mechard Rwizile
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 1,571
- 875
Mimenusa hisia na joto la wengi kuhusu hoja ya kumkaribisha Lowasa CHADEMA - Madhara yake ni makubwa kuliko viongozi wanavyodhania. Huu ndio ukweli wenyewe:
Hata kama Lowasa angepitishwa kuwa mgombea wa CCM, bado UKAWA wangefanya vizuri maana wananchi wanakiu ya mabadiliko.
Kitendo cha Kumpitisha Magufuli kimefanya kazi ya kuichachafya CCM kuwa nyepesi zaidi maana wafuasi wa Lowasa wengine bado ungekuwa mtaji wa UKAWA hata bila kumuingiza Lowasa katika kundi la UKAWA.
Kumkaribisha Lowasa na kundi lake ni Ku-bland UKAWA, haitauwa UKAWA tena maana wanaokuja na Lowasa ni waliopitisha KATIBA mbovu, vita yetu tutakuwa tumeipoteza kwa kujisalimisha kwa adui kia aina.
Lowasa na Kundi lake ni kama mbwa mwitu. watakao baki salama ni CCM maana wao magamba yatakuwa yamevuka, yamevaliwa na CHADEMA. Chadema yenye Rostam Azizi, Karamagi, Kingunge, Lowasa, n.k siioni kama CHADEMA ya kuleta nafuu kwa walalahoi. itakuwa ni Muungano wa CCM na CHADEMA, hapo itikadi na harakati zinatakiwa zibadilike, wananchi hatukuunga nkono CHADEMA mfanye hayo.
Hii agenda ya kumpokea Lowasa mmeitoa wapi? Mbona Wabunge wa upinzani wachache waliokuwa bungeni ndio wameshawishi watu wengi kuiunga mkono kwa sababu ya hoja zao? kwani nilini Lowasa alisimama bungeni akatoa hoja ya kueleweka? Lowasa anamtazamo gani kuhusu katiba Mpya?, kuhusu ufisadi?, kuhusu muundo wa muungano? atanadi vipi ilani ya uchaguzi asiyoiamini? au kunanini hasa la ziada?
Lowasa na kundi lake wakiingia CHADEMA, wengi tutatoka CHADEMA na iko siku viongozi wote mtajikuta mnatakiwa kutoka nje ya CHAMA kwa njia ya nguvu ya vikao na katiba ya chama halafu wanabaki wao. Huu utaratibu wa mtandao hawatauacha utawatafuna nyie mnao wakaribisha watu hawa. Itakuwa kama MREMA na TLP na Ngawaiya.
Nguvu ya CHADEMA kwa sasa ni kubwa, achana na agenda ya LOWASA kuja CHADEMA, tuletee ngombea wetu asiye sehemu ya watu wa LOWASA, sisi tumeisha jiandikisha, na tunasubiri masanduku ya kupiga kura. CHADEMA bila LOWASA inawezekana. MBOWE, anayekushauri ati utapata mtaji wa watu anakuongopea. wao kama wamechukia si watupigie kura tu, unatosha. usichafue chama. Hoja yetu kwa muda mrefu ni kwamba CCM ni mafisadi, akina LOWASA, ROSTAM AZIZI, KALAMAGI, sasa wamekuwa wasafi lini? yaani kukatwa kwa LOAWASA kumewasugua na kuwasafisha??? acha mzaha, sisi tuko serious na ukombozi wa nchi hii. Bora kukosa URAIS tukawa na wabunge wengi kuliko kuwa na LOWASA kama mgombea URAIS kwa CHADEMA.
Siku moja mtakumbuka maneno yangu.
PAPA1, ni mara yangu ya kwanza kuona na kusoma mchango wako katika mtandao huu, sina maana huwa hauchangii nina maana sikuwahi kusoma ulichokiandika. Na kwa kuwa nimesoma ulichokiandika nimevutiwa sana na aina ya uchambuzi wako na uwasilishaji wako wa hoja hii. Hakuna chembe ya kashifa kwa watu na hasa Mzee wenu ( mimi ni kaka yangu) Mhe. Lowasa lakini umeonyesha kutohitajika kwake katika chama cha Democrasia na Maendeleo. Haitajiki kabisa. Aachwe akajipange upya, huko huko CCM.