Holy Week | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Holy Week

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Nyerere, Mar 29, 2010.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Mar 29, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Holy Week,Monday

  Saa tatu asubuhi,Yesu alifika kwenye Hekalu,yeye na wafuasi wake,na akaanza kuhubiri.
  Kulikuwa na fujo sana. Kulikuwa na wanyama wengi wanatolewa sadaka Hekaluni,hii ilikuwa inaleta makelele;pia kulikuwa na wabadilishaji fedha. Katika Hekalu kulikuwa na sheria kwamba kila mtu lazima atoe nusu shekeli[half a shekel]na hii shekel ilikuwa ni ya Wayahudi,walikuwa hawatumii hela za Kirumi Hekaluni. Kwa hiyo kila mtu ilibidi abadili hela pale,watu walipokuwa wanafika kutoka Mataifa yote;pamoja na kubadili fedha,walikuwa pia wanafanya kazi za kawaida za Benki.
  Katika mazingira ya namna hii,watu walikuwa wanadhulumiwa sana fedha,na watu wengi hawakupendezwa na biashara hii iliyokuwa inafanywa na Mafarisayo.
  Kijana mmoja alikuwa anaswaga ng'ombe,halafu Yesu akamwona kijana mmoja anakejeliwa na kudhulumiwa.Hapo 'uzalendo ukamshinda Yesu'.
  Kwa hiyo akatoka pale alipokuwa anahubiri,akauchukua ule mjeledi kutoka kwa yule kijana,akawaswaga ng'ombe wote akawatoa Hekaluni,pia akaenda kufungua milango,na kuwandoa ng'ombe wote waliokuwa wamewekwa Hekaluni,halafu umati uliokuwepo pale ukazigeuza meza za wabadilisha fedha,hizi fujo zote zilikwisha kabla askari wa kutuliza ghasia [warumi] kufika. Halafu wakaweka walinzi wa kiraia kulinda mtu yoyte asifanye biashara wakati Yesu anahubiri. Askari walipofika wakakuta shwari,Yesu anahubiri.
  Yesu akasema,''Leo mmemshuhudia maeno yaliyoandikwa katika Msahafu kwamba,'Nyumba yangu itakuwa Nyumba ya sala kwa Mataifa yote,lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wezi'' Alishindwa kuendelea,kwa sababu watu wote wakalipuka kwa kushangilia, na kuanza kuimba pambio,na kushukuru kwamba wale mafisadi wameondolewa Hekaluni.
  Kitendo hiki kilionyesha kwamba Yesu hakuafiki mtu yoyote asipotumia nguvu kuizuia majority isionewe na kikundi kidogo cha mafisadi,kinachotumia nguvu na ulaghai na oganaizesheni, kufanya udhalimu.
  Halafu wakafika Mafarisayo kumuuliza Yesu anahubiri kwa ruhusu ya nani,by what authority;kwa sababu Yesu alikuwa hajawahi kupata ordination na kupewa title ya ''Rabbi'' Yesu akawauliza swali,Je,Yohana Mbatizaji,alikuwa anahubiri kwa mamlaka ya nani,kama yalitoka kwa Mungu,mbona hamkumwamini?
  Yesu akawaambia Mafarisayo,''baba mmoja aliwaambia wanae waende shambani kufanya kazi;mmoja akasema,hataki kwenda,lakini baadaye,akaenda;mwingine akasema atakwenda,lakini hakuenda. Yupi kati yao alifanya alivyoagizwa na Baba yake? Kwa hiyo makahaba,na wauza baa,wamelipokea neno la Mungu,baada ya kulikataa kwanza,lakini ninyi mmelikataa.
  Baada ya hapo,Mafarisayo walivyoona Yesu amewasema vibaya,wakaondoka kwenda kupanga njama dhidi yake.
  Yesu akawaambia makutano.
  Mtu mmoja alilima shamba akalikodosha,baaadaye akarudi kudai hela zake. Wale watu waliotumwa kudai hela,waliuawa wote. Mwenye shamba atawafanya nini wale wapangaji? Watu wote wakasema,''Atawatimua na kuweka wengine'' Yesu akasema,'Jiwe alilolikataa mwashi ndilo limekuwa jiwe la msingi. Hawa watu wakiikataa Injili hii,itapelekwa kwa wengine.
  Jiwe la msingi limewekwa kuwa kikwazo kwa wengi. Kuna fumbo katika hili jiwe. Hili jiwe likimwangukia mtu yoyote litampondaponda,lakini,ingawa huyo mtu atapondwapondwa,roho yake itaokoka.
  Yesu akasema,''Mtu mmoja aliwaalika watu katika arusi. Waloalikwa katika arusi hawakutaka kufika,wakaenda katika shughuli zao;mmoja kwenye shamba lake,mwingine kufanya ufinyanzi,mwingine kufanya biashara zake.
  Akawatuma watu wengine kutoa mwaliko. Watu waliotumwa kualika,wakatendewa vibaya,wengine hata kuuawa. Mwishowe akatoa amri wale wote waliokataa mwaliko wauawe.
  Halafu akasema,'Waliolikwa hawakustahili,nendeni mkamwalike yoyote mtakayemwona huko . Wakaalikwa watu wengi.
  Mwenyeji wao,alipokuwa anatazama akashangaa kuona mtu mmoja ameingia bila vazi la arusi
  Akamuuliza 'Vipi wewe umeingia bila vazi la arusi,kwa sababu mimi niliagiza mavazi ya arusi yatolewe bure kwa yoyote atakayefika' Akatoa amri,'Mtoeni nje huyu mtu.
  Wanaokaribishwa humu ndani ni wale tu wanaokubali mwaliko,na wale wanaoniheshimu kwa kuvaa vizuri .''
  Watu wakamuuliza,'Tutajiyayarisha vipi kwa hii arusi.Unaweza kutoa ishara gani kwamba wewe ni mtoto wa Mungu?
  Yesu akasema ''Bomoa hili Hekalu,na nitalijenga baada ya siku tatu.''
  Lakini hawakuelewa kwamba 'Hekalu' alilokua anazungumzia ni mwili wake.
  Saa kumi jioni wakarudi Bethany. Akawambia Andrew,Philip na Thomas,kwamba wajenge kambi nyingine karibu zaidi na Jerusalem,ili wakae hapo mpka mwisho wa wiki. Kwa hiyo kambi nynigine ikajengwa kwenye bonde,karibu na Bustani ya Gethsemanebado ilkuwa katika eneo la Simon.
  Kuhusu mambo yaliyotokea Jumanne,tutajadili kesho,Jumanne.
   
Loading...