Hoja kwa malumbano ya hoja - itv | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja kwa malumbano ya hoja - itv

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by babykailama, Apr 13, 2012.

 1. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  HOJA KWA MALUMBANO YA HOJA:


  [FONT=&amp]Dada Nyangasa hongera kwa jinsi mnavyoendesha kipindi sasa.[/FONT]

  [FONT=&amp]Hakuna haja ya kuwakaribisha baadhi ya watu kila wakati kwani sasa wamevimba vichwa na kujiita Mjumbe wa Kudumu wa Malumbano ya Hoja na Mzalendo # 1.

  [/FONT]

  [FONT=&amp]Aidha haiwezekani mtu awaye yeyote awe kama Mungu mwenye uwezo wote wa kujua kila jambo vyema au mada zote zilizoko hapa duniani, kumfanya awe anahudhuria na kutamba kuchangia kwa mbwembwe katika kila kipindi. Ukiwasikiliza kwa makini huwa wana kauli tata na nyingi hazina ukweli endapo utazichekecha katika kipima kweli (truth meter).[/FONT]

  [FONT=&amp]Kwa kipindi kichachokitakachozungumzia Kero za Muungano; naomba nafasi kwa kutoa mchango wangu (Baby Kailama) toka mtandaoni, maana sitaweza kufika kama ifuatavyo:

  [/FONT]

  [FONT=&amp]1. [/FONT][FONT=&amp]Miaka 48, ndiyo, Kero za upili za Muungano km. vile mifumo ya kodi, uwakilishi bungeni, bajeti n.k zimekuwa zinashughulikiwa katika ngazi mbalimbali km vile katika Wizara, Idara na hata kupitia Vyama vya Siasa.

  [/FONT]

  [FONT=&amp]2. [/FONT][FONT=&amp]Miaka 48, hapana, kero ya msingi ya Muungano bado haijashughulikiwa kabisa. Nayo ni kupata ridhaa ya wananchi wa pande zote (Bara & Visiwani) kama leo hii bado wanauhitaji Muungano au la na uwe wa aina gani (Serikali moja, mbili au tatu) kama unahitajika. Kwangu mimi kura huru na ya haki toka kwa Wananchi katika hili ndiyo ingekuwa ya kwanza hata kabla ya kutaka Katiba mpya. [/FONT][FONT=&amp]Maana ninachoona ni kuwa tunataka kufagia sakafu (Katiba ya Muungano) kabla ya kusafisha dari ( Muundo wa Muungano kama unakubalika).

  [/FONT]

  [FONT=&amp]Kuendelea kuogopa kujadili na hata kuacha Wananchi kuamua wanataka nini juu ya Muungano, ndiyo jinamizi linaloendelea kututafuna barabara. Watu wa upande mmoja wataendelea kulalamikia upande mwingine maana pengine sababu na Muundo wa Muungano ulioanzishwa na Waasisi wake tunaowaheshimu sana, leo hii zimepitwa na wakati au zinahitaji maboresho makubwa. Kero hii itaisha na tutaeshimiana wote sawia bila kumwona mwingine kuwa ama mnyonyaji (mburuzaji) au wa kulalama lalama kama Wananchi watapewa nafasi ya kupiga kura ya wazi katika karne hii juu ya huu Muungano.

  [/FONT]

  [FONT=&amp]Angalia tu mimi binafsi ninavyokereka kwa jambo la msingi la aina ya Muungano tulionao:

  [/FONT]

  [FONT=&amp]a. [/FONT][FONT=&amp]Nakereka kuona wenzetu wanaendelea kuenzi tunu za ‘utaifa’ wao kama Katiba, Alama za SMZ, Bendera na Wimbo wao wa Taifa? Mimi sina zangu ila nina zetu wote! Nakereka kuona Rais wa JMT akienda katika sherehe za kusimikwa Rais wa SMZ hawi wa mwisho kuingia uwanjani wala hawi wa kwanza kutoka uwanjani bali Rais wa SMZ anayepigiwa Mizinga na kukagua gwaride rasmi; Je Amiri jeshi wako wangapi?

  [/FONT]

  [FONT=&amp]b. [/FONT][FONT=&amp]Sipendi mtu mwingine kujadili bajeti yangu yote zikiwemo hata na Wizara zisizo za Muungano km. Afya n.k wakati ya kwao mimi sikaribishwi kuijadiri.

  [/FONT]

  [FONT=&amp]c. [/FONT][FONT=&amp]Sitaki mtu kunichagulia Rais (& Makamu) wangu wakati mimi simchagulii wake!

  [/FONT]

  [FONT=&amp]d. [/FONT][FONT=&amp]Sikubali kuendelea kubeba lawama kuwa mimi ninalazimisha Muungano kwa sababu za kujinufaisha kuliko mwenza wangu katika Muungano wa aina yeyote. [/FONT]
   
 2. i

  ikindo Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 25
  Well said kiongozi,huu muungano umekaa kifremason kwa sababu unawalakini mwingi na nigharama sana kuumeintain.
   
 3. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni matumaini yangu kuna mtoto atapiga kelele kuwa 'Mfalme yu uchi' ndipo na wengine waseme kuwa kweli !! Maana hili suala la Muungano ni la Msingi kabla ya mengine yote!!
   
Loading...