figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,720
- 55,843

Homa ya Lassa yatua Benin, yaua wawili.
Ugonjwa wa homa ya Lassa bado imeendelea kuwa tishio na kuzitesa nchi za afrika Magharibi hususan Nigeria.
Taarifa ni kwamba tayari ugonjwa huo unaoenezwa na Panya, umeingia nchini Benin baada ya kutesa watu kadhaa kwenye mpaka na Nigeria huko Edo State.
Afisa wa afya jimboni humo Heregie Aihanuwa, amesema tayari wamepata taarifa za wagonjwa wa 5 kuripotiwa nchini Benin pamoja na maiti mbili.
Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Nigeria kutokana na ugonjwa wa homa ya Virusi vya Lassa, imeongezeka mpaka 35 kutoka watu 2.
Mikoa iliyoathirika na kutoa wagonjwa wengi zaidi ni pamoja na Ibadan Oyo, Taraba, Kano, Edo na Niger.