Hoja Binafsi za Zitto na January:Je, Wabunge watalipa visasi


Kwa hilo nipo ukurasa mmoja na wewe. Kwa mtazamo wako, nini kifuate? Zitto asubiri hiyo kamati gani sijui imalize kazi yake kama alivyo adhidi Waziri wa Kilimo? Zitto ajipange tena na hoja yake binafsi? Au Zitto na Chadema kwa ujumla wajipange zaidi kwa kuliweka hili katika bajeti yao ya wizara kivuli ya kilimo hapo mwezi Juni?
 
Reactions: FJM

Mtamzamo wangu kuanguka kwa hizi hoja za hawa 'Boys II Men' ni salamu kutoka kwa wabunge wa ccm kwamba wasijione kama wao (Zitto na January) ni smarter kuliko wabunge wengine. Inawezekana wanahisi (hasa January) anakitumia chama chake cha ccm kujijenga yeye kisiasa baada ya chama kumfikisha hapo alipo. Whether kuna ukweli kwenye hili au la hayo ni mambo mengine lakini kwa sasa safari imeanza ya kufungana speed governor. CCM wanaweza kuwa na wakati mgumu kwa kutaa hizi hoja lakini wanaweza kuvuka kizingiti kama wakitoa sababu za msingi (kama wanazo).

Zitto naye amekuwa muumini mzuri wa hizi siasa za calculations. Huyu kijana is very smart lakini sina hakika kama approach aliyotumia siku hizi itamfikisha kwenye kiti cha enzi. Kwa kurudia maoni yangu niliyowahi toka huko nyuma naomba niseme, naridhika na Zitto wa Buzwagi era na ninasononeshwa na Zitto wa Blackberry.
 
hoja ya makamba ni contradicting, wote twajua gharama za ujenzi zilivyo juu, na watu wengi hukopa ili kujenga, leo hii utamwambia nin mtu huyu eti kodi ni ya miezi 2 tu maximum...

Hata wenye daladala nao huwa wanakopa ili kununua magari yao.lakini bado wanakuwa controled na sumatra.wewe unaonekana live kuwa ni mmoja kati ya akina BABA MWENYE NYUMBA
 
ccm haina wabunge, ina watu mbumbumbu, mazoba, wasifikiri, watu legelege, wasiofaa, hakika ccm ni kielelezo cha watu duni na mamluki kwa taifa lao.

Kimsingi una hoja lakini nadhani huo umbumbumbu, uzoba, ulegelege n.k, ni wa wabunge wa CCM kitaasisi, sio mbunge mmoja mmoja, kwani wapo wabunge kadhaa wa CCM ambao ni makini sana. Unajua kinachowabana wabunge wengi ni suala la kwenda kinyume na serikali na chama chao cha CCM ambapo adhabu yake ni jina kukatwa na vikao vya chama i.e. NEC, baada ya mchakato wa kura za maoni kugombea ubunge kupitia CCM huko majimboni. Ni hilo tu; vinginevyo wakiruhusu tu suala la mgombea binafsi, mambo mengi sana yatabadilika, kwani kuna wabunge ambao wapo tayari kuachana na CCM lakini hawapo tayari kujiunga na upinzani kama vile Chadema kutokana na historia baina ya vyama hivi viwili humo bungeni. Ndio maana defections nyingi za CCM zikija, wa kufaidika watakuwa vyama kama CCK na NCCR. Naenda nje ya mada lakini mawazo yangu ndio hayo juu ya hilo.
 

The point is very clear,
linalowezekana leo lisingoje kesho. Its only february, bajeti mpya ni june kwa
ajili ya mwaka 2012/2013, sioni tatizo lolote kwenye hoja ya Zitto kama nia
ingekuwepo. Au kama Serikali ingehitaji kujipanga zaidi, marekebisho yangekuwa
kwenye mwaka tu... lakini tumeona haikuwa hivyo.

Nasikitika kukuambia mchambuzi huyo unayejaribu kumuelimisha ana ugonjwa wa
Zittophobiasis.
 
na kiwanda kilichokuwa Morogoro si hizi kimekuwa nini. Isije ikawa ni kituo cha Mabasi au bohari

Kwa mwendo wa CCM na Serikali yake, inawezekana kabisa kiwanda hicho sikuhizi ni ghala la kuhifadhi unga wa ulezi bila ya wahusika kuchukuliwa hatua kutokana na kwenda kinyume na mkataba wakati wa zoezi la ubinaifshaji.
 
Reactions: FJM
Wabunge wa CCM sasa wafike mahala pa kikomo hoja zeje tija kwa Taifa wasiziache wazishupalie kuliko kuzikataa
 

Upo sahihi kwani kimsingi Zitto stands to be correct both in content (hoja yenyewe) na context (2012); Cha ajabu ni uwendawazimu wa serikali kupinga hoja kwa kwa kujenga hoja inayobebwa zaidi na context (2012), badala ya content (umuhium wa kufufua zao hili haraka iwezekanavyo ili tupate MW 100 za umeme, tutoe ajira kwa vijana, tuongeze pato la uchumi);
 

Umenena masuala ya msingi sana ambayo kimsingi ndiyo yanatakiwa kutoa mwongozo mkubwa sana kwenye mada hii juu ya kwanini wamekwama na hatima yao ni nini katika vyama vyao na siasa za Tanzania kwa ujumla, kwa kuzingatia both, vyama husika, lakini pia the electorate.
 
Reactions: FJM
Wadau kumbukeni mashamba yote ya mkonge yalishauzwa wa wawekezaji uchwara ambao wameshindwa kuyaendeleza. Na wengine ni viongozi ndani ya serikali. Hoja hii ingepita, ingeibua madhambi mengine yaliyojificha kwenye sekta ya kilimo cha mkonge.
.

