Hoja binafsi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja binafsi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bbukhu, Feb 28, 2012.

 1. b

  bbukhu Member

  #1
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wednesday, February 15, 2012

  UNAFIKI HUU WA WANASIASA WETU HADI LINI


  BY BARNABA BUKHU.

  Mwaka 2008, baada ya kuibuka kwa kashfa ya kampuni hewa ya richmond, watanzania tuliamini kuwa ukombozi wa kweli umepatikana kwani wabunge wengi walionesha uzalendo wa hali ya juu kwa kujadili kuhusu kashfa ya richmond na kuunda kamati teule kuchunguza kampuni ya richmond.

  Kamati teule baada ya uchunguzi, ilibaini kuwa kampuni ile ilikuwa hewa au ya mfukoni. Wabunge wengi wakatoa machozi yao kuonesha uchungu walionao kwa rasilimali ya wananchi wa tanzania.
  Mfano wabunge kama vile: Anne kilango, Samwel Sitta, Harrison mwakyembe, na wengine wengi walichukizwa sana na ufisadi uliofanywa kupitia kampuni ya richmond.

  Imani ya watanzania kuwa wabunge wao ni wazalendo, ilianza kufifia baada ya kugundua kuwa kashafa mbalimbali za ufisadi zilizokuwa zikiibuliwa ikiwamo hii ya richmond hazikushughulikuwa. Imani hiyo ilitoweka kabisa mwaka jana baada ya wabunge walewale wa ccm ambao mwaka 2008 walionesha uzalendo kwa kuchukia ufisadi, kupitisha muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 bila kujali matakwa ya watanzania.

  Tuliona kuwa wabunge wa chadema na nccr mageuzi walipotoka nnje ya ukumbi wa bunge ili kupinga muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba,wale wa ccm wakaanza kuupitisha kwa mbwembwe nyingi huku wakionesha madharau kwa wabunge wa upinzani.

  Hapo ndipo tulipobaini kuwa wabunge wetu ni wanafiki wakubwa kwani wanapuuza matakwa ya wapiga kura wao. Ajabu mwaka huu mwezi wa pili mheshimiwa rais pamoja na kusaini ule muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba mwaka jana akawasilisha mabadiliko ambayo wabunge wa chadema waliyataka. Wabunge wa ccm walichukia sana kitendo kile kwani mwaka jana wapinzani walipotoka nnje ya ukumbi wa bunge kupinga muswada huo, wao waliwacheka kwa hiyo ilikuwa aibu kubwa kwao.

  Haikutegemewa kabisa kuwa wabunge kama akina Kilango na wenzake waliokuwa wakitoa machozi bungeni kutokana na ufisadi uliofanywa kupitia kampuni ya richmond leo wangekuwa mstari wa mbele kutetea mambo ambayo hayana maslahi kwa umma. Hii inaonesha ni jinsi gani wanasiasa wana ndimi mbili. Yaani unafika uliokithiri. Unafiki huu hadi lini?
  Posted by barnaba bukhu at 6:10 AM 0 comments [​IMG] Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook

  OUR POLITICIANS AND THE LIP SERVICE

  It is now common to see that our politicians just provide the lip service for the people. During the general election they cheat their voters that they could make the life of the people better but when they get into power they go and live in Dar es salaam. They totally forget their voters. When another general election comes they come again to cheat their voters.

  In Tanzania for example in 2005, Mr. Jakaya Kikwete the fourth phase president cheated Tanzanians. He told them that he would make their life better. He warned his fellow leaders that he has a smiling face but he is serious. Mr. Kikwete also promised people that he would fight against corruption and eliminate it in his presidential phase.

  Now our president has shown his weakness that he is unable to fight against corruption. Corruption has now increased than before. The simple question that people can ask themselves is: Why Mr Kikwete failed to eradicate poverty? The reason behind is that the people who engage in corruption practices are his friends who helped him during general election of 2005 in campaign. So he afraid to create hatred with them.

  It is corruption that makes life of the people to be so hard. Most of the politicians are only considering their interest. They misuse the resources of the nation.

  It is now known that the treasure of country is empty because much money is used by politicians to pay themselves.Their salary and allowance is higher than salary of other workers. This shows the classes in Tanzania. The government is now bankrupt. Because the income of the nation is used for interest of some people in the society.
   
Loading...