HOJA YA MSUKUMA YAPATA SUPPORT KUTOKA KWA WASOMI.

HOJA YA MSUKUMA YAPATA SUPPORT KUTOKA KWA WASOMI.

M2pc

Member
Joined
Jun 14, 2016
Posts
89
Reaction score
59
Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.[emoji24][emoji24] Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa. [emoji851][emoji851]

Wasomi wengi wana maisha ya kawaida [yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi na magari mawili ya kutembelea [tena kwa mikopo!].

Na tena wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini [kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga]. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana.

Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga. Hii inachangiwa na mambo mawili.

Mosi; [wameelezwa na kuaminishwa kwamba] yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli.

Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio. Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee [kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika].

Pili; madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

Katika maisha ya kawaida(hasa ya kusaka fedha), unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha. Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

Simaanishi kusoma hakuna maana [hata mimi nimesoma nina kadigrii kangu, na vicertificate vya kozi mbalimbali] isipokuwa ninakwambia hivi: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani.

Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri na mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti. Ukitaka kutajirika usiulete "u-smart" wa darasani huku mtaani. Jumapili njema[emoji1593]
 
Mh. Msukuma ni miongoni mwa watu ambao ninawakubali kwa ujasiri wa kuweza kusema kweli.
Suala la ajira ya watumishi wa darasa la saba ni miongoni mwa mambo ambayo ameweza kuyapambanua vizuri.
 
Na hili kwakweli anahitaji pongezi,maana amefikisha ujumbe mbashara sema wahusika watambeza japo ujumbe umewafikia.
 
Back
Top Bottom