri yenye mantiki. Katika siku zote za utendaji kazi wako kama Katibu muenezi leo (ktk hii post) umeonyesha ukomavu, nimeipenda. JIANDAENI 2015 ITAKUWA NI TSUNAMI, VIJANA TUMEJIPANGA POA!
   
 8. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwani wewe ni NANI?

  Kwanini unatumia Nnauye? Je wewe ndo katibu mwenezi wa ccm? ukikubali ndo nitaendelea kuchangia
   
 9. Lucas

  Lucas JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 2,452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hapo kwenye red sijui kama ni mimi nimekosea kusoma au ilikuwa typing error!! (siamini kama ni frustration...lol)

  Ahsante Kaka Nnape, tunashukuru kwa salamu zako. tafakarini, jipimeni, mchukue hatua........ Kila la heri
   
 10. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  sawa ninyi zenu mlizoahidi mlitekeleza?
   
 11. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Ni Kata gani nyingine ambazo CCM walishinda? Mimi ninafahamu kata 2 za Vijibweni (DSM) na Chang'ombe (Dodoma) Je Nape unaweza kunifahamisha hizo kata nyingine 2 ziko wapi?
   
 12. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hongera kwa kuukubali ushindi la kujiuliza kwa nini chama kinazidi kuporomoka????????????????
   
 13. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,334
  Likes Received: 2,657
  Trophy Points: 280
  democracy at work!
  CCM mnanishangaza sana na zile sera zenu za "Msipomchagua mgombea wetu, msitegemee kabisa huyo wa upinzani kupata ushirikiano kutoka Serikalini".
  Hii ni kauli ya kitumwa,kibabe na kidikteta na wala sio demokrasia hata kidogo,tena inakiuka misingi ya uwepo wa vyama vingi!
   
 14. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kimbe ccm ni watani wa ccm! Hakuna kitu hiyo Na
   
 15. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nyie Magamba muda wenu wa kuwadanganya Watz umekwisha, mwenye macho ya akilini ahitaji darubini kuliona hili.
   
 16. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #16
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Usitoe pongezi huku moyo unauma
   
 17. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #17
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Unawaambia wenzako watimize Ahadi, zile boss wako alizoahidi katimiza ngapi?
   
 18. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi hizi trick zenu toka 1995 za kuingiza kura bandia mtaziacha lini? Yani Nape amini njia hizi za kulazimisha ushindi zinawaabisha sana. Nakusiin badilikeni mbona mtaheshimaka tu.
   
 19. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #19
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  hapa umepost kama msemaji wa CCM kuiwakilisha CCM au kama NApe??? maana isije kesho ikaja kesi, kesi na kesi... coz CCM is good at wasting people's time mahakamani wakati watu wanataka uwakilishi bungeni
   
 20. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kumbe ccm ni watani wa ccm! Hakuna kitu hiyo Nape! watu wako kwenye ukombozi Wa kweli. Weka utani pembeni.
   
Loading...