Hapo kwenye red nadhani ndio pa kuanzia. Kwanza ku-idenfity mashamba ya mkonge yalipo na nani anamiliki shamba lipi? Nahisi kuna kitu hapa sio bure!
 
siamin baba anaweza kataa neema kwa wanae ila leo baba amekataa maendeleo jimboni kwake kwa madai serikali haiko tayari ni kweli ama 'cake eaters' hawako tayari kulinda maslahi yao???
 

Kuna mambo mengi ambayo serikali ilishasema inayafanyia kazi lakini muda mwingi unapita bila matokeo kujulikana; ina maana mbunge akileta hoja juu ya jambo hilo haikubaliki?
Je hoja ikukubaliwa na kujadiliwa si serikali itakuwa imepata input nyingine katika utekelezaji!
Kwa maoni yangu hoja hizi zimehusishwa na suala la posho.
 
Wabunge wa CCM wanaongozwa na ilani ya chama chao ambayo haiwezi kumletea mtanzania maendeleo na kumtoa mwananchi kwenye lindi la umaskini.

Nenda kajisaidie ukirudi utakuwa na mawazo mazuri zaidi kwani waonyesha kuna kitu kinakusumbua

 
Wabunge wa ccm hawashindi kwa hoja bali kwa kutumia vibaya wingi wao wakisaidiwa na kinara wao Makinda. CDM endeleeni hivyo hivyo, sisi wananchi tunawasikia na kusikia na kuona hayo yanayotokea bungeni. MSIOGOPE KUPELEKA HOJA ETI HAZITAPITA. Ni kweli hazitapita, lakini kamailvyosema Mbowe jana; hoja zenu tutazipokea huku kwenye umma.
 
Shida kubwa waliyo nayo wabunge wengi wa Chukua Chako Mapema ni UVIVU WA KUFIKIRI. Hoja hizo zitakataliwa tu kwa sababu hakuna aliyejipanga kufikiri namna ya kuzichangia huko Mjengoni.

imwan
 
siamin baba anaweza kataa neema kwa wanae ila leo baba amekataa maendeleo jimboni kwake kwa madai serikali haiko tayari ni kweli ama 'cake eaters' hawako tayari kulinda maslahi yao???

nadhani una maana mbunge aliyepinga hoja ya Zitto au? Kama una maana hiyo, ni kweli, huyu mheshimiwa hajui kabisa kucheza na siasa za zama hizi, hilo jimbo ndio asahahu kabisa 2015 kwani hata kama alikuwa na hoja, kitu ambacho mimi sikukiona, mpinzani wake 2015 akifanya political spinning kidogo tu, huyu mheshimiwa atakwenda na maji.
 
Reactions: FJM
Shida kubwa waliyo nayo wabunge wengi wa Chukua Chako Mapema ni UVIVU WA KUFIKIRI. Hoja hizo zitakataliwa tu kwa sababu hakuna aliyejipanga kufikiri namna ya kuzichangia huko Mjengoni.

imwan

Hivi kweli unadhani suala hapa ni uvivu wa kufikiri kweli? Mimi sikubaliani na hilo; ni uwoga wa kupingana na serikali inayoongozwa na chama chao kwani wakicheza na hilo, majina yao kwenye kura za maoni ubunge 2015 yatakatwa; wabunge wa CCM wanakuwa na ujasiri pale tu ambapo hoja husika inakuwa imeigawanya serikali (in terms of msimamo), nusu kwa nusu huku serikali ikiwa tayari kulalia upande wowote kutegemea na upepo wa siasa, hapo ndio utabaki umeduwaa jinsi gani wabunge wa CCM wanavyokuwa mbogo mle bungeni.
 

Ni wananchi wangapi wanasikia haya mkuu. Ninavyosikia ni kwamba bunge halitangazwi tena kwenye redio, sijui kama ni kweli, ila kama ni kweli, wananchi wamebakiwa na TV tu, na je ni wangapi wanaotazama hizo TV? Otherwise the most watched programme on TV in Tanzania ni Ze Comedy,ikifuatiwa na taarifa ya habari ya saa mbili usiku. Tupo pamoja mpaka hapo?
 
hoja ya makamba ni contradicting, wote twajua gharama za ujenzi zilivyo juu, na watu wengi hukopa ili kujenga, leo hii utamwambia nin mtu huyu eti kodi ni ya miezi 2 tu maximum...

Nakubaliana na ww kabisa hoja ya Makamba haina mshiko na haiwezi kupita asilani, kwa nini mtu nyumba yako uweke wapangaji si bora uiweke stoo, au uweke kabisa Guest hela utaiona kuliko kupangiwa kodi ya kumtoza mpangaji na kwenda lipa TRA viwanja vinatolewa watu hawavifuatilii lawama iende serikalini, wao ndio wajenge nyumba ili ziwatosheleze wananchi wote
mfano miji ya Kigoma, Kondoa, Bagamoyo, Tanga, Korogwe, Lushoto ukijenga nyumba ww maisha yako yapo hatarini.
Kwa nini miji yote ya mijini watu wanawekeza katika majengo? (maguest, maduka mahoteli na nyumba za kupanga) na hata ukienda Mkoa wa kagera Mbeya Kilimanjaro zipo nyumba tele vijijini zinazoachwa wazi mwaka mzima baada ya mwenyeji kuja mara moja kwenye likizo kwa hiyo asipangishe ili mtu aiweke katika usafi sasa kwanini muwalazimishe kuwapangia kodi
Makamba hapo kachemsha bora Zitto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…