A
Anonymous
Guest
Mheshimiwa Anthony Mavunde,
Nitumie nafasi hii kukupa salamu na pongezi kwa jitihada zako kubwa katika kuimarisha maisha ya vijana wa Dodoma kupitia nafasi yako ya uongozi.
Mimi ni kijana mkazi wa Dodoma, mjasiriamali, na mshiriki wa mashindano ya Mavunde Cup. Hata hivyo, kuna jambo ambalo limeniacha na maswali mengi sana.
Wakati mechi ya Mavunde Cup ikiendelea 31st July 2025— tukifurahia tunu ya michezo uliyoanzisha kwa ajili yetu — vijana kadhaa walikamatwa ovyo na kuwekwa mahabusu bila kosa la msingi. Mimi mwenyewe nilinusurika kwa bahati tu.
Mheshimiwa, hali kama hii inazima matumaini ya vijana. Inajenga hofu na kuharibu maana ya jitihada zako nzuri. Wapo wenye familia, bajaji na bodaboda za kupeleka hesabu. Sisi ndio wapiga kura wako, na pia ndio kizazi unachokijenga.
Kwa heshima kubwa, naomba ulitizame Mheshimiwa. Ninaamini kuwa sauti yangu ni sauti ya wengi waliokosa nafasi ya kuzungumza.Nahitaji kushiriki nawe maono ya kujenga mfumo wa haki, usalama, na matumaini kwa vijana wa Dodoma.
Naamini kwa pamoja tunaweza kusukuma mbele gurudumu la mabadiliko.
Ahsante kwa muda wako na kwa moyo wa utumishi.
#SautiYaVijana #DodomaYetu #MavundeCup