Hoja yangu: Tunakoelekea ni Kubaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja yangu: Tunakoelekea ni Kubaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hemed Maronda, Jun 2, 2012.

 1. H

  Hemed Maronda Senior Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watanzania sasa tuache tofauti zetu za vyama,dini na sehemu tunakotoka ili tujadili mustakbali wa Nchi yetu.Nimelazimika kuleta uzi huu ili kila mwenye mapenzi mema na Nchi hii aujadili kwa mapana na marefu.Hivi sasa kuna mjadala mkubwa wa uandikaji upya wa Katiba ya Nchi yetu lakini nionavyo mimi mchakato huu hautafanikiwa kama matarajio ya wengi.Nimeona kuna vikwazo vingi vimewekwa kwa sisi ambao tunatakiwa tujadili Katiba tunayoitaka,kwa mfano Wanainchi hatuna ruksa ya kuujadili Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,na tumeona siku za hivi karibuni Zanzibar kumetokea vurugu ambazo chanzo chake inawezekana kuwa ni kero za Muungano ambazo sisi wanainchi tumezuiwa kuzijadili,swali hivi tumezuiwa kuujadili Muungano hasa kwa maslahi ya nani? Wakristo na Waislamu,Waunguja na Wabara Visiwani Unguja na Pemba wanaishi kwa mashaka makubwa hivi viongozi wako wapi mpaka wanaiacha hali kuwa mbaya kiasi hicho? Tukiachana na jambo hili la mjadala wa Katiba Mpya na kero za Muungano nije kwenye suala la Vitambulisho vya Taifa,nimeona mchakato huu nao pia utatufikisha pabaya kwa mambo mawili,jambo la kwanza kuwa hatuna maandalizi ya kutosha ya kuwatambua watu ambao si raia halali wa Tanzania jambo ambalo ni hatari kubwa sana ikiwa asiye kuwa raia akafanikiwa kupata Kitambulisho cha Taifa,jambo la pili ni bajeti husika ya mradi wa Vitambulisho hivyo,bajeti yake ni kubwa mno na kuna uwezekano kuwa huu nao ni mradi wa kutaka kuzitafuna fedha zetu,swali hivi kuna umuhimu gani uliooneka ghafla wa kutupatia Vitambulisho vya Taifa ikiwa miaka 50 tumeishi bila vitambulisho? Swali lingine,kuna haja gani ya kutumia zaidi ya Tshs 250 Bilioni wakati Hospitali zetu hazina Madawa,vitendea kazi vya kisasa na wataalamu wa kutosha? Nije sasa kwenye suala la Utawala bora,hivi juzijuzi Raisi JK amevunja Baraza lake la Mawaziri na kuteua jipya,alifanya hivyo baada ya kupata shinikizo kutoka kwa Wabunge na hasahasa wa kambi ya upinzani na tunawashukuru kwa uzalendo wao, baraza jipya limepatikana wapo Mawaziri walioachwa kutokana na utendaji wao mbaya na jambo hilo limethibitishwa na CAG kuwa kuna fedha zimetafunwa kwenye Wizara hizo,swali hivi Raisi anachelea nini kuwachukulia hatua za kisheria wale wote walioshiriki kula fedha zetu za umma? Yapo mambo mengi yanayotupeleka kombo kama Watanzania na tuna nafasi ya kuyajadili bila ya kuwa na jazba za ushabiki wa Chama chochote cha kisiasa, ninapendekeza hivyo kwa sababu hatakama Chadema kwa mfano watashika Dola mwaka 2015 Bado wanaweza kukutana na tatizo na kero za Muungano hivyo tujadili matatizo haya kwa mapana na marefu. wakuu nawasilisha.
   
 2. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,891
  Likes Received: 1,649
  Trophy Points: 280
  Havmuitaji Rais mwenye kubeba watu na kwa mawazo yangu J. K. Niwamwisho
   
Loading